khaliciouz
JF-Expert Member
- Nov 12, 2013
- 579
- 210
Hivi website ya tiss ni ipi ?
Hivi website ya tiss ni ipi ?
Mimi siijuiHivi website ya tiss ni ipi ?
Hawana website. Ni taasis ya siri.. kila kitu chao ni siriHivi website ya tiss ni ipi ?
Umri kuanzia miaka 18 hadi 35Kwa wale graduates na wenye diploma. Usaili hapa unakuwaje
Kumbeeee mm nilikuwa sijui hayoKumbe TAKUKURU na TISS wanafanya mafunzo pamoja!!!
waaalimu wa hao wanawafundisha waleKumbe TAKUKURU na TISS wanafanya mafunzo pamoja!!!
Wanafundishiwa wapiwaaalimu wa hao wanawafundisha wale
Welcome to the CIA Web Site — Central Intelligence AgencyHawana website. Ni taasis ya siri.. kila kitu chao ni siri
amesema tiss sio cia mkuu ..sasa iyo link veepeeeee
Kwa Akili yako CIA mambo yao siyo ya Siri Ukilinganisha Na TISSamesema tiss sio cia mkuu ..sasa iyo link veepeeeee
Kikomo cha kujiunga na jwtz kupitia jkt ni umri gani mkuu?Ok Mkuu udagadagaa nafasi ni mwezi wa 12 na january hii ni confirmed kwa sasa jeshi halina hela za kuajiri so subiria uende jkt then TPDF. ahsante.
Kwa watu kama madaktar,wafamasia na manes wenye shahada (degree)utaratb wao hua unakuaje mkuu?Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa
Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa chimbuko la kuandaa vijana kuajiriwa na vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini kama JWTZ, Polisi, Magereza, Usalama wa Taifa na taasisi binafsi za ulinzi. Hivyo Jeshi la Kujenga Taifa linachukua vijana wa kujitolea na mujibu wa sheria.
Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi.
Masharti ya kijana wa kujitolea kwa ajili ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa
1.Awe raia wa Tanzania
2.Awe na Umri kati ya miaka 18-23
3.Awe amemaliza darasa la saba na kuendelea
4.Asiwe ameoa au kuolewa na asiwe na mtu yeyote anayemtegemea
5.Awe tayari kufuata sheria zote za kijeshi zitazokuwa juu yake wakati akiwa jeshini(kutoroka,wizi,ulevi,uvutaji bangi, madawa ya kulevya na upatikanaji wa mimba n.k) Jeshini ni makosa makubwa na utaweza kushtakiwa na kufutiwa mkataba na JKT
6.Awe tayari kurudi nyumbani baada ya kumaliza mkataba wake na Jeshi la Kujenga Taifa
7.Awe na tabia na mwenendo mzuri
Masharti ya kijana wa mujibu wa sheria kwa ajili ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa
1.Awe raia wa Tanzania
2.Awe na Umri kati ya miaka 18-35
3.Awe amemaliza kidato cha sita na kuendelea
4.Awe tayari kufuata sheria zote za kijeshi zitazokuwa juu yake wakati akiwa jeshini(Uvutaji bang, madawa ya kulevya na upatikanaji wa mimba atashitakiwa na kufutiwa mkataba na JKT
5.Utoro haukubaliki na kosa la utoro mkataba utasogezwa mbele
6.Awe na tabia na mwenendo mzuri
UJUE UTARATIBU WA KUJIUNGA NA JKT
JKT huandikisha vijana wa kujitolea kutoka mikoa yote ya hapa nchini kila mwaka. Utaratibu unaotumika ni kwa JKT kuandika barua kwa wakuu wa Mikoa na kuanisha nafasi ambazo mkoa umetengewa. Baada ya Mkoa kupata barua kutoka kwa Mkuu wa JKT na idadi ya nafasi za vijana waliopangiwa kujiunga. Mkoa hugawa nafasi hizo kulingana na wilaya zake. Pia wilaya zinatakiwa kupeleka katika tarafa, kata na vijiji. Mara nyingi uongozi wa wilaya hubandika tangazo la nafasi hizo katika ubao wao wa matangazo. JKT hutangaza nafasi za kujiunga na jeshi hilo kupitia vyombo vya habari vya Serikali na biafsi kwa nia ya kuharakisha taarifa kuwa. kia wananchi hasa vijana. Usaili wa awali hufanyika chini ya Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya wanakotoka vijana hao, baadaye hufanyika mkoani, ili kupata idadi ya vijana wa mkoa mzima. Zoezi hilo linapokamilika mikoani, JKT hutuma timu za maafisa na askari kutoka Makao Makuu ya JKT kwa ajili ya kuhakiki vijana waliosailiwa katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Vijana hupimwa afya zao na kusafirishwa katika vikosi vya JKT.
Kumbe mkuu ??.....aiseeh sikuwa nafahamu sasa kwanini inakuwa siri hao tiss etKwa Akili yako CIA mambo yao siyo ya Siri Ukilinganisha Na TISS
Hakuna mwenye taarifa humu jamiiforumsSamahani wadau ivi izi nafasi za JKT kwa mwaka huu 2018 zinatoka lini kwa anejua maana nimeuliza nikaambiwa mujibu washatoka na kuna wanao maliza course yao mwezi 11, mwenye tarifa jamani.