onjwayo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 1,342
- 1,300
Hivi majuzi Kuna tamko limetolewa kufungwa kwa ubalozi wa Denmark.
Sisi kwa macho ya haraka tunaona Kama Ni tishia mtoto Tena 2024 halafu tunajisemea kuwa acha waende kainchi kamoja hako.
Tunajipa matumaini kwa sababu tuna kiburi Cha kuweza kuwatoza wananchi wetu tozo lukuki tutakavyo tukajenga shule bila ya misaada ya mabeberu.
Tunaweza kuongeza chochote kwa sababu wabunge wote tumewaweka bungeni kuruhusu na kupitisha chochote kilicholetwa na serikali bila ugumu sababu wote Ni CCM. Kama nchi hatujapata dira Kama taifa. Mipango yetu Ni ya zimamoto. Leo tutakuwa na hili kesho like ilimradi tunajisogeza Kama kibarua aishivyo.
Kauli ya kufunga ubalozi wa Denmark unakuja baada ya nchi hiyo kupitia diplomasia wao kutoridhishwa na utawala wetu wa Sheria.
Ni kweli Kama nchi kuingiliwa kwenye Mambo yetu ya ndani Ni kosa. Lakini pia Kama nchi tumewaachia jeshi letu kufanya propaganda na maisha ya kisiasa nchini.
Jeshi linatumia nguvu kubwa mno kudhibiti upinzani. Jeshi linatekeleza kwa 100% katazo la serikali
Kauli ya mtu moja kuzuia na kudhibiti shughuli zote za kisiasa bila kuona katiba inasemaje.
Wanaojitokeza wanashughulikiwa kwa nguvu kubwa pamoja na kuwaweka mahabusu na kuwabambikiza vyesi vingi.
Mahakama imekuwa sehemu ya jeshi na serikali kuonyesha uonevu huu.
Juzi Kuna katazo ya wanadiplomasia kutoruhusiwa kuhudhuria vyesi vinavyowahusu wanasiasa wetu wa juu toka upinzani. Tafasiri ya hili Ni kuwa pengine wanahofu ya kujulikana hila zao na namna wanavyotumika polisi kuhujumu upinzani.
Mitaani akili zimeanza kubadilika kufuatia tukio la juzi. Hamza pamoja na tukio lake bovu lakini amepata watetezi . Iweje raia waanze kupishana na polisi , Kuna wanaoshangilia polisi kuuwawa, hii unaleta picha gani.
Polisi kwa upande wao wanajisikiaje? Huu mpishano ndio unaowapa mashaka balozi zetu kwa kutumia vyanzo vyao kuwa in the long run pengine hii nchi ikaingia katika sintofahamu.
Tukio la mtu anaelezwa na majirani na wengi wanaomfahamu, Hamza kuwa mpole na kugeuka kufanya yote in a no time s lisipuuzwe hata kidogo.
Juzi Rais aliongelea kuhusu polisi kuua na kutumia nguvu kubwa kabla ya kumfikisha mtu mahabusu. Sirro kwa upande mwingine alisikika kuubeza wito wa amiri jeshi mkuu wake.
Polisi wakiendeylea hivi tutatengwa. Polisi ndio kimbilio la mwisho. Kuna makaka Fulani YouTube inaweka wazi uonevu wa jeshi hili kwa raia wema .
Rais aisiishie kukemea tu Bali abadilishe uongozi wa jeshi hili na kulisuka upya kiweledi na kuipa karipio. Hii nguvu ya polisi kuingia kwenye siasa na kuisaidia CCM itatufikisha pabaya. Leo Ni Denmark, marafiki wa kipindi kirefu, je, kesho Nani?