Wanaotafuta Utajiri wa Punje za Mahindi na Jogoo, Imekaaje Hii?

Utajiri wa masharti ni bora kufa masikini tu uishi kwa amani, siyo kumhofia jogoo kala nusu punje dah.

Ila bado siamini kama ni kweli kuna hayo mambo ya utajiri na jogoo, how? Utajiri unaletwa kwa kupiga kazi tuu.
Believe or not,no impossible under the sun!
Maisha ni kuchagua tu uwe masikini wa kutupwa,ujimudu wastani au tajiri wa kutupwa ni maamuzi yako,muda fulani hata damu yako (kifo chako) yaweza kuwa ndio jasho lako. Chagua moja kusuka au kunyoa mkuu
 
Believe or not,no impossible under the son!
Maisha ni kuchagua tu uwe masikini wa kutupwa,ujimudu wastani au tajiri wa kutupwa ni maamuzi yako,muda fulani hata damu yako (kifo chako) yaweza kuwa ndio jasho lako. Chagua moja kusuka au kunyoa mkuu
Hee hadi umesema under the "son" badala ya sun ila umeeleweka. Kiukweli mimi ntapambana kihalali kabisa bila kuhusisha hayo mambo meusi, nataka utajiri wa kujimudu tu na familia na jamii yangu ikiwezekana, Mungu wetu ni wa neema atabariki kazi za mikono yetu.
 
Typing error mkuu,shukrani chief kwa kunielewa,unaogopa sana utajiri wa punje eeh! Unaikana nafsi tu maisha yanaenda,na masharti kama yote unakula ngumu tu
 
Secret Societies zipo nyingi na mojawapo ni Freemasonry. Hizi za West Africa nyingi ndiyo zilizo waongoza Wafalme katika utawala.

Hata Wakoloni kutawala bara la Afrika haikua rahisi. Wafalme walielekezwa mbinu za kupambana kutoka kwa mizimu.

Ninaamini Wazungu walitumia uchawi pia kuweza kututawala.
👍👍
 
Typing error mkuu,shukrani chief kwa kunielewa,unaogopa sana utajiri wa punje eeh! Unaikana nafsi tu maisha yanaenda,na masharti kama yote unakula ngumu tu
Yaani kuikana nafsi hapo ndiyo pagumu, utajiri wa masharti mara usile kuku, usilale kitandani, usivae viatu dah utajiri gani huo sasa, hujakaa sawa kuku kadonoa punje 1 yaani 1 aisee ntampiga huyo kuku na huyo mganga wake😂😂
 
Haijawahi kutokea kula ata punje 10...wenye bahati 8-5...mganga Ni dalali ndio maana hukuti ampe ndugu yake utajiri wa hivo yeye anategemea ufanikiwe umpe fadhila...na Yule jogoo Ni jini ndio unaeingia nae mkataba...na ndo Mana akishakula punje anapotea ..akishapotea jua anakua mwilini mwa muhusika Sasa kumtimizia mahitaji yake ya utajiri..na ikifika siku huyohuyo ndo atamuondoa...that's why Kuna wahuni miaka ya nyuma walikua wanaenda kutegua kigoma hiyo ya deadline ya kufa...
Duh....,
 
Na walikuwa wanafanikiwa chief kutegua?
 
Story ya uyu jamaa nimeifananisha na zile msg "binamu mpigie huyu mganga alinisaidia nikapata utajiri wa magari sjui nyumba na nini, maana ukitafakari hawana sehemu ya kuongelea adi waje kuongelea sehemu watu wanapita ili wawasikie?
Pengine tayari ameshaibiwa.
Nakumbuka story za jamaa yetu mmoja enzi hizo boarding ameuziwa chupa akidhani almasi.

Alikuja kutupa story kana kwamba yaliyemtokea ni abiria mwenzake, baadae tukaja ng'amua aliyeibiwa ni yeye na si yule aliyemtaja kwenye story.
 
Nikiwa kwenye basi katika harakati za kuitafuta shs, tumesimama kuchimba dawa eneo linaonekana kama kijiji baada ya makambako kuelekea mafinga, ni eneo flani inaonekana kuna vyoo vya mtu binafsi ila abilia hatulipi na sijui nani anayehudumia hivyo vyoo!.

Nikiwa ndani ya chumba natoa oil chafu ya mwilini kwa nyuma nasikia majibizano makali tu kutoka kwa watu wawili, kutokana na majibizano yao nikagundua mmoja ni mganga na mwingine ni mteja.

Jamaa aliyekuwa anafoka alikuwa anadai inakuwaje jogoo akala punje 3 za mahindi kisha kuondoka wakati hakuwa na chakula kwa muda?, Sikusikia jibu kutoka upande wa pili ila baadaye jamaa inaonekana ni mteja akaomgeza "jogoo wangu niliyekuja naye mpaka sasa bado anakula punje za mahindi ila wako amekula 3 na kuondoka, kwa nini?"

Ila kwa sababu tulipewa dakika 5 za kuchimba dawa sikuweza kufuatilia au kujua kilichoendelea katika kujiuliza nimeileta ili wale wadau wa Jogoo na punje za mahindi mje mtujuze ni nini hiki?.

Niliwahi sikia utajiri wa punje za mahindi kuwa jogoo anapokula punje kadhaa basi huo ndiyo uhai wa utajiri wako kulingana na alivyokula but imekuwaje kukawa na jogoo wawili tofauti, yaani wa mteja na wa witchcraft. na huyo wa mganga akala tatu na kusepa ila wa mteja akaendelea kula?
Fafanua kidogo kwamba mkiwa hapo ulipokuwa unatoa oil chafu kwa nyuma, ukawasikia wakiongea. Alafu kuna jogoo mpaka muda alikuwa anaendelea kula punje za mahindi. Elfu Lela ulela.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom