Wanaoshindwa kazi waagizwa kujiuzulu

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
803
Wanaoshindwa kazi waagizwa kujiuzulu

Na Beatrice Charles

VIONGOZI wa umma wametakiwa kujiuzulu nyadhifa zao wanaposhindwa kutekeleza wajibu wao, ili kupisha wenye uwezo kuchukua nafasi hizo na kuliwezesha taifa kufanikisha malengo yake ya kuleta maendeleo katika jamii.

Hayo yalisemwa juzi na Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizindua Mfuko wa Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.

Alisema kuwa viongozi wanatakiwa kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi zaidi na kwa kiwango cha juu majukumu ambayo wanakabidhiwa katika kuwatumikia wananchi wao na taifa kwa ujumla.

Alisema mfuko huu wa uadilifu, uwajibikaji na uwazi utashirikisha jamii nzima, taasisi za serikali, sekta binafsi, maashirika yasiyo ya kiserikali, vyama vya kiraia, vyama vya kitaaluma na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAakukuru).

?Suara la kujenga na kudumisha, uadilifu, uwajibikaji na uwazi katika nchi yetu siyo la serikali peke yake, bali ni jukumu la jamii nzima,? alisisitiza Dk Shein.

Aliongeza kuwa mfuko huo utakuwa chini ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma na uendeshaji wake utafanywa na kamati ya uendeshaji yenye wajumbe kutoka serikalini, sekta binafsi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Kamishina wa Maadili.

Alisema utawala bora na uwajibikaji ni moja ya nguzo kuu tatu za Mkakati wa Taifa wa Kukuza Uchumu na Kuondoa Umaskini (Mkukuta.

Dk Shein alisema mfuko huo umeanzishwa kwa jumla ya dola za Marekani 4.5 nilion (Sh bilioni4.5) ambazo zimetolwa na Benki ya Dunia.

Source: Mwananchi
 
Hivi kweli watajitokeza watu watakaonyosha mikono juu na kusema "najiuzulu, nimeshindwa kazi". Kama wakubwa wanawafahamu wawafukuze!!
 
jamani tumechoka na hii michezo ya kuigiza...si aanze show yake tuu ashindane na Ze Comedy maana nimechoka kweli kweli.
 
Hii inaonesha udhaifu wa anayetoa kaluli hii. Nadhani angetaja ni nani walioshindwa halafu atangaze kuwafukuza na kuwaweka wale anaoamini wanaweza. Hii sentensi yenyewe inaweza kuchukuliwa kuwa inaonesha aliyeitoa ndio ameshindwa kazi.
 
VIONGOZI wa umma wametakiwa kujiuzulu nyadhifa zao wanaposhindwa kutekeleza wajibu wao, ili kupisha wenye uwezo kuchukua nafasi hizo na kuliwezesha taifa kufanikisha malengo yake ya kuleta maendeleo katika jamii.

Hayo yalisemwa juzi na Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizindua Mfuko wa Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.

Kauli ya Kuogopana hiyo, kama anawajua wasiowajibika naye ni Msaidizi Mkuu wa Nchi awawajibishe! sio kutoa kauli tu, Watz hasa Viongozi wetu hawana utamaduni wa kujiuzuli wenyewe mpaka wasukumwe.
 
Hayo aliyaongea bila kutumia karatasi ya hotuba? kama ilikuwa ni hotuba aliongea hayo ktimiza wajibu wake kadri ya lengo la ufunguzi huo, na inaelekea alichokuwa anakiongea practically was not possible kwa mazingira ya nyumbani, ndio maana watu waliokuwepo walikuwa wanataka kuona zecomedy na sikusikiliza hadithi za kila siku za hawa viongozi.
 
Shein nae kwa "kuzindua" tu namvulia kofia! Naambiwa kitendea kazi chake kikubwa ni mkasi wa kukatia utepe!
 
Kati ya watu ambao mchango wao ni zero Tanzania ni SHEIN--so angeanza yeye kujiuzulu kwani hata maneno yake hawezi kuyasimamia.
 
Back
Top Bottom