Wanaopita na kushukuru baada ya kushinda uchaguzi, wanatucheleweshea maendeleo

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,234
2,000
Habari wanajamvi!

Tukumbuke ni kitambo sisi tangu uchaguzi ufanyike tarehe 28/10/2020 ila ukistaajabu ya Mussa unaweza kuyaona ya Firauni.

Nasikia kuna viongozi bado wanajizungusha tu mitaani wakidai wanapita kuwashukuru wananchi.Je nani aliyesema wananchi tunataka shukrani ya maneno?

Rais wa nchi alishasema na kuwaambia kwamba kwa ushindi ambao chama cha Mapinduzi umepata kwny uchaguzi wa wabunge na madiwani viongozi waliochaguliwa wana deni kubwa kwa wananchi waliowachagua hivyo wasipoteze muda waende mara moja wakachape kazi ya kuwatumikia wananchi.

Lakini utakuta kuna viongozi bado wanajizungusha zungusha tu hawajaanza kuchapa kazi binafsi inaniuma sana,japo kuna baadhi yao siku walipochaguliwa tu kesho yake wakaanza kazi.

Wito wangu kwa viongozi waliochaguliwa wachape kazi wasingoje kuzima moto miaka mitano michache sana.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
41,866
2,000
Uchaguzi ushapita ukubali ukatae hao ndio wabunge na madiwani wako ,hata Seif na ACT wanatambua hilo .

Ni kweli, lakini hawawezi kupata ushirikiano wetu maana hatuwatambui. Mtaani kwetu kuna mtendaji alipita kwenye ule uchaguzi wa kihuni wa SM, ameitisha mikutano mara 2 sijui kujadili maendeleo, watu waliojitokeza mara zote ni wachache sana, mpaka ilibidi aahirishe hiyo mikutano. Na hata hawa watapata ushirikiano kwa waliowachagua na sio sisi.
 
TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,234
2,000
Ni kweli, lakini hawawezi kupata ushirikiano wetu maana hatuwatambui. Mtaani kwetu kuna mtendaji alipita kwenye ule uchaguzi wa kihuni wa SM, ameitisha mikutano mara 2 sijui kujadili maendeleo, watu waliojitokeza mara zote ni wachache sana, mpaka ilibidi aahirishe hiyo mikutano. Na hata hawa watapata ushirikiano kwa waliowachagua na sio sisi.
Usipotoa ushirikiano yeye atapata ushirikiano kwa mke wake.Ss unamkomoa nani mtaa wako ndio utachelewa maendeleo.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom