Wanaotaka wengine walipe kodi hawana biashara, na hawajui uchungu wa kulipa kodi

MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
500
Habari zenu wote humu ndani wakuu, nimejaribu kutafakari kwa kina, na kuwaza juu ya ulipaji kodi hapa nchini kwetu, na kubaini wale wafanyakazi karibu wote wa TRA, Na mamlaka nyinginezo za ushuru na kodi. Hawana uzoefu na biashara wanazo toza kodi au mapato.

Nimeona niandike ili nao waweze kusoma na kufanya tafiti za kutosha juu ya mwenendo wa biashara zetu, zote na za madaraja yote. Kwa mfano; gharama halisi za uendeshaji biashara hizo. Aina ya biashara inayotakiwa kulipa kodi au mapato. Na pia sehemu biashara ilipo.

Zipo biashara zina kodi zaidi ya moja na uendeshaji wake ni mgumu kulingana na faida inayopatikana.

Mfano namba moja ni biashara ya daladala au gari za biashara. Biashara ile ina kodi nyingi pamoja na faini zisizo na maana angali ni biashara inayotoa huduma kwa jamii.

Ningeshauri biashara zote ziangaliwe upya kwa jinsi ambavyo wananchi wanavyo nufaika na huduma zake; halafu zipewe unafuu wa kodi na si kuzikamua kiasi kwamba huonekana si biashara yenye kumwinua mwananchi tena.

Kuna Tra hupata sehemu ya mapato kutoka ktk vyombo hivi vya usafiri, kuna Trafic nao faini wanazopiga; hutokana na faida ya biashara hii; kuna Sumatra, nao faini zao hutokana na faida ya mapato ya biashara hii. Zaidi kuna kodi serikali inazo pata kutoka ktk Mafuta; spea; n.k.

Ukitazama kwa makini hii imegeuka kuwa biashara inayo kimbiwa na watu wengi kwa kasi kwa kuwa inajiendesha kwa hasara sana.

Tuna shauri serikali na vyombo husika vinvyo itazama sekta hii ya biashara usafiri kuifikiri upya ktk swala la kodi; na mambo mengine kwa kuwa ni sekta muhimu ktk jamii yetu.

Ikiwezekana, TRA wanunue mabasi ya kutoa huduma kama hii, kwa muda ili waweze kufanya utafiti wa kutosha namna bora ya kuiokoa nayo iwe sehemu ya biashara yenye faida.

Zipo biashara nyingi zenye makodi mengi kama vile baa na hotel. Lakini leo nimeona nisemee ile biashara ninayoijua kwa undani.

Naomba kuwasilisha kwenu nami nipate maoni yenu. Pia unaweza kuanisha ni biashara ipi unafikiri ingekuwa vyema mamlaka yetu ya Mapato ingeingalia upya ktk kurekebisha kodi zake ziwe ndogo zenye kunufaisha pande zote mbili?
 
MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
500
wafanyabiasha kwa sasa wanafanya tu ilimradi siku zisonge mazingira ya biashara kwa Tanzania ni magumu sana TRA wamekuwa kama wahujumu wa biashara!!?
Mm nahisi kwa kuwa hawana biashara yoyote; ama wale wafanyakazi wao kutokuwa wafanyabiashara, kunachangia wao kutokujua vyema ugumu wa biashara zenyewe. Ni sawa na mtu anaye fanya jambo kwa nadharia na si vitendo.
 
knowledge quench

JF-Expert Member
Nov 4, 2017
227
250
Kwani unalipa kutoka katika mfuko wako???
UCHUNGU WAKURUDISHA FEDHA TULIZO LIPA WAKATI WAKUNUNUA HIZO BIDHAA ZAKO!!!!
ACHA WIZI RUDISHA FEDHA ZETU KUPITIA TRA!!!
TUPATE HUDUMA STAHIKI KUTOKANA NA HIZO FEDHA ZETU!!! UNAZO ONEA UCHUNGU KURUDISHA!
 
sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
4,485
2,000
Kodi ni muhimu,LAKINI,utilili wa kodi ni kikwazo kikubwa cha kuingizia serikali mapato yakutosha.
Bado kuna taasisi ambazo ni duplicate kwa mfano traffic na Sumatra wanafanya kazi mmoja,hamishia kazi za sumatra traffic itapendeza zaidi.
Pammoja na TRA kuna mamia ya kodi zisizo rasmi zikikusanywa na serikali za mitaa,shule,harambee n.k.
 
mtanzania1989

JF-Expert Member
May 20, 2010
2,966
2,000
Acha ubinafsi, lipa kodi. Wafanyakazi na vimishahara vyao kidogo wanakatwa kila mwezi, wewe ni nani usilipe. Halafu kwa nini unaweka faini za Traffic na Sumatra kama sehemu ya kodi, kama hutaki hizo faini si ufuate masharti tu.
 
Copenhagen DN

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
6,057
2,000
Taifa Hili liendelee lazima kuwe Na utawala Bora wa katiba Na sheria Na pia utawala was sheria.

Baada ya hapo wananchi wengi wanaotakiwa waajiriwe siyo wananchi wengi wafingue biashara iyo haiwez kuleta uchumi mzuri. Ajira zikiwa nyingi
 
MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
500
Kwani kodi si analipa mlaji wa Mwisho? Ama? Tuelimishane wajuvi!
Si kwa Tz; mlaji wa mwisho hamkadirii bali wakala mkusanyaji ambaye ni mfanyabiasha. Hawana kuangalia kipato cha mwenye biashara anachoingiza. Wanachanja hadi mtaji na si faida itokanayo na biashara.
 
MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
500
Kwani unalipa kutoka katika mfuko wako???
UCHUNGU WAKURUDISHA FEDHA TULIZO LIPA WAKATI WAKUNUNUA HIZO BIDHAA ZAKO!!!!
ACHA WIZI RUDISHA FEDHA ZETU KUPITIA TRA!!!
TUPATE HUDUMA STAHIKI KUTOKANA NA HIZO FEDHA ZETU!!! UNAZO ONEA UCHUNGU KURUDISHA!
Tunarudishaje ambacho hamjakinunua? Nunueni kwa faida tulipe tukiwa kama mawakala wa ukusanyaji kodi. Nauli unayolipa kwenye chombo chochote cha usafiri hatujakuwekeni gharama za vipuri; gaharama za faini n.k.

Kama endapo mpo tayari nauli kipanda itapendeza zaidi ili tuweze kukusanya kodi kwa uwiano stahili.
 
MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
500
Kodi ni muhimu,LAKINI,utilili wa kodi ni kikwazo kikubwa cha kuingizia serikali mapato yakutosha.
Bado kuna taasisi ambazo ni duplicate kwa mfano traffic na Sumatra wanafanya kazi mmoja,hamishia kazi za sumatra traffic itapendeza zaidi.
Pammoja na TRA kuna mamia ya kodi zisizo rasmi zikikusanywa na serikali za mitaa,shule,harambee n.k.
Kweli mkuu; umenena haswaa.
 
MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
500
Acha ubinafsi, lipa kodi. Wafanyakazi na vimishahara vyao kidogo wanakatwa kila mwezi, wewe ni nani usilipe. Halafu kwa nini unaweka faini za Traffic na Sumatra kama sehemu ya kodi, kama hutaki hizo faini si ufuate masharti tu.
Masharti tunafuata; kodi kwa wafanyakazi ina afadhali kubwa kuliko wafanyabiashara. Na mfanyakazi yoyote ana uhakika wa kudaka mwisho wa mwezi, tofauti na biashara unapotoka asubuhi; hujui kama biashara itafanyika ama la. Inakuwa bahatisha ndulute.
 
knowledge quench

JF-Expert Member
Nov 4, 2017
227
250
Tunarudishaje ambacho hamjakinunua? Nunueni kwa faida tulipe tukiwa kama mawakala wa ukusanyaji kodi. Nauli unayolipa kwenye chombo chochote cha usafiri hatujakuwekeni gharama za vipuri; gaharama za faini n.k.

Kama endapo mpo tayari nauli kipanda itapendeza zaidi ili tuweze kukusanya kodi kwa uwiano stahili.
FAINI!!! LOH! HUNA HATA AIBU! MAKOSA YAKO TULIPE SISI, KULIKONI!!!
 
MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
500
Taifa Hili liendelee lazima kuwe Na utawala Bora wa katiba Na sheria Na pia utawala was sheria.

Baada ya hapo wananchi wengi wanaotakiwa waajiriwe siyo wananchi wengi wafingue biashara iyo haiwez kuleta uchumi mzuri. Ajira zikiwa nyingi
Kweli kabisa ajira za hakika ni njia bora ya kuimarisha uchumi kwa nchi yoyote ile duniani.
 
Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
9,995
2,000
Kwa kweli jamaa wanashida sana cheki importatition ya magari kuna kitu kinaitwa excise duty due to age sasa ulizia tangu ianzishwe je? Imepunguza kiwango cha ununuzi wa magari chakavu? Hakuna kitu kama hicho
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
3,182
2,000
Habari zenu wote humu ndani wakuu, nimejaribu kutafakari kwa kina, na kuwaza juu ya ulipaji kodi hapa nchini kwetu, na kubaini wale wafanyakazi karibu wote wa TRA, Na mamlaka nyinginezo za ushuru na kodi. Hawana uzoefu na biashara wanazo toza kodi au mapato.

Nimeona niandike ili nao waweze kusoma na kufanya tafiti za kutosha juu ya mwenendo wa biashara zetu, zote na za madaraja yote. Kwa mfano; gharama halisi za uendeshaji biashara hizo. Aina ya biashara inayotakiwa kulipa kodi au mapato. Na pia sehemu biashara ilipo.

Zipo biashara zina kodi zaidi ya moja na uendeshaji wake ni mgumu kulingana na faida inayopatikana.

Mfano namba moja ni biashara ya daladala au gari za biashara. Biashara ile ina kodi nyingi pamoja na faini zisizo na maana angali ni biashara inayotoa huduma kwa jamii.

Ningeshauri biashara zote ziangaliwe upya kwa jinsi ambavyo wananchi wanavyo nufaika na huduma zake; halafu zipewe unafuu wa kodi na si kuzikamua kiasi kwamba huonekana si biashara yenye kumwinua mwananchi tena.

Kuna Tra hupata sehemu ya mapato kutoka ktk vyombo hivi vya usafiri, kuna Trafic nao faini wanazopiga; hutokana na faida ya biashara hii; kuna Sumatra, nao faini zao hutokana na faida ya mapato ya biashara hii. Zaidi kuna kodi serikali inazo pata kutoka ktk Mafuta; spea; n.k.

Ukitazama kwa makini hii imegeuka kuwa biashara inayo kimbiwa na watu wengi kwa kasi kwa kuwa inajiendesha kwa hasara sana.

Tuna shauri serikali na vyombo husika vinvyo itazama sekta hii ya biashara usafiri kuifikiri upya ktk swala la kodi; na mambo mengine kwa kuwa ni sekta muhimu ktk jamii yetu.

Ikiwezekana, TRA wanunue mabasi ya kutoa huduma kama hii, kwa muda ili waweze kufanya utafiti wa kutosha namna bora ya kuiokoa nayo iwe sehemu ya biashara yenye faida.

Zipo biashara nyingi zenye makodi mengi kama vile baa na hotel. Lakini leo nimeona nisemee ile biashara ninayoijua kwa undani.

Naomba kuwasilisha kwenu nami nipate maoni yenu. Pia unaweza kuanisha ni biashara ipi unafikiri ingekuwa vyema mamlaka yetu ya Mapato ingeingalia upya ktk kurekebisha kodi zake ziwe ndogo zenye kunufaisha pande zote mbili?
Mkuu nikiazima maneno ya rais mstaafu mh. Mkapa ni "wapumbavu na malofa peke yao" wanaoweza kubeza hoja yako.

Ni tatizo kubwa sana wafanya biashara kutoshirikishwa vilivyo katika ukusanyaji wa takwimu ili mamlaka husika ziweze kufahamu operational issues. Kungekuwa na nia njema ilikuwa ni muhimu kuwashirikisha wahusika ili kupata ufahamu kamili na si kuzingatia nadharia pekee katika mamlaka hizi: TRA, SUMATRA na hata hata huko polisi.

Lakini sasa kwa sababu nia njema haipo hivi hata biashara zote zikifa na watu wakaishi kama mashetani kwani kuna madhara gani? Mawazo ya kimasikini kabisa yasiyo kuwa na tija katika jamii yoyote iliyo staarabika.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom