Msakila KABENDE
JF-Expert Member
- Dec 28, 2017
- 510
- 314
Wanajf, salaam!
Hakuna mashaka kwamba kuna mgogoro unaoendelea kati ya viongozi wastaafu na viongozi walioko madarakani.
Katika mgogoro huu wengi wanazidi ama kumshauri mtawala kukandamizia hapo hapo, Wengine wako nyuma ya viongozi wastaafu na wengine wako katikati.
Kwa haraka CCM tufahamu kuwa:-
(i). Mwezi Oktoba / Novemba 2019 tutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa, hivyo mgogoro uliopo utatuliwe ili tusiathiri matokeo;
(ii). Oktoba 2020 huenda tutakuwa na uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge, na Madiwani. Ushindi ktk kipindi hiki utategemea umoja na mshikamano utakaokuwepo miongoni mwa wanaccm - hivyo kabla ya kipindi hiki hebu tumalize kasoro zetu,
Je, vita hii ina mshindi?
Kwangu mimi naona vita hii ikiwa haina mshindi iwapo kila upande utashikilia msimamo wake (tukumbuke hii ni episode ya pili, ya tatu, nne nk hatujui zitakuwaje).
Kwa vyovyote vile tujitahidi kuunganisha pande hizi ili mwisho wa siku CCM ndiyo iwe mshindi sababu wote ni uzao wa CCM - wananchi tujiepushe na kumjaza Rais upepo lkn tujiepushe na kuwajaza Kinana, Makamba nk upepo badala yake tuwajenge ktk kumaliza mgogoro (huu ndio uungwana na uzalendo)
Uimara wa CCM utategemea mshikamano na umoja wetu. Migogoro siku zote ndiyo kipimo cha ukomavu - tuitatuwe na kuzimaliza.
Msakila M KABENDE
Mwananchi Mwema
19 Julai, 2019