Wanaotaka kuanza kusoma CPA, karibuni tushauriane

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
11,799
2,000
Duh aisee ule mziki wa cpa sijawahi ona, ulinipeleka mchaka mchaka mno hata nikiunganisha msuli wa form 6 na degree bado haifiki hata nusu.

Sitting ya kwanza nilifanya May huku nimelipia tuition centre / review classes, nikitoka kazini naenda centre huku nimechoka balaa, kwa misifa nilichukua masomo 6, aisee nlikula za ovyoo ovyo usoni nikafaulu somo moja tu la B6 (hili somo jepesi kuzidi yote ni kama civics), nilitamani kulia!!, hata hivyo matokeo hayakunishangaza maana nilikuwa nikifika centre nimechoka sana kufatilia kwa umakini kipindi, nkirudi home nina majukumu ya kifamilia, n.k

Sitting ya pili nikaona wacha nijisomee kivyangu tu nikaona centre inanibana nikawa private candidate nikachagua masomo yangu manne tu, ikawa ni mwendo wa kusolve past papers za bodi yetu na nchi nyingine ((acca, cima, cpa ireland, cpa ghana, cpa nigeria, ca india)), maswali ya vitabu, kula pindi youtube videos, google, n.k yani msuli wa notes asilimia 30 na msuli wa kusolve pepa asilimia 70, nilipiga pepa 4 nikachomoa zote B5 baba lao, B1 mama mwenye nyumba, b3 na b2. hiki kipindi nlikuwa naamka saa 10 nasukuma kalamu hadi saa 12 na nusu, computer ya kazini niliijaza pdf za maswali ya kutosha, saa 11 na nusu jioni nafika home nakaa hadi saa 12 na robo ivi naenda kasehemu karibu na home napiga piga msuli hadi saa 3 narudi home, weekends jumamosi na j2 saa 7 mchana hadi saa 10 then misele ya hapa na pale, jamani hiki kipindi sitasahau, hadi hapa nilipo nakumbuka formula za variance analysis topic ya b5.

baada tu ya kumaliza pepa za sitting ya pili nliliyofanya, sikubweteka kwamba nianze kusoma january baada ya matokeo kutoka, nilianza kusoma b4 na c4 yanayohusu tax huku nasubiria matokeo ya masomo niliyofanya, baada ya takribani miezi miwili matokeo yalipotoka, tayari nilikuwa mbali sana kwenye haya masomo niliyoanza kusoma mapema, yani nlikuwa nmebakiza topics chache fupi fupi huku zile ngumu nimeshazielewa nasolve tu maswali, hii mbinu ilinisaidia mno kubalance ratiba yangu kwenye sitting inayofata na kunipa ahueni ya kupunguza msuli.

sitting ya tatu ya may mwaka ujao nikafanya masomo manne ...ya final level matatu c1, c2, c4 na kiporo kimoja cha intermidiate b4, nilifaulu yote!! unajua kwanini ?? c4 na b4 masomo ya tax nilianza kusoma mapema mno kama nilivyoweka wazi hapo awali, kwa hio nikawa nimepunguza mzigo, ikawa na deal sana na c1 na c2 ambayo nayo hayakua mapya sana maana hilo c1 ni kaka mkubwa wa b2, c2 ni kaka mkubwa wa b3, na c4 nae wanashare vitu na b4, c4 sijamwita ni kaka kubwa wa b4 sababu c4 ina vitu vichache sana hata kitabu chake ni kidogo kuzidi vitabu vyote vya cpa, ndio somo jepesi zaidi kwa final level. hii sitting nlikuwa nasoma lisaa limoja asubuhi na usiku mawili, sio kama msuli tembo niliowekea sitting iliyopita 😂😂.

sitting ya mwisho novemba hapo sasa nikawa nimebakiza somo moja tu la C3, mfalme wa wafalme, huyu mjinga ukienda kichwa kichwa anakupa kichapo heavy na hana undugu na masomo mengine kama wenzake kina c1, c2 na c4, ikawa kila siku jioni masaa mawili nampapasa yeye tu 🤠, siku ya mtuhani ikafika nikafanya pepa na nikaimaliza nikiwa nina uhakika nishamakiza game, matokeo yalivyotoka nilifurahi sana kutua mzigo huku machozi yakinilenga kwa furaha, wife alipika msosi wa maana sana.

graduation sikwenda, ratiba zilinibana

niliacha kazi private baada ya jambo kutiki serikalini

nilimaliza cpa ila moto ilionipelekea siji sahau

CONCLUSION:

-Wahi kuanza kusoma cpa kabla ya majukumu mengi, ukimaliza tu chuo we unganisha.

-Kama umeamua kusoma cpa uwe umemaanisha, Cpa haisomwi kilelemama, cpa inahitaji jitihada kubwa mno, watu wengi hukatisha safari zao za cpa kwa kukata tamaa baada ya kufeli mara kwa mara ama sheria za bodi kuwalazimu kuacha, hivyo usitegemee kusoma cpa kama unavyosoma chuoni, huku mtu kufaulu somo inabidi upate alama ya C inayoanzia maksi 40 na hapo bado ni shughuli pevu inakubidi utie bidii, kuhusu kupata B ni nadra sana maana wanaozipata ni takribani asilimia moja tu ya watahiniwa, kuhusu alama A ni kama muujiza maana binafsi nimewahi kuiona moja tu kati ya maelfu ya watu wanaofanya mitihani hii.

-Solve sana maswali kuliko kusoma notes, solve maswali ya pastpapers ya Tz, ireland, india, nigeria, cima, acca, n.k

-fanya walau masomo manne manne ili kupata timetable nzuri na concetration kubwa.

-usifatilie matokeo ya wenzako unaweza kukata tamaa na kuwa jealous, binafsi sitting yangu ya kwanza nlipofanya masomo 6 na kufaulu 1 tu kuna wenzangu walifaulu manne, ila hadi navyohitimu walikuwa hawajamaliza maana kuna masomo yalikuwa yamewabana wanarudia hadi mara 3 ngoma inadunda, kiufupi kuwahi kuanza ku clear masomo mengi usimcheke yule ambae kafaulu moja au kafeli yote


-Mitihani ya may inakazwa sana kuliko novemba, tumia nafasi za novemba vizuri
Aisee ahsante sana kwa kushare na sisi hili, CPA si mchezo mimi nimeanzia foundation balaa lake + kazini +majukumu mengine🤔
 

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
11,799
2,000
Hello, hiyo exemption wamekupa kwasbb ulisoma degree ya banking au? So unatarajia kufanya mtihani nov?

Ni mitihani ya masomo gani ambayo utafanya?
Hi mkuu! Ndiyo nimepewa exemption ya 4 out of 6 subjects sababu nilisoma Banking kidogo kuna masomo tulisoma kabisa, ila natakiwa kufanya 2 subjests Cost Accounting na Financial Accounting(A3 and A4). Ntafanya Nov.

Exemptions wanaangalia kama kuna masomo mlisoma chuo nk.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom