Wanaotafuta Utajiri wa Punje za Mahindi na Jogoo, Imekaaje Hii?

Nikiwa kwenye basi katika harakati za kuitafuta shs, tumesimama kuchimba dawa eneo linaonekana kama kijiji baada ya makambako kuelekea mafinga, ni eneo flani inaonekana kuna vyoo vya mtu binafsi ila abilia hatulipi na sijui nani anayehudumia hivyo vyoo!.

Nikiwa ndani ya chumba natoa oil chafu ya mwilini kwa nyuma nasikia majibizano makali tu kutoka kwa watu wawili, kutokana na majibizano yao nikagundua mmoja ni mganga na mwingine ni mteja.

Jamaa aliyekuwa anafoka alikuwa anadai inakuwaje jogoo akala punje 3 za mahindi kisha kuondoka wakati hakuwa na chakula kwa muda?, Sikusikia jibu kutoka upande wa pili ila baadaye jamaa inaonekana ni mteja akaomgeza "jogoo wangu niliyekuja naye mpaka sasa bado anakula punje za mahindi ila wako amekula 3 na kuondoka, kwa nini?"

Ila kwa sababu tulipewa dakika 5 za kuchimba dawa sikuweza kufuatilia au kujua kilichoendelea katika kujiuliza nimeileta ili wale wadau wa Jogoo na punje za mahindi mje mtujuze ni nini hiki?.

Niliwahi sikia utajiri wa punje za mahindi kuwa jogoo anapokula punje kadhaa basi huo ndiyo uhai wa utajiri wako kulingana na alivyokula but imekuwaje kukawa na jogoo wawili tofauti, yaani wa mteja na wa witchcraft. na huyo wa mganga akala tatu na kusepa ila wa mteja akaendelea kula?
huo upo mbeya huko na tunduma. unauza uhai wako kwa shetani na manake unakubaliana naye kwamba hata ukifa utaenda motoni moja kwa moja kwa raha chache za dunia hii. ndio maana kuku akidonoa punje moja, utaishi maisha ya pesa ndefu kwa mwaka mmoja na utapata kifo cha kushtukiza tu hata nafasi ya kutubu hutapata, watasikia tu umedondoka umekufa. wale wa Mbeya wanajua kilichompata yule jamaa wa kahotel golden city hotel pale sae. sitaki kuongeza neno.
 
Mzee ambae alikuwa anatoa huo utajiri alishakufa, alikuwa akiishi sehemu moja inaitwa isagwa , unaingilia ilula unashika boda ndo unafika, alijenga haswaa, ukifika mwenyewe unakuwa mpole! ila mikoba alibaki nayo mwanae wa kiume! ila nasika hawiki kama baba yake,
 
Sawa mkuu, ila kuna jambo wakati nawasikiliza wakirumbana ni kuhusujogoo wa mganga inaonekana alikula punje 3 ndipo sokomoko lilipokuwepo kuwa jogoo 🐓 aliyekuja na mteja aliendelea kula punje so, inakuwaje hapo?.
huo upo mbeya huko na tunduma. unauza uhai wako kwa shetani na manake unakubaliana naye kwamba hata ukifa utaenda motoni moja kwa moja kwa raha chache za dunia hii. ndio maana kuku akidonoa punje moja, utaishi maisha ya pesa ndefu kwa mwaka mmoja na utapata kifo cha kushtukiza tu hata nafasi ya kutubu hutapata, watasikia tu umedondoka umekufa. wale wa Mbeya wanajua kilichompata yule jamaa wa kahotel golden city hotel pale sae. sitaki kuongeza neno.
 
Maana yake yule jogoo wa mganga ndio Dawa Ni mwakilishi wa mganga ndo utajiri utakaoishi nao huku duniani na yule jogoo wako anakuwakilisha wewe kwenye upande wako wa pili baada ya kupata hzo pesa katika kipindi utakachokuwa unakirudisha kulipa hzo pesa.

Hvyo utapata utajiri duniani kwa muda mfupi Ila utaenda kutumikia kurudisha hzo pesa kwa muda mrefu Sana huko upande wa pili (ndio tafsiri ya jogoo wako kuendelea kula hzo punje bila kuacha).
Mkuu nimekusoma asante sana.

Ila haya mambo ya utajiri wa fasta unawafanya vijana wengi hasa wanaotaka kuonekana kujitoa mhanga na mwisho wa siku wanapotea pasi kutubu.

NImesoma comments nyingi inaonekana wengi wa waliopta huu utajiri ufariki gafla sana pasi nafasi ya kupelekwa hospitali au kwenye matibabu.
 
Sawa mkuu, ila kuna jambo wakati nawasikiliza wakirumbana ni kuhusujogoo wa mganga inaonekana alikula punje 3 ndipo sokomoko lilipokuwepo kuwa jogoo 🐓 aliyekuja na mteja aliendelea kula punje so, inakuwaje hapo?.
punje atakayodonoa ndio idadi ya miaka utakayoishi kabla shetani hajaja kukuchinja na kuondoka na wewe kwa ghafla kabla haujamrudia Mungu wako, na ukifa kifo cha aina hiyo ni moja kwa moja kuzimu.
 
Yeah hii wanategua kwa maelezo ya jamaa mwaka 2016...Yani ikifika karibu na ile tarehe Kuna nyama ya mbuzi inapakwa dawa...halafu muhusika anakaa juu ya mti akiwa na nyama a..chini linachimbwa kaburi..halafu muhusika mdogo mdogo anaangusha nyama shimoni alafu kiumbe kinatokea kwenye ile kaburi na kuanza kula nyama kikiamini Ni muhusika aliechukua utajiri...kikimaliza kinapotelea kaburini...means kimerudi kilipotoka...hivo muhusika anakua ametapeli majini mamaeeeee.....ambao naona hawatapeliki Ni Freemason..au mabingwa wa congo au Malawi maana inavoonekana huku tz Kuna loop waganga walikua wanaacha ndo Mana magwiji wa kigoma kina juma marasta walikua wanategua
Huyo juma marasta ni mganga maarufu sana huko kigoma naskia kawategulia watu mitego mingi sana
 
Back
Top Bottom