Wanaosema wanaume hawajatulia kwenye ndoa wanatuonea tu

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari za wakati huu ndugu zangu

Baada ya kupitia nyuzi mbali mbali humu na malalamiko ya baadhi ya wachangiaji kuhusu ugumu wa maisha ya ndoa nimegundua kwamba wanaosema wanaume hawajatulia kwenye ndoa wanatuonea tu

*Umetoka zako kazini umechoka unafika nyumbani unakuta chakula bado maji ya kuoga hakuna kwa nn usitafute kimada sasa.

*Unaacha pesa ya matumizi ya kununua nyama unakuta maharage ukichepuka wanalalamika.

*Umerudi zako kutoka kazini umechoka mwanamke anaanza kuleta gubu kisa kwenye vicoba wanasema kwa nini usipite bar sasa.

*Ndugu zako kutoka kijijini wakija kukutembelea mkeo ananuna kwa nini usitafute mwanamke mwenye kujali ndugu zao sasa.

*Unataka umlipie ada mtoto wa kaka yako na mdogo wako kijijini mkeo ananuna ila anataka uweke nyumba ya mama yake umeme wa REA huko kijijini kwanini usitafute mpango wa kando

*Unampa hela ya kuwanunulia watoto nguo anabania ananunua nguo za hovyo halafu anacheza vicoba si bora uwe single tu

*Unamfungulia biashara ila hela za faida usiziguse muache ateseke tu.


Yote kwa yote Mtaonge mtabishana lakini huo ndio ukweli kwamba vicoba michezo upatu na vitu kama hivyo vinachangia ndoa kuharibika


IMG-20211206-WA0001.jpg
 
^Mchezo wa wakubwa huo, hauhitaji hasira^ :) Wakati unamchumbia na kumwahidi pale Serena, ^kwa uzima ama kwa mauti, kwa tabu na raha, ntakupenda daima,^ sie hatukuwepo. Sasa mashtaka haya yote ya nini!??? Tuache sie tupambane na tozo za Bi Mkubwa.
 
Tabu yote hiyo ya nini??

Kuna jamaa humu aliandika ni vizuri kuoa kwani kuna faida sana. Nikamuuliza ni faida gani unaipata kwenye ndoa hajajibu mpaka sasa.

Kama unajua ndoa ina maswahibu yote hayo kwanini unaoa???
 
Tafuta pesa

Hizo zote ukizoziandika sio changamoto kuuubwa za kukufanya uchepuke/usitulie na mwanamke mmoja.....kwanza kuchepuka ni gharama zaidi
 
Kuwa na mwanamke mmoja ni unafki wa hali ya juu hata kuoa mke mmoja


Ukiwa na wake wawili huwezi pata hizi tabu
 
Back
Top Bottom