Elections 2010 Wanaotaka kuhama waende ikiwezekana tutawasindikiza - Msekwa

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Chama cha Mapinduzi-CCM kimesema mwanachama yeyote wa chama hicho aliyeshindwa katika uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani anayeona ni vizuri akahamia chama kingine cha siasa, anaruhusiwa kufanya hivyo, imeelezwa.

Chama hicho kimesema hakitaathiriwa na hatua ya wanachama wake wasioridhika na uamuzi wa vikao vyake vya juu na hivyo kinatoa baraka zote.

Akizungumza na gazeti hili jana akiwa Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, alisema iwapo kuna mwanachama anayetaka kuhama kwa kisingizio cha kushindwa kuteuliwa na afanye hivyo na ikiwezekana chama kitamsindikiza.

"Waende … waacheni waende nasi tutawasindikiza. Kwanza kuondoka kwao ni sawa na kuchota ndoo moja au mbili za maji Mto Rufiji, kwani maji yake kamwe hayatapungua, yatabaki vilevile kwa hiyo waende tu," alisema Msekwa.

Source: Habari Leo

My take; Ina maana CCM imetosheka kiasi hicho hata haioni hasara kuondokewa na wanachama wake kama huku si kufuru ni nini. Nafikiri kazi mojawapo ya chama ni kuongeza wanachama naona hapa Msekwa kateleza kidogo.
 
Hajateleza ndugu yangu. Hiyo ndiyo sera ya CCM kwa sasa. Mwenyekiti wa Chama hataki kura za wafanyakzi, na sasa Makamu anafukuza wanachama kuwa hawahitajiki. Subiri Katibu Mkuu naye atatoka na la kwake.

Asiyejua ubaya kiuno, hukigeuza mto wa kulalia!
 
Wakati mwingine viongozi wetu huwa wanasema bila kuangalia athari za matamko yao, nilitegemea wakati huu watajitahidi kutibu majeruhi badala yake wanazidi kupigilia misumari kwenye vidonda ambavyo bado ni vibichi kabisa, wazee wetu hawa si bure kuna wanachokitegemea.
 
Hawa watu wanajigamba namna hii kwa sababu gani? wanasahau wanaccm ndio walipiga kura za maoni kupata wagombea wao sasa wanategemea wao kuja na vitisho watawabakiza hao wanachama wawapigie kura wale ambao hawakuwachagua.. ccm mna njozi kweli mnafikiri sisi ni wendawazimu sasa mwaka huu kitaeleweka mmetuchosha tumewachoka
 
wenye uchu wa madaraka ndo waondoke...wanaodhani kuwa bila wao chama hakipo hawafai........kuna baadhi ya vyama miaka 15 wagombea ni hao hao havifai ...uchaguzi kuna kushinda na kushindwa...wanaotaka kushinda tu HAWAFAI....!
 
Ni vyema wanachama hao wakaonesha msimamo wao kwa kutekeleza kauli ya Pius.
 
wenye uchu wa madaraka ndo waondoke...wanaodhani kuwa bila wao chama hakipo hawafai........kuna baadhi ya vyama miaka 15 wagombea ni hao hao havifai ...uchaguzi kuna kushinda na kushindwa...wanaotaka kushinda tu HAWAFAI....!

Kweli ccm kama ni kiburi mnacho. sawa bwana
 
Chama cha Mapinduzi-CCM kimesema mwanachama yeyote wa chama hicho aliyeshindwa katika uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani anayeona ni vizuri akahamia chama kingine cha siasa, anaruhusiwa kufanya hivyo, imeelezwa.

Chama hicho kimesema hakitaathiriwa na hatua ya wanachama wake wasioridhika na uamuzi wa vikao vyake vya juu na hivyo kinatoa baraka zote.

Akizungumza na gazeti hili jana akiwa Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, alisema iwapo kuna mwanachama anayetaka kuhama kwa kisingizio cha kushindwa kuteuliwa na afanye hivyo na ikiwezekana chama kitamsindikiza.

"Waende … waacheni waende nasi tutawasindikiza. Kwanza kuondoka kwao ni sawa na kuchota ndoo moja au mbili za maji Mto Rufiji, kwani maji yake kamwe hayatapungua, yatabaki vilevile kwa hiyo waende tu," alisema Msekwa.

Source: Habari Leo

My take; Ina maana CCM imetosheka kiasi hicho hata haioni hasara kuondokewa na wanachama wake kama huku si kufuru ni nini. Nafikiri kazi mojawapo ya chama ni kuongeza wanachama naona hapa Msekwa kateleza kidogo.

Hayo ni maneno ya mfamaji na mkosaji......TIME WILL TELL
 
Daaaaaaaaa kumbe hata matamko ya kiranja mkuu kwa wafanyakazi yametoka CCM?

Nyodo ni sera namba moja ya CCM ya kutojali wanachama/wananchi wake.Jamani jamani mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio haambiwi sikia, wakati wa mabadiliko ni sasa.

Leo asubuhi nimesikia Makamba akisema Bashe sio raia licha ya kupatikana udhibitisho wa barua toka uhamiaji na hata Chiligati kasema hakuna jungu, nauliza je? siku zote hawakujua mpaka kapata vyeo kibao CCM wajue leo? Je si majungu hayo?

Bashe ndugu yangu na wanaCCM mliopigiwa zengwe, CCM hawawahitaji wala kuwajali, mmekuwa reject njoo CHADEMA sisi tunawajali na kuwapenda sana, njooni tujenge upinzani wa kweli ili tuiangushe serikali ya CCM.
 
Jeuri ya CCM, wanajua mtaji wao ni Ujinga na Umaskini wa Mtanzania
 
wenye uchu wa madaraka ndo waondoke...wanaodhani kuwa bila wao chama hakipo hawafai........kuna baadhi ya vyama miaka 15 wagombea ni hao hao havifai ...uchaguzi kuna kushinda na kushindwa...wanaotaka kushinda tu HAWAFAI....!
Mwakalebela hakushinda?, Bashe na Sellelii hawakushinda?..............wananchi sio wajinga kiivo!!! you wait and see!
 
Naunga mkono kwa dhati kauli ya MSEKWA. Hii anataka kuwaonyeshaa kuwa wale wanaotaka kuondoka CCM hawana haja ya kutishia nyau..WAONDOKEE TENA NI WATU WAZIMA KABISAA...SLAA ALIPOONDOKAA CCM HAKULIALIA KAMA SHIBUDA!!!
 
Hebu nyote mlo ambiwa hivo fanyeni kweli maana CCM wanasema hayo wakihisi kuwa kwa kusema hivo mtaogopa! Waonesheni kuwa mnao msimamo na njooni kwetu CHADEMA. Msije juta pale nchi itakapokuwa mikononi mwetu!
 
wenye uchu wa madaraka ndo waondoke...wanaodhani kuwa bila wao chama hakipo hawafai........kuna baadhi ya vyama miaka 15 wagombea ni hao hao havifai ...uchaguzi kuna kushinda na kushindwa...wanaotaka kushinda tu HAWAFAI....!
Mbona Athman Ramole wa Moshi Mjini alishinda ameenguliwa na kuchukuliwa aliyeshika nafasi ya tatu Justine Salakana nyuma ya Ngawaiya, nasikia hata huko Moshi Mjini kunawaka moto sijui kwa kitendo hicho CCM itaweza kumtikisa Ndesamburo.
 
Msekwa ni kiongozi makini sana, naamini katika aliyosema na anajua kuwa chama chake ni zaidi kuliko wagombea walioshindwa! pia msekwa anajua uoga wa wanasiasa watanzania! anajua kuwa umaarufu wa wanasiasa wengi akiwemo yeye wameupata kutokana na uimara wa chama chao, kwa hiyo asingependa chama chake kibabaishwe na upepo wa uchaguzi. alichosahau ni nguvu iliyoko CHADEMA na mgombea wao wa urais!
 
Hatukatai Msekwa ni makini kwani JK alipozikataa kura za wafanyakazi hakuwa makini, na yeye alijiridhisha kabisa ni makini lakini sasa zinamgeuka nasikia anazitaka tena. Hata huyu kuna wakati atawakumbuka hawa anaowaambia atawasindikiza, tumpe muda.
 
Hawa watu wanajigamba namna hii kwa sababu gani? wanasahau wanaccm ndio walipiga kura za maoni kupata wagombea wao sasa wanategemea wao kuja na vitisho watawabakiza hao wanachama wawapigie kura wale ambao hawakuwachagua.. ccm mna njozi kweli mnafikiri sisi ni wendawazimu sasa mwaka huu kitaeleweka mmetuchosha tumewachoka

wataiba kura ndio sababu
 
Back
Top Bottom