kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,418
- 7,206
Kuna watu wabinafsi na walaku wa mali kupindukia ambao badala ya huo ulaku na ubinafsi kuutumia kutafuta mali zao wanafikiria kupora mali za umma.
Ubinafsishaji wa mashirika mengi ya umma ulifanyika awamu ya mkapa. Yapo yalibinafsishwa vizuri na yapo mengi vigogo waliyapora wala hawakuyaendeleza badala yake wakakopea fedha kutoka mabenki na kugeuza majengo bohari au kutelekeza hivyo viwanda.
Kuna mashirika ubinafsishaji ulishindikana kutokana na ukubwa wake uwekezaji uliyofanyika na serikali na aina ya huduma na pia yanahusika na usalama au uhuru wa nchi yetu.
Kuna majaribio yalifanyika kubinafsidha mashirika kama hayo taifa likaishia kutapeliwa na kuibiwa bila wala kupata ufanisi wowote. Mwisho wake ikawa serikali kuyarejesha mashirika kama hayo kwenye uthibiti wa serikali.
Mfano wa mashirika kama hayo kwa siku za karibuni ni tanzania sisal corporatio ambalo uchunguzi ulionyesha liliporwa tu wala halikununuliwa. Kuna ttcl ambapo mnunuzi wa hisa alifanya ubabaishaji tu na kupora kampuni ya shirika hilo ya simu za mikononi celltell. Wala hakuongeza ubora wowote. Kuna tanesco tuliweka muendeshaji kutoka afrika kusini. Hakika hakuongeza thamani yoyote zaidi kulichuna shirika tu. Kuna shirika la reli trc. Huu ubinafsishaji ulikua wa ovyo tu na kuigeuza nchi tegemezi. Eti servive ya vichwa ikawa vinapelekwa india wakati tuna karakana kabambe dar morogoro na tabora. Wahindi wakauza majengo na assets chungu mzima za reli hadi walivyotimuliwa. Kuna ule mradi wa kuzalisha umeme kwa makaa ya mawe mbeya. Nako tulipigwa hadi imebidi kurejeshwa serikalini.
Kwanza tujue kuna vitu ukibinafsisha hasa kwa wageni ni hatari kwa usalama na uhuru wa nchi. Kuna shughuli ndio mhimili wa maendeleo ya nchi. Ni mambo matokeo yake ni ya muda mrefu. Muwekezaji binafsi hawezi kua na malengo sawa na serikali. Vinginevyo hiyo serikalu haina maslahi ya wananchi wake.
Mashirika mhimili wa uchumi kama ttcl tanesco trc atcl na mengine kama ya maji etc sio mambo ya kubinafsisha kiholela. Vinginevyo ltakua kupigwa na wajanja wanaoshirikiana na wageni. Ni ujinga kuumwa na nyoka mara ya pili hadi tatu. Vinginevyo umma wataamua hili wimbi la wahuni kurejeshwa kuongoza tena.