John Reese
Member
- Nov 19, 2018
- 29
- 50
Duh hatari sana mkuu ,Habari zenu,
Kama unatafuta kazi kwenye hizi NGO's ziwe za Local au International kuna usanii mkubwa sana kwenye kuajili au kwenye ajira zao.
Yani wanajifanya wanatangaza kazi na kuita watu kwenye usaili kumbe wana Mtu wao mapema yupo na kazi ashaanza wanaita na kukufanyia usaili wakiwa wanakuenjoy tuu.
Mfano mimi.
1. Niliitwa kwenye usaili Morogoro kwenye NGO moja hivi tukiwa wanne tuu wakatufanyia usaili ila kabla ya usaili walitupatia chai kumbe aliyekuwa anatusavia chai ndio mwenye nafasi hiyo akawa anatuenjoy tuu
2. Niliitwa kwenye usaili Mbeya nako tukawa tunafanya usaili na anayetufanyia usaili ndio mwenye nafasi wajinga sana wale jamaa harafu ni shirika la dini
3. Kwenye shirika ninalofanya kazi japo ni international nako tumewafanyia watu usaili jana tarehe 7 wakati watu wameajiliwa toka tarehe 2/1/2019 yani mwendo ni ule ule tuu mie nimeumia kweli
N.B .
Wasaka ajili kwenye haya mashirika eleweni hivyo japo siyo mashirika yote yana upumbavu huo ila mengi ndio mtindo wao.
OMBI LANGU KWA MA HR na Ma-Director General
1. Acheni kusumbuwa watu kama mnavindugu vyenu au wapenzi wenu mnavipachika tuu basi sio manajifanya mnatangaza harafu mnnawapotezea watu mda na nauli zao
2. Acheni unafiki wa kuwafanyisha watu usaili wakati mshaajili na mkiulizwa mshaajili mnajibu bado tuta tuma email kumbe unafiki mtupu
3. Kama mnajuwa mshawaweka jamaa zenu jengeni utaratibu wa kuwarudishia watu nauli,, yani mtu anatoka kigoma anakuja kwenye usaili hewa hapa dar, mngejuwa safari ya dar to kigoma ni noma
ASANTENI
By. Akili Mbili
Sasa tusiokuwa na hizo connection tufanyaje? 🤔🤔