Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,944
- 18,653
Ninashindwa kuwaelewa hawa vijana wa sasa na hata wazee unaokuta wanashabikia kuwa JPM anafanya mambo ambayo wengine walishindwa. Najiuliza huwa wanaakili timamu kweli?
Kwanza kabisa hivi wanapochagua kiongozi, huwa wanategemea afanye nini? Je afanye ya wenzake waliopita au aboresho maendeleo aliyoyakuta?
Leo unakuta jitu zima linashabikia et JPM kanunua ndege lakini wengine hawakuweza. Wanasahau kuwa izo ndege leo zinatua kwenye viwanja ambavyo wenzao walijenga. Ukiwauliza hata faida za izo ndege mpaka sasa hawawezi kukueleza. Nakumbuka awamu ya JK. Watu tulipanda ndege mpaka kwa elf 90. Na zilikuwa ndege za shirika binafsi. Tukategemea labda manunuzi ya ndege za taifa bei ingeshuka hadi hata elfu 50 kutokana na promo zinazopewa. Ila angalia bei zilivyoopanda hivi sasa.
Leo mtu anashabikia kuwa JPM kaweza kufanya elimu bure shule za msingi hadi secondary. Wanaponda marais waliopita kuwa walishindwa hili. Wanasahau ni wakinanani walijenga hizo shule. MKAPA alijenga shule za kata za primary. JK alijenga shule za kata za secondary. JPM hajajenga shule ila anatoa elimu bure katika shule walizojenga waliomtangulia.
Hivyo hivyo katika ujenzi na upanuzi wa barabara. Hivi sasa zinapanuliwa barabara mpaka njia sita. Ila waliomtangulia walizijenga hadi njia 4. Leo tunasahau waliojenga njia nne, tunashabikia anayeongeza njia mbili tu.
Leo tunashabikia madaraja, na maflyover huku tukiponda waliojenga barabara za chini au zinazounga ayo madaraja. Tunasahau bila barabara kusingekuwa na daraja. Au bila barabara ya chini, kusingejengwa barabara ya juu.
Kinachofanya niwe na mashaka zaidi na halimashauri za ubongo zao, ni pale unapojiuliza huyu JPM alikuwa serikalini miaka zaidi 20 iliyopita, na yeye anakuwa miongoni mwa wanaoquestion utawala uliopita.
Ndani ya miaka 4 deni la taifa limeongezeka kwa trilion 20. Kitu tangible unachoweza ongelea ni ununuzi wa ndege, elimu bure, ujenzi wa zahanati, SGR, na maflyover. Hizi pesa zote zinatumika wapi wakati na mapato tunaambiwa wameongezeka sanaaa????
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Watanzania tuacheni haka katabia ka kusahau mapema kiasi hiki. Hakuna mbili bila kuwa na moja.
Haka katabia ka kudhihaki viongozi waliopita na kusifia waliopo sasa sio kazuri kwa masilahi ya Umoja wa Taifa letu.