Wanaopenda Ufisadi Wanye Maslahi Binafsi Hawampendi Raisi wanatumia Vyombo vya Habari kama Silaha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaopenda Ufisadi Wanye Maslahi Binafsi Hawampendi Raisi wanatumia Vyombo vya Habari kama Silaha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Nov 2, 2011.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Ni vigumu kumuamini mwana siasa yeyote
  Unajua, kwenye siasa unaweza kuwa msafi au mchafu sana tu, lakini kwa vyote pia vinaweza kugeuzwa na kuwa kinyume kabisa na ukaonekana tofauti kabisa, na zana muhimu katika hili ni vyombo vya habari! Kile kiburi cha EL wakati anajiuzulu si bure kuna mengi ambayo hatuyajui. Kwa Jamvi hili tunaweza kuona taarifa ambazo vyombo vya habari vimepotosha kabisa kwa mawili, kwanza vikitaka kuuza habari, pili kwa maslahi yao binafsi ambavyovyote vinashabihiana. Vyombo vya habari sivishambulii kwa makusudi, lakini hata nchi za magharibi zinavitumia vizuri sana kueneza kitu ambacho vijana sikuhizi hamkifahamu sana kinaitwa "propaganda". Sumu inakuwa chakula na chakula kinakuwa sumu.

  Sasa basi, mara nyingi kwakuwa vyombo vya habari ndio dirisha pekee la kuchungulia yanayoendelea kwa viongozi na utawala wao, basi kinachosemwa na kuandikwa huonekana ndivyo kilivyo.

  Katika utawala wowote ule, lazima kuwe na active agent, awe ni yule mkuu au msaidizi wake, hawezi kuwa wa chini sana maana itageuka kuwa conflicting, ukizingatia inahusisha maamuzi. Mh Nyerere aliwika sana kwa kuwa alikuwa maarufu na mwenye uwezo ukilinganisha na wasaidizi wake, Marehemu Sokoine alpoibuka hata Nyerere umaarufu wake ulikaribia kupotea kabisa (ambapo hapa kwa mujibu wa kanuni mojawapo ya leadership utawala unakuwa mgumu kwa hawa wawili na inakuwa haifanyi kazi) mafahali hawa waili wasingeweza kukaa zizi moja hata kidogo, wote walikuwa wanapenda kuwa na final decissions, wako ambitious, hard working na visionary most likely wangegongana tu!, Mwinyi aliwabadili mara kadhaa mpaka alipo,mpata ambaye ni loyal na obidient maana nayo ina matter, na hatimaye Ben hakufanya kosa, alimweka mtu ambaye asingeweza kuinfluence mambo bila yeye kuwa na mkono, kitu ambacho kiliimarisha mwonekano wa uwezo wake bila kuwa na mshindani wa ndani, zingatia kuwa pia Ben anapenda kuwa na maamuzi ya mwisho na huwa anapenda yaonekane mara moja (ktu ambacho vijana wengi wanakitamani ingawa hawakipendi kinapowakuta maana huchanganya na independence yao).

  Sasa, kwa swala la hawa wawili, wote ni watu wanapenda umaarufu, mmoja ni active na mwengine ni passive, mmoja ni mtaalamu na mwingine ni mwanasiasa tu, na mmoja ni mtu asiyefanya maamuzi kwa haraka na huchukua muda kufanya maamuzi mpaka ashawishike vya kutosha na wakati mwingine huruhusu liwalo na liwe lakini asiwe yeye aliyeamua (Pragmatic) na mwingine ni mtu wa kufanya maamuzi haraka mwenye kuona opportunitioes na kujua linkage ya mambo kwa haraka na mwenye kufanya maamuzi haraka bila kuhpfia risk inayokuja ilimradi awe ameona results na benefits mbeleni. Mf. Yeye kumuondoa mzembe kazini halikuwa jambo linalohitaji siasa kuamua, kuvunja mkataba hata wa nchi haikumsumbua, na ni mtu ambaye akijua hadhi yake iko hatarini yuko tayari kufanya lolote lile ili mradi kurekebisha mambo (nadhani anaweza hata kujinyima)! Hii ndiyo tofauti ambayo wamekuwa wakipambana, sio kwamba walikuwa hawajui tofauti zao, na matokeo ndiyo hayo tuliyoyaona.

  Kwa sasa ninachokiona ni hivi, ni vigumu kukubaliana au kukataa hoja hii, hakuna ukweli katika mengi tunayoyasikia, na matokeo yake ndiyo tunachagua viongozi tusiojua undani wao kwa sababu tu ya dirisha hili la vyombo vya habari. Viongozi wengi tuliowachagua wamepata nafasi zao kwasababu ya uwezo wao wa kutumia dirisha hili na kutuonyesha wao ni wachapa kazi kwelikweli. Bahati mbaya sana Mh. Kwa sasa anapata shida mojawapo ya hizi, aidha hana washauri wazuri wa kuweka mambo yake sawa kwenye dirisha hili, au ni mgumu kushaurika kutokana na tabia yake ya kuwa pragmatic ambayo wengi wa wasaidizi wake hawaielewi. Hii imepelekea kwa Mh Raisi kuonekana "Legelege" kitu ambacho nina uhakika wanaokisababisha ni watu wake wa karibu kabisa wa ndani ambao sio waaminifu. Wenye kuvujisha siri na wasioweza kutumia vyombo vya habari katika kuweka mambo sawa ya kiutawala.

  Siamini kama Raisi ni mdhaifu kiasi hiki, hapana siamini kabisa, ila naamini walioko karibu nae ni wazembe hakuna mfano, wenye ubinafsi na wasio na maslahi na nchi hii ambao kwakiasi kikubwa ndio wanaoupotosha ukweli na hawamsaidiii raisi ipasavyo kuweka mambo sawa. Haya tutayajua baada ya utawala wa raisi huyu, na iwapo tu atakayekuja atakuwa mkweli. Ninashawishika kusema raisi huyu amekumbwa na mahasimu wengi sana kutokana na maamuzi aliyoyafanya mwanzoni ambayo yaliwathiri hadi watu wake wa karibu ambao walikuwa wachafu, ni muhimu kulikumbuka hili. Kama kuna kinachomsumbua sassa, ni vita ambayo ni kubwa kiasi cha kuona ni vema kupuuzia baadhi ya mambo ili kutokutoa faida kwa maadui ambao, nadhani hakutarajia kuwaona wakiwa wengi hivi, na karibu hivi, maana hata wengine inabidi aishi nao tu atafanyeje.
   
 2. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 1,522
  Trophy Points: 280
  .....umenitumia tu hapa!
   
 3. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Bonge Bonge.. Najitahidi ndugu kutoa mtizamo unaowiana, hasa pale ambapo wengi wanapafungia macho... pamoja na udhaifu wa Mh Raisi, ambapo kila mtu anaweza kuwa nao hata waliopita tunaweza kuchambua udhaifu wao mwngi tu, ila System imeporomoka na maadili yamekwenda kombo kabisa, nchi za wenzetu hata risi hawezi kubadili sera za nchi hana mamlaka hayo... na hata akiwa mdhaifu, mfumo huimarisha na kujaza nafasi zenye mwanya kwa maslahi ya Taifa. Hapa tunapita kipindi cha mpito kuelekea mabadiliko.... hatari ninayoiona ni mapambano ambayo hayana proper management, maadui wamevamia kila kona ndani ya vyama na ndani ya serikali. Hii kwa sassa akama tungekuwa na vipimo halisi basi umaarufu wa Rasisi ungeweza kuwa umeshuka vibaya sana... kitu ambacho kingefanyiwa kazi na mfumo wa usalama ulioimarika
   
Loading...