Wanaopenda kujua kuhusu Kujiunga na JWTZ na Vikosi Vingine vya Usalama

Vijana wangu acha kupotea sasa nakupa ukweli. Ajira zote zinatoka jkt na uwa zinatoka kwa mfumo huu.
1.polisi
2.migodi
3.magereza
4.usalama wa taifa hila baadhi sana sana wenye elimu kidogo form6 na chuo hapa uwa wanachukua watu wachache
5.tanapa
6.JWTZ hila hapa uwa mnafanya usail na uwa wanachukua wachache kwani wanachukua kwa hawamu mbili 1.wanachukua form 4 kuanzia division 1 mpaka 4 ya 28 pamoja na form six /diploma /na degree

Hawamu ya pili wanachukua form 4 wenye 4 ya 29 mpaka darasa la saba hila wenye fani sana sana madereva, fundi chereani, computer, n.k

7.magration. wale uwa wanatoka polisi kwani uwa wanapiga koxi moja na polisi na mwisho wa kuitimu uwa wanabaki wiki moja kwa ajil ya kumalizia masomo yao


N.B sio wanao anza kufanya usaili ndo wanahanza kuondoka hapana mnaweza kuwa wakwanza kufanya na mkawa wa mwisho kuondoka kutokana na waliopo koxi kucherewa kumaliza.

Hila usaili wowote ukija japo utakuwa huko jkt kama unataka kuwa JWTZ husifanye maana uwezi kufanya usaili mara mbili
ASANTHE WANA MMU
 
Soo kuhusu watu ambao wapoo mtaani wanawambia kuwa watakutafutia kazi tiss,jwtz,takukuru, uhamiaji ambao watu wanataka utoe pesa wakusaidie upate kazii kaa ukijua unatapeliwa...ni hayoo tuu


Asante, vichwa vigumu vitakua ngumu kuelewa ila onyo umetoa.
 
Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa
Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa chimbuko la kuandaa vijana kuajiriwa na vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini kama JWTZ, Polisi, Magereza, Usalama wa Taifa na taasisi binafsi za ulinzi. Hivyo Jeshi la Kujenga Taifa linachukua vijana wa kujitolea na mujibu wa sheria.

Kuwaanda vijana kuwa jamii yenye kutekeleza wajibu na moyo wa kupenda kufanya kazi.
Masharti ya kijana wa kujitolea kwa ajili ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa
1.Awe raia wa Tanzania
2.Awe na Umri kati ya miaka 18-23
3.Awe amemaliza darasa la saba na kuendelea
4.Asiwe ameoa au kuolewa na asiwe na mtu yeyote anayemtegemea
5.Awe tayari kufuata sheria zote za kijeshi zitazokuwa juu yake wakati akiwa jeshini(kutoroka,wizi,ulevi,uvutaji bangi, madawa ya kulevya na upatikanaji wa mimba n.k) Jeshini ni makosa makubwa na utaweza kushtakiwa na kufutiwa mkataba na JKT
6.Awe tayari kurudi nyumbani baada ya kumaliza mkataba wake na Jeshi la Kujenga Taifa
7.Awe na tabia na mwenendo mzuri
Masharti ya kijana wa mujibu wa sheria kwa ajili ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa
1.Awe raia wa Tanzania
2.Awe na Umri kati ya miaka 18-35
3.Awe amemaliza kidato cha sita na kuendelea
4.Awe tayari kufuata sheria zote za kijeshi zitazokuwa juu yake wakati akiwa jeshini(Uvutaji bang, madawa ya kulevya na upatikanaji wa mimba atashitakiwa na kufutiwa mkataba na JKT
5.Utoro haukubaliki na kosa la utoro mkataba utasogezwa mbele
6.Awe na tabia na mwenendo mzuri

UJUE UTARATIBU WA KUJIUNGA NA JKT
JKT huandikisha vijana wa kujitolea kutoka mikoa yote ya hapa nchini kila mwaka. Utaratibu unaotumika ni kwa JKT kuandika barua kwa wakuu wa Mikoa na kuanisha nafasi ambazo mkoa umetengewa. Baada ya Mkoa kupata barua kutoka kwa Mkuu wa JKT na idadi ya nafasi za vijana waliopangiwa kujiunga. Mkoa hugawa nafasi hizo kulingana na wilaya zake. Pia wilaya zinatakiwa kupeleka katika tarafa, kata na vijiji. Mara nyingi uongozi wa wilaya hubandika tangazo la nafasi hizo katika ubao wao wa matangazo. JKT hutangaza nafasi za kujiunga na jeshi hilo kupitia vyombo vya habari vya Serikali na biafsi kwa nia ya kuharakisha taarifa kuwa. kia wananchi hasa vijana. Usaili wa awali hufanyika chini ya Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya wanakotoka vijana hao, baadaye hufanyika mkoani, ili kupata idadi ya vijana wa mkoa mzima. Zoezi hilo linapokamilika mikoani, JKT hutuma timu za maafisa na askari kutoka Makao Makuu ya JKT kwa ajili ya kuhakiki vijana waliosailiwa katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Vijana hupimwa afya zao na kusafirishwa katika vikosi vya JKT.
 
Kwenye namba 6 kwa masharti ya kwanza hapo sijaelewa! !??
Ina maana wakishamaliza mkataba wanarudi tena hom? ?
Kweli mtaani patakalika na ugumu huu wa maisha angali vijana wanateknik zote za kijeshi. .?
 
mi ninachokiona hapa ni ubishani tu kama ni jkt ndio wanachikua basi hilo tangazo la kazi uko magereza wamelieka la nn ss tuwe na upeo wa kufikilia kidogo it means jeshi la magereza linadanganya raia wema kuwa wanahitaji watu kumbe wanachukua kutoka jkt tuache hizo tetesi tetesi tusubiri kama ni kweli wanachukua jkt inamana walitudanganya kutoa tangazo la ajira kwa public plz tuweni wavumilivu tu
 
mi ninachokiona hapa ni ubishani tu kama ni jkt ndio wanachikua basi hilo tangazo la kazi uko magereza wamelieka la nn ss tuwe na upeo wa kufikilia kidogo it means jeshi la magereza linadanganya raia wema kuwa wanahitaji watu kumbe wanachukua kutoka jkt tuache hizo tetesi tetesi tusubiri kama ni kweli wanachukua jkt inamana walitudanganya kutoa tangazo la ajira kwa public plz tuweni wavumilivu tu

Tayari walishapita kambi za jkt wamechukua vyeti vya watu waliofanya usaili. Professional hawajatuchukua tuliwauliza wakasema watarudi kufanya usaili kwa professional. Mnavyoumia vichwa mtaani hata huku jkt tunaumia hivyohivyo, sema tu huku kazi uhakika maana hakuna kurudi nyumban hata mkataba ukiisha. Ni lazima uajiriwe. Kama wametangaza msiache kutuma maombi huku sio kwamba wote waliopo wanatimiza vigezo wanavyoviweka. ushauri wangu ni kupima damu kwanza ndo utume maombi.
 
Nilionana na washauri wa mgambo hapa kwetu dodoma. nilikuwa nataka nipate maelezo juu ya kujiunga na jeshi la kujenga taifa kwa mujibu wa kujitolea, hususani kwa sisi tuliomaliza elimu ya juu (degree).. wakaniambia tangazo litatoka mwezi wa kumi na moja. tatizo utata unakuja kwenye umri, na bado haijafahamika rasmi umri wanaohitaji kwa bachelor holders uwe ni miaka mingapi. TUJUZANE ZAIDI KWENYE UMRI WANA JF
 
Usijidanganye mkuu,nina rafiki yangu hakuchukuliwa jwtz but akachukuliwa TAKUKURU bila kushikwa mkono na mtu mpaka leo anapiga kazi!
mmh! i dont think if they can stay away frm the so called "kamlete system" for departiment like tiss.
 
Mimi niko wizara ya mambo ya ndani ukweli ni kwamba jwtz wao hawachukui vijana mtaani wanachukua jkt hila police, magereza, Uhamiaji na tiss wao wanachanganya na wa mtaani kiac hila wengi wanatoka jkt cku hizi wanachukua fresh from school kulingana na mahitaji ya professional mbalimbali ndani ya vyombo hivi hila kiukwel nafac nyingi wamepewa jkt so vijana chamkia fursa ya jkt hajira ziko kibao mfano polic jwtz magereza, zima moto, bandari, tiss uhamiaji na migodin wanachukua jkt.
 
kama unataka kuajiriwa kwenye hizi sector soma degree ya law enforcement pale udsm lakini nafasi ni chache ni watu 55 tu. Ukitoka ajira ni uhakika
 
guys me ni moja ya watu waliopiga jakata ni hivi kule ajira zipo za kutosha kama form four ndo huwez rudi nyumbn labda uweke historia chafu,na kwa kesi ya jwtz nowdays ukiisubiria mtaani ni sawa na kwenda kuvua pweza ziwa victoria jitolee miaka yako miwili upate ajira kwa uhakika na urahisi na wakati huo ukiwa umepata mafunzo mengi ya kimaisha ikiwemo course ya entrepreneurship bureeeee kabisa....vyombo vinavyochukua wa2 jakata ni pamoja na jwtz,police,uhamiaji,Usalama wa taifa,fire,migodi,bank of Tanzania(b.o.t),nida,magereza,makampuni binafsi ya ulinzi n.k mwenye swali aulize.....

Via op.sensa 12
 
Daaah,kweli ajira bado ni tatizo nawaombea sana vijana wenzangu mfanikiwe kwenye harakat zenu za kusaka fursa za kupata mkate wa HALALI
 
Back
Top Bottom