Elections 2010 Wanaomumwagia sifa maalim seif kwa kuwasaliti wazanzibari wananipa kichefuchefu

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
0
Kama ni kweli Maalim Seif alipata kura 211,000 na Shein kura 161,000 halafu wakakaa mezani pamoja na Seif akiwepo, ili kupanga namna ya kumpunguzia kura Seif na kumuongezea Shein ili kuipa ushidi CCM, na kwa namna hiyo kuendekeza dhana ya mapinduzi daima, nasema kitendo hicho kinapashwa kilaaniwe na wapenda maendeleo wote kwasababu kinarejesha nchi yetu katika enzi za ukoloni, ambapo wananchi walikuwa hawana kauli yeyote juu ya ni nani anastahili kuwa kiongozi wao. Hivi ikiwa viongozi wa siasa wanaweza wakakaa wakapangiana vyeo bila ya kujali maoni ya wananchi, kuna maana gani kuingia kwenye hizo gharama kubwa kuendesha uchaguzi! Tusidanganyane, Maalim Seif analo deni kubwa la kuwaelezea Wanzanzibari nini hasa kilitokea.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom