Wanaomsifu rais wanamharibu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
KATIKA utawala wa Rais Benjamin Mkapa, kutokana na uandishi wangu wa kukosoa serikali, ilifika mahali vijana wake wakanifikishia ujumbe mzito, kwamba nisipoacha ‘kumlima’ rais, nitakiona, anaandikaAnsbert Ngurumo.

Kwa hiyo, sishangai ubabewa Rais John Magufuli na vitisho vya serikali yake dhidi ya vyombo vya habari na wachambuzi wanaokosoa mwenendo wa utawala wake.

Haya ni marudio au mwendelezo wa mfumo na hulka ileile ya utawala mkongwe wa CCM, chini ya marais tofauti.

Nakumbuka Januari 2001 alipofariki Rais Laurent Kabila, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baadhi ya wafanyakazi wenzangu waliotoka msibani walinifikishia ujumbe mzito kutoka kwa waliojiita ‘vijanawaMkapa.’

Wakati huo nilikuwa nafanya kazi katika gazeti la The African, lakini pia naandika makala kwenye gazeti la Rai, katika kampuni yaHabari Corporation iliyomilikiwa na kusimamiwa na akina Jenerali Ulimwengu, Salva Rweyemamu, Johnson Mbwambo, Gideon Shoo, na Shaban Kanuwa. Katika kipindi kifupi, Ulimwengu alivuliwa uraia.

Nilitumiwa tena ujumbe kuwa, “bosi wako kashughulikiwa; bado wewe… endelea na uchokozi wako.” Sikuwa na tatizo la uraia, lakini kwa kujua ukatili wa vyombo vya dola, nilihisi lolote linaweza kunitokea.

Baadaye nilianzisha safu, nikaiita ‘Maswali Magumu’ kwenye gazeti la Mwananchi, baada ya kushauriana na rafiki yangu Absalom Kibanda, akiwa mhariri wa gazeti hilo.

Huko nyuma, hata kabla ya safu ya Maswali Magumu, Alhamisi moja, mwaka 1998, niliandika uchambuzi juu ya suala la rushwa, ukachapishwa kwenye gazeti la Rai ukiwa na kichwa cha habari: “Rais Mkapa unajivunia nini?”

Uchambuzi huo ulilalamikiwa sana na Rais Mkapa. Alinuna na kugomba. Alikwenda mbali hadi akamtuhumu Ulimwengu, rafiki yake wa siku nyingi, kwamba ndiye aliandika uchambuzi na kuweka jina langu.

Siku hiyo hiyo, Paschal Dismas, mhariri wa habari wa The African, alikuwa amenipanga kuambatana na Kikwete katika ziara ya kisiasa jimboni kwake Chalinze, wakati huo akiwa pia Waziri wa Mambo ya Nje.

Pamoja na waandishi wengine, tulipanda gari moja na waziri, na magazeti tulikuwa nayo, lakini yeye hakuwahi kusoma gazeti la Rai. Jioni yake tuliporejea Dar es Salaam, waziri alikuwa anawahi hafla Ikulu, ambayo Rais Mkapa alikuwa amemwandalia mgeni wake, Rais Bakili Muluzi wa Malawi.

Kesho yake tukiwa ofisini kwa Kikwete kwa ajili ya kuendelea na ziara jimboni kwake, nilianzia kwa Simon Ileta, aliyekuwa ofisa habari wa wizara. Akanitania akisema, “jana mbona mmemgonga sana mzee?” Nikamjibu, “mbona hiyo ni kawaida kwa Rai? Ulitarajia tuandike kwa staili tofauti?” Nilijua alikolenga. Sikufafanua.

Lakini sikuwa nimejua uzito wa alichokuwa anazungumzia.

Baada ya kuanza safari tukiwa ndani ya gari lake, Kikwete akauliza kwa utani, “Kwani Rai mmeandika nini? Rais amekasirika kwelikweli; jana alishindwa kujizuia hata mbele ya wageni.”

Swali la Kikwete lilinifanya nitambue kuwa alikuwa hajasoma kilichoandikwa, na hakujua kuwa aliyeandika kilichomuudhi rais ni mimi. Naye nilimjibu kama nilivyomjibu Ileta, kwamba ni uchambuzi wa gazeti kuhusu utendaji wa serikali.

Sikujua uzito wa maandishi yangu hadi niliporejea ofisini jioni. Wakati huo, ofisi zetu zilikuwa kwenye ghorofa ya tano, Jengo la NSSF, katika makutano ya Barabara za Morogoro na Bibi Titi Mohamed, Jijini Dar es Salaam.

Nikiwa nashuka ngazi, nilikutana na Muhingo Rweyemamu, wakati huo akiwa mhariri wa makala wa gazeti la Mtanzania. Akaniambia kwa utani, “Mkapa anakutafuta. Ile makala uliyoandika imemkera sana, nasikia anasema ataondoka na kichwa chako!”

Nilicheka, lakini nikaunganisha maswali ya watu watatu hawa – Ileta, Kikwete na Muhingo. Nikahisi uchambuzi wangu utakuwa umegusa pabaya. Nikalazimika kuusoma upya.

Niliusoma kwa jicho la msomaji. Kweli, nikagundua kuwa ulikuwa uchambuzi wenye ukweli mchungu kwa watawala. Katika maandishi yangu, nilikuwa nahoji majigambo ya rais kwamba anapambana na rushwa.

Nilimrejesha kwenye historia ya mbio zake za kusaka urais.

Nikamkumbusha kuwa kama si jitihada binafsi za Baba waTaifa, Mwalimu Julius KambarageNyerere, yeye (Mkapa) asingeteuliwa kuwa mgombea, na hata baada ya kuteuliwa, asingepata urais.

Nikamkumbusha kuwa hata kura za kuwapiku washindani wake wakuu – Kikwete na CleopaMsuya – zilitiliwa shaka, kwani wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM, walijua, na walisema kilichofanyika ili Mkapa apitishwe.

Nilienda mbali na kuzungumzia hata kampeni yake nzito na ngumu, na kwamba licha ya nguvu na ushawishi wa Mwalimu Nyerere, taarifa zisizo rasmi zinasema, na wananchi wananong’ona, kuwa kama si mbinu kutumika, si ajabu rais angekuwa Augustino Mremawa NCCR-Mageuzi.

Nikamkumbusha jinsi matokeo ya Jiji la Dar es Salaam yalivyofutwa kihuni, baada ya kugundua kata nyingi zimechukuliwa na wapinzani.

Baada ya hapo nilirejea uamuzi wake wa kuunda tume ya kuchunguza mianya ya rushwa, chini ya Joseph Warioba; na mapendekezo ya tume hiyo ambayo rais alikataa kutekeleza.

Na kila alipohojiwa kuhusu suala hilo alisema, “sikuwatuma kuchunguza rushwa au wala rushwa, bali mianya ya rushwa.”

Nilisisitiza kwamba ingawa aliingia kwenye kinyang’anyiro akiitwa “Mr. Clean,” ndani ya miaka mitatu, alikuwa ameanza kupoteza sifa ya usafi uliomfanya Mwalimu Nyerere amnadi na ampendelee dhidi ya akina Kikwete.

Nilisema pia kwamba kwa vigezo vyote hivyo, Mkapa alipata urais wa kupewa. Hivyo, hakuwa madarakani kwa ridhaa ya wananchi, bali kwa ridhaa ya waliolazimisha awe rais kwa njia zozote zile.

Nikahitimisha hoja yangu kuwa rais anayeingia madarakani kwa “wizi wa kura” hawezi kuaminika kwa wananchi anapokuwa anazungumzia kupambana na rushwa, kwa kuwa naye ni zao la rushwa, hata kama si yeye aliyeziiba.

Nilionesha kuwa Rais Mkapa hakuwa na uwezo na nia ya dhati ya kupambana na rushwa. Nikahoji kwamba akishindwa hilo, huku akitambua kuwa hiyo ni moja ya mambo muhimu ya liyomfanya Mwalimu Nyerere ampiganie, atajivunia nini?

Baada ya kupitia uchambuzi huo, name niliridhika kwamba nilikuwa nimeandika “kitu kikali.” Nilielewa sababu ya rais kukasirika – kibinadamu. Lakini si kudhani kwamba zingekuwa hasira za kudumu, na zenye kuumiza watu kwa sababu ya uwezo wao wa kutia shaka, kufikiri, na kuhoji.

Katika mfumo wa kidemokrasia, kiongozi anayechukia wananchi wanaomkosoa anakuwa hajui kazi yake na wajibu wa wapigakura wake.
 
Wakati ule tulijua ulikuwa mpambe wa kikwete na kusomeshwa ulaya
 
Mwanahabari huru unajipya kwa sasa umezidi kutetea mafsadi na ndo marafiki wako wamebanwa na JPM wamekutuma umshambulie to late to catch a moving aeroplane
 
Kichwa cha habari na habari yenyewe haviwiani. Naona mwandishi anatupa CV yake kuliko kutupa habari za kusifiwa kwa JPM na jinsi anavyoharibiwa. Nimeshangaa kufika mwisho wa post pasipo kusoma namna ya wanavyomwaribu hao wanaomsifia. Mwandishi ni bora abadiri kichwa cha habari hii!!
 
Huyu mwandishi ni zao la mafisadi ndiyo waliyomsomesha
 
Andika hivyo hivyo tena kama ulivyoandika kwa Mkapa, kuhusu MAGUFULI alivyopata URAIS.
Mlikosoa sana utendaji wa KIKWETE nini kilibadilika?
 
Kichwa cha habari na habari yenyewe haviwiani. Naona mwandishi anatupa CV yake kuliko kutupa habari za kusifiwa kwa JPM na jinsi anavyoharibiwa. Nimeshangaa kufika mwisho wa post pasipo kusoma namna ya wanavyomwaribu hao wanaomsifia. Mwandishi ni bora abadiri kichwa cha habari hii!!
Jamaa wakati anaandika atakua alikua kautwika
 
Kichwa cha habari na habari yenyewe haviwiani. Naona mwandishi anatupa CV yake kuliko kutupa habari za kusifiwa kwa JPM na jinsi anavyoharibiwa. Nimeshangaa kufika mwisho wa post pasipo kusoma namna ya wanavyomwaribu hao wanaomsifia. Mwandishi ni bora abadiri kichwa cha habari hii!!
Habari imefichwa,ukisoma kwa kutumia jicho la X uwezi kuielewa hiyo habari. Rudia kusoma ukishindwa muambie mtoto wako akusaidie kusoma.
 
Moyo wa kutojali kukosolewa ni moyo mkuu si wa kawaida. ni sawa na upendo wa Agape. kama umepata kuchunguza kidogo ungegundua kuwa watu ambao wanahisi mwonekano wao si kivile hawakipendi kioo maana kinawaonyesha walivo wakati wao hawataki kuziona hizo kasoro. Hatutumii kioo kuona uzuri bali kasoro ili tuzirekebishe kwa hiyo tukikikataa kasoro hazitatoka na nyingine zitaongezeka!
 
Unataka watu wasifie mafisadi kwa kudhani kuwa kila mtu anavuta kibahasha?
mkuu,katika makala yake hakuna aliposema mafisadi wasifiwe. kikubwa amezungumzia tatizo la rushwa katika jamii ambalo rais mstaafu Mkapa hakuweza kulimaliza na hata rais aliyemfuatia.kutokana na andiko lako inaonyesha jinsi msivyotaka rais akosolewe katika jambo lolote.
 
Back
Top Bottom