Wanaosema ushoga siyo kosa kisheria nchini Tanzania wapo sahihi

lord atkin

Senior Member
Sep 30, 2018
197
683
Wanajamvi salaam!

Mwanzo nilipoona mwanasheria msomi sana Fatma Karume anatetea sana ushoga nilishtuka sana. Nilijaribu kupitia post zake Twitter mbili tatu nione hoja zake nikakutana na moja anadai ushoga au homosexuality siyo kosa nchini Tanzania ila Sodomy ndiyo kosa mimi mwenzenu hapa nilichanganyikiwa kabisa.

Baadaye nilikaa nikatulia nikiwa ni mtu ambaye sijui nishike lipi. Niliamua kukaa chini na kutafakari na kutumia ujuzi wangu mdogo wa sheria na uchanganuzi wa mambo baadaye nimekuja kubaini kuwa ni kweli nchini Tanzania USHOGA (Homosexuality) siyo kosa kisheria bali sheria inakataza sodomy. Zaidi ya hapo nimegundua sheria inayokataza Sodomy pia ni sheria kandamizi.

Sodomy ni nini? Ni kufanya mapenzi kinyume na maumbile, ukisoma kifungu cha 154 cha SOSPA kinakataza mwanaume kumuingilia mwanaume au mwanamke kinyume na maumbile, pia kinakataza mwanaume au mwanamke kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile.

Sasa ushoga ni nini? Ushoga siyo tu kufanya mapenzi kinyume na maumbile. Ushoga ni hali anayokuwa nayo mtu mwilini mwake wazungu wanatumia gender identity au sexual orientation.

Hapa kuna neno linalofaa na hutumika sana kuelezea makundi ya ushoga nalo ni LGBT likiwa na maana ya Lesbians, Gay, Bisexual and Transgender.

Transgender ni wale wote ambao wana jinsia fulani lakini hawana sifa na tabia za jinsia husika na wakati mwingine hii huusisha hadi baadhi ya maumbile
Mfano unakuta mtu ni mwanaume lakini ana tabia na sifa za kike hii wakati mwingine ukimuwahi mtoto inatibika kwa kumuongezea mtoto hormone za jinsia sahihi.

Gay ni mwanaume ambaye anavutiwa kimapenzi na wanaume wenzake.

Lesbians ni wanawake wanaovutiwa kimapenzi na wanawake wenzao.

Na Bisexual ni mtu anayevutiwa kimapenzi na wanaume at the same time na wanawake.

Hitimisho.

Ushoga ni "hali" its all about what you feel inside, kufanya mapenzi against the order of nature kinyume na maumbile siyo lazima uwe shoga ndiyo maana watu wanafirana kwenye ndoa. Wengine wananajisi watoto wadogo kila siku tunasikia lakini wao siyo mashoga.

Kiufupi hakuna kosa la mtu kumtamani kimapenzi mwanaume mwenzake kwenye sheria zetu, wala hakuna kosa la mtu kuwa bisexual, ila kama mtu atamtamani mwanaume mwenzake kimapenzi na kufikia kumuingilia against the order of nature hapo ndipo kosa lilipo. Vipi kwa wale mashoga ambao ni lesbians ambao actually hawafanyi sodomy wanasagana je sheria imewagusa? Haijawagusa hata kidogo. Kusagana siyo carnal knowledge kama ilivyotumika kwenye sheria, yawezekana ikawa ni gross indecent lakini siyo sodomy wala unnatural offense.

Mwisho sheria yetu haijagusia ushoga na wala haijaukataza ana believe me kuna mashoga wengi sana huko mitaani ambao hawajafikia hatua ya kufanya sodomy, yaani unakutana na mwanaume anawatamani wanaume wenzake lakini haendi zaidi ya hapo, wengine wanafikia hata kuwashikashika wanaume wenzao kwa namna ya ajabu na hawafanyi sodomy.
Wengine wanabambiana huko kwenye daladala na mwendokasi na tunaona mpaka mtu anaerect kabisa wote huu ni ushoga na siyo kosa kisheria.

I rest my case!
 
Pole sana!!!!
We have been given a free moral agency..
It depends on how you drive it...
That's the way you have chosen brother

Kuna njia mbili tuu
1-YA KWELI
2-YA UONGO
HAKUNA NJIA YA KATIKATI YAANI KWELIUONGO

kuna Miungu wawili tu
1-MUNGU WA KWELI
2-MUNGU WA UONGO

It's either YOU BELIEVE OR YOU'RE UNBELIEVER

IT DEPENDS ON WHAT WAY YOU'LL CHOOSE
it's your choice brother

But remember EACH WAY YOU'LL CHOOSE HAS IT'S DIFFERENT DESTINATION

have a nice day
 
sisi tunatafuta watu wanaofira hayo maelezo ya kwamba sijui ushoga sijui sodomy hatutaki kuyajua.
Makonda anawatafuta wote wanaopigwa bomba na sio wanaotamaniana.
Mashoga/wasagaji and whatever the hell we are after you.
 
Nakunukuu "ushoga sio kosa kisheria ila sheria inakataza sodomy "hapo ndio penye utata wa bandiko lako kwa upande wangu. Naona ni sawa na kusema wizi sio kosa ila sheria inakataa wizi.
 
sisi tunatafuta watu wanaofira hayo maelezo ya kwamba sijui ushoga sijui sodomy hatutaki kuyajua.
Makonda anawatafuta wote wanaopigwa bomba na sio wanaotamaniana.
Mashoga/wasagaji and whatever the hell we are after you.
Mkuu tulia usome vizuri uzi kuna hoja za msingi anazungumza.
 
Mtaambulia kuwapata wasiokuwa na uwezo kifedha; wenye fedha zao wala hamna hata uwezo wa kufika kwenye mahekalu yao wanapofanyia uchafu huo.
Jambo ninaloona linafaa kufanyika mapema kwenye jamii yetu ni kuanzisha somo la kujitambua kuanzia kindargarten vinginevyo watoto wetu wanaendelea kutifuana kila iitwayo leo.
 
Nakunukuu "ushoga sio kosa kisheria ila sheria inakataza sodomy "hapo ndio penye utata wa bandiko lako kwa upande wangu. Naona ni sawa na kusema wizi sio kosa ila sheria inakataa wizi.
Nadhani ushoga siyo kuingiliwa kinyume na maumbile... hapo ndipo unapochanganya
 
Hawa Jamaa hawawezi pata viza za kuingia USA au ulaya wataishia tandale tu,huko wataishia kupaona kwenye YouTube. Wamewachokoza mashoga.
 
Umeandika mengi lakini ukweli utasimama Daima, kuwa hakuna aliyezaliwa akiwa shoga na hakuna utofauti kati ya kuwa shoga na kufanya vitendo vya kishoga kwa sababu ili mtu aitwe shoga sharti awe anafumuliwa marinda. Wanachokifanya wazungu kwa nchi maskini kushinikiza tukubaliane na ushoga nakifananisha na vitabia vile tulivyokuwa tunawafanyia wasichana wasio na boom na wanamaisha magumu, yaani unamuwekea demu Sekela room kwako akija na akaila tuu ilikuwa lazma naye aliwe.
 
Acheni kuandika mambo meeeengi kutetea upuuzi, Ushoga si jambo la kulishangilia na linatakiwa kukemewa na kila mwenye akili timamu.Period!!!
 
Pole sana!!!!
We have been given a free moral agency..
It depends on how you drive it...
That's the way you have chosen brother

Kuna njia mbili tuu
1-YA KWELI
2-YA UONGO
HAKUNA NJIA YA KATIKATI YAANI KWELIUONGO

kuna Miungu wawili tu
1-MUNGU WA KWELI
2-MUNGU WA UONGO

It's either YOU BELIEVE OR YOU'RE UNBELIEVER

IT DEPENDS ON WHAT WAY YOU'LL CHOOSE
it's your choice brother

But remember EACH WAY YOU'LL CHOOSE HAS IT'S DIFFERENT DESTINATION

have a nice day
Hakuna Mungu #2. Mungu ni mmoja tu. Huyo "wa uongo" ni wako ww na hastahili kuitwa mungu.
 
kujua au kutojua sheria sio sababu ya mtu kuja na upuuzi wake na kutudanganya.
Umemsikia Ninja lakini? Amesema mashoga wako salama na watalindwa ingawa kufanya ushoga ni kosa. Sema naye mpuuzi tukusikie
 
Back
Top Bottom