Wanaoning'iniza vitambulisho vya kazi nje ya ofisi zao huwa wanamaanisha nini?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,668
40,916
Huwa nashindwa kuwaelewa jamaa ambao huwa wanatoka mazingira ya ofisi zao wakiwa bado wamening'iniza vitambulisho vyao.

Yaani utawakuta mtaani wanatembea navyo hata huko migahawani bado wanavyo tu.

Huwa inakua ni mikwara tu.

Au ni Usongo baada ya kusota mtaani Bila ajira kwa muda mrefu

Ama ni jambo la kawaida tu.
 
Vijana wa SUMA JKT ndio hupelekea watumishi kuvaa vitambulisho a.k.a Barakoa kila saa wawapo kazini, waingiapo au watokapo kazini. Hii huwapekekea athari za kimawazo . Hujikuta wanavaa kila sehemu .
Pia jambo lingine ni ujinga, ushamba na majivuno
 
Hii nimeitoa Insta, nlijua tu itakua na kazi JF. Acha majungu 😂
DC69D436-5437-4AF6-8363-46563BD42A14.png
 
Hakuna ubaya,ukijivunia ofisi unayofanya kazi,itangaze tu maana ndio insyokuweka mjini.

Ninapopata lunch,huwa nakutana na jamaa wa MDH,BBC,VODA,hizo Swaga zao,utacheka mwenyewe,wanatembea "with entitlement "kwamba maisha wao wameyapatia,wengine wote mafala.

Kuna wakati huwa najiuliza,hivi tukinyanganywa hizi ajira, tunabaki na nini?na vijana waliotusua maisha Kama Diamond,Ali kiba,bila kupitia mfumo Kama wetu,soma kuanzia primary mpaka chuo kikuu,pata degree,tafuta ajira,wakituangaria,wanatuonsje?,,nani mbabe hapa?

Wadogo zangu tumieni ajira kutafuta financial freedom.
 
Vijana wa SUMA JKT ndio hupelekea watumishi kuvaa vitambulisho a.k.a Barakoa kila saa wawapo kazini, waingiapo au watokapo kazini. Hii huwapekekea athari za kimawazo . Hujikuta wanavaa kila sehemu .
Pia jambo lingine ni ujinga, ushamba na majivuno

Huwa unawaponda sana hao jamaa! Waache watoto wa watu wapumue.
 
Huwa unawaponda sana hao jamaa! Waache watoto wa watu wapumue.
Nenda TANESCO UBUNGO, nenda MSD HQ. Staff ukisahau I'd nyumbani huruhusiwi kuingia ndani hata ulie vipi . Labda walegeze masharti sasa hivi. Nimesimuliwa na staff wenyewe pili mimi nafanya kazi karibu na ofisi mojawapo kati ya hizo nilizotaja
 
Back
Top Bottom