Wanaosafirisha mihadarati wakamatwa


Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,613
Likes
610,863
Points
280

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,613 610,863 280
Wanaosafirisha mihadarati wakamatwa
Friday, 10 December 2010 20:56

Salim Mohamed,
Tanga

POLISI wilayani Handeni mkoani Tanga imendesha msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watu wawili waliokuwa wakitafutwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji wa biashara haramu ya mihadarati.

Pia watu hao, wanadaiwa kumiliki vilabu vya kuuzia pombe aina ya gongo ambavyo viko karibu na makazi ya watu na hivyo kuwa kero kero kwa wakazi wa eneo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatius Sabas alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 11:15 jioni huko katika Kijiji cha Maraha wilayani Handeni.

Majina ya watu waliokamatwa, yamehifadhiwa na lwamba ni wakazi wa Kijiji cha Maraha Kata ya Kwelimila wilayani Handeni.

Alisema msako huo, iliendeshwa baada ya kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kama vile uporaji wa baiskeli na pikipiki.


Kamanda alisema watu hao, baada ya mahojiano walikiri kumiliki vilabu vya kuuzia pombe haramu aina ya gongo katika maeneo ya makazi ya watu na kusababisha kero kwa watu wanaoishi jirani na vilabu hivyo.
 

Forum statistics

Threads 1,203,903
Members 457,007
Posts 28,134,259