Wanaompinga Zitto kuutaka urais ni wahaini wa demokrasia ya ushindani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaompinga Zitto kuutaka urais ni wahaini wa demokrasia ya ushindani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwakajilae, Mar 31, 2012.

 1. m

  mwakajilae Member

  #1
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Binafsi nimefuatilia kwa kirefu juu ya kauli aliyoitoa Comrade Zitto hivi karibuni kwamba anautaka Urais.

  Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,aliitoa kauli hiyo wakati Taifa lipo katika hali mbaya ya Uchumi, Siasa na Jamii isiyo na uhusiano wa Kitabaka.Alitoa kauli hiyo huku akichambua kwa kina jinsi ambavyo baadhi ya matatizo ya kitaifa yanavyolitafuna taifa,huku viongozi wakuu waliopewa dhamana wakikosa ujasiri na Uzalendo wa kimaamuzi wa kuyashughulikia ili yalete tija kwa wananchi wa Tanzania.

  Kwa kifupi aliweza kudokeza vitu vya msingi ambavyo vinamfanya mtu kuwa Rais,kama uwezo,uzalendo na ujasiri wa kufanya maamuzi yatakayowaudhi wengi wanaojinufaisha na hali hii ya Taifa ilivyo.

  Kuna watu ambao wameunga kauli ya Zitto na wengine wamekuja juu wakipinga hata kwa matusi huku wakikosa usitaarabu, hii ni mbaya na tunahitaji kujitafakali upya juu ya fikra hizi.

  Binadamu tumeumbwa huku tukiwa tumezaliwa katika mazingira tofauti yenye Utamaduni,siasa na jamii iliyotofauti na jamii nyingine. Mazingira hayo ndiyo yanayomuumba mwanadamu akiwa mwenye fikra tofauti na mwingine, huku binadamu huyo akiwa amefinyangwa na taasisi za kijamii zinazotofautiana kwa ukubwa sana kimtizamo, taasisi kama Familia, shule, Dini na jamii inayomzunguka, hivi ndivyo vinavyomfanya Juma atofautiane kimawazo na Baraka au Daudi kutokana na tofauti ya kuzaliwa kwao na makuzi yao.

  Hoja ya Zitto kuutaka Urais,hili ni suala linalojikita katika misingi mikuu ya Demokrasia na Katiba ya nchi.Misingi ya Katiba ni juu ya Haki ya Kupigiwa Kura na Haki ya Kupiga Kura.

  Zitto alilifahamu hilo toka mapema, Aliutaka Ubunge toka akiwa Shule ya Msingi, Sekondari na Chuo kikuu, aliwaza kuwatumikia wananchi kupitia Ubunge, akautaka ubunge toka utotoni, alitangaza nia na alitimiza dhamira yake akiwa bado kijana mbichi. Katika historia ya jimbo la kigoma Kaskazini kwa Miaka 50 ya Uhuru amejijengea historia ya pekee kwa wakazi wa jimbo hilo kushuhudia mapinduzi makubwa ya kimaendeleo,ukitaka kubisha,nenda we mwenyewe ukajionee maendeleo ya kigoma Kaskazini,kabla ya Zitto kuongoza kigoma utaijua kigoma kaskazini ilikuwaje na sasa ipoje?huyu ndiye Zitto ninayemjua mimi. Hakuishia tuu kuwa mbunge wa watu wa KIgoma Kaskazini bali alikuwa mbunge wa Watanzani[Seneta] anayebisha afuatiliye Hansard za Bunge ili amfahamu Zitto kwa kazi yake na siyo vinginevyo.

  Sasa Zitto anatangaza adhima ya kuomba kuomba kupigania kinyang'anyiro cha Urais,anao Uzalendo,anao Ujasiri na anao uwezo.

  Watu wanakuja kwa hoja nyepesi kwamba huko ni kuwagawa wanachama!

  Vipi CCM inaposema kwamba kuchagua Upinzani ni kUvuruga amani na umoja wa Kitaifa?kuna ukweli?

  Kwanini kwa CCM iwe ni propaganda za hofu halafu CHADEMA tusema ni kukigawa chama?
  Vyama vya upinzani vimekuja katika wakati ambao Tanzania tulikuwa tumejinyima haki ya kuamua na kujichagulia nuru au mwanga.Tulilazimishwa kuchaguwa giza huku tukiambiwa ile siyo giza bali ni mwanga?hivyo hata wenye akili waliimba nyimbo moja hata kama walikuwa hawakubaliani.

  Vyama vya upinzani vinapaswa kuwa mfano mkubwa wa Demokrasia ya kweli,ambayo tumeihubiri kwa miongo miwili sasa.

  Vyama vya Upinzani tunapaswa kuifundisha CCM siasa ya karne ya 21,Tunapaswa tuwafundishe muundo wa uongozi wa kitaasisi na jinsi masuala yanavyoshughulikiwa kiutaalamu.

  Hilo ndilo lililo kuwa tumaini la mpambazuko wa Vyama Vingi.

  Kijana kama Zitto anapojitokeza kuwania nafasi ambazo utamaduni wa Zamani ulikuwa unawanyima vijana,Inatakiwa tumsifu na kumpa ujasiri na siyo kumkatisha tamaa na dhamira yake kwa Taifa.

  Nyerere alichukuwa nchi hii akiwa na umri wa miaka 39 kama sikosei,Nyerere hakuwa na Uzoefu wa Ubunge wala Uwaziri hata ukuu wa wilaya hakuwa nao. Zaidi ya harakati za mapambazuko ya Ukombozi. Lakini aliongoza Taifa hili kwa ufanisi mkubwa.

  Aliunda baraza la mawaziri,wakuu wa wilaya na mikoa pamoja na makatibu wakuu wa wizara ambao kwa asilimia 75 walikuwa Vijana.Walifanya maamuzi kwa ujasiri na uzalendo mkubwa, waliwajibika kaadiri ya wakati ulivyo waruhusu.

  Tanzania ikang'ara katika Siasa za jamii ya Kimataifa na kitaifa.Watu walitoka dunia nzima wakiwa wanakuja kuitafuta Tanzania na Falsafa ya Taifa la Tanzania.Mshikamano wa kitaifa uliimarika.

  Leo hii wanapojitokeza Vijana wa kada mbalimbali kuwania nyadhifa mbalimbali ikiwemo hata ya Urais,wanatukumbusha historia ya miaka 1960's ya Uhuru iliyopita na miaka 25 ya Nyerere ikajenga historia tunayojivunia. Vijana haw wanakuja kwa wakati muafaka wa kuandika tena historia mpya ya miaka 50 ijayo kwa kuanzia, wakija na Falsafa mpya ya kuongoza na kutatua migogoro ya kitaifa juu ya uchumi na siasa yake.

  Ujio wa katiba mpya unaenda kuamua swali la muda mrefu kwamba vijana wenye miaka 35 na kuendelea ambao Sera ya taifa haiwatambui kama Vijana,tuwaweke katika kundi lipi la kiuongozi,naamini Sera hiyo inawajua na kuwatambua kwamba wana nafasi ya kuwa marais wa nchi.

  Watu wengi walimuogopa sana Kagame alipo chukua nchi mara baada ya mauaji ya kimbari, wakimpuuza kwamba mauaji na vurugu zingetawala uongozi wake.

  Majibu tuliyo yapata ni maendeleo na mshikamano wa Kitaifa wa kupigiwa mfano, uadilifu wa kitaasisi ndicho tunachokiona sasa Rwanda, hiyo ni kazi ya Kagame.

  Kiufupi nina amini katika demokrasia inayoonekana, demokrasia ya Ushindani, demokrasia ya kuomba kupigiwa kura na kupiga kura na siyo vinginevyo.

  CHADEMA Tutasimama kwa kufuata maamuzi ya Kidemokrasia ambayo zao lake ni wanachama walio wajumbe wa Kamati kuu, Baraza kuu na hatimaye Mkutano mkuu na siyo zaidi ya hapo.
  Uhuru wa kufikiri ni Uhuru wa kuamua.

  Mwakajila ni Mwanachama wa CHADEMA na alikua Mkt wa Baraza la Vijana CHADEMA-Mbeya.
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tatizo limejikita kwenye TIMING. Wewe unadhani katangaza ktk muda muafaka?
   
 3. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwani hili jambo haliwezi kuisha mpaka watu watoane macho?

  Zitto alitumia "Demokrasia" kwa mujibu wa wale wanaomuunga mkono na alionekana "mhahini" kwa wale wanaompinga. Tatizo hili kwenye siasa za Tanzania linatokana na watu wa vyama vingine kuurithi mfumo mbaya wa CCM ambao ndani ya chama kuna "sisi" na "wao" hatimaye kujenga ile tabia ya "huyu ni Mwenzetu". Kuna watu ndani ya CHADEMA akiguswa Dr. Slaa inakuwa kama mtu kafanya Kufuru na wapo pia wa Zitto na Mbowe!!

  Siasa za Tanzania kila siku badala ya kuimarika zinazidi kuwa za Kimaslahi siku hata siku. Watanzania maskini wanatumiwa kama uwanja wa wakubwa kuonyeshana mabavu yao badala ya kushindana jinsi ya kutatua matatizo yanayowakabili wananchi!!
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nami nautaka Urais pia. Kila mtu si anatangaza kuutaka Urais? Kuanzia Lowassa, Zitto, Sitta na labda siku za karibuni tutasikia akina Nape, Makinda, Mwanakijiji, Wassira, AshaDii, Kilango, Sugu, Invisible na wengineo wakitangaza rasmi kuutaka Urais. Si ndio demokrasia ya ushindani unayoiongelea?

  Kama walivyosema wengine waliokwishatangaza kuutaka Urais, ninaamini pia ninao uwezo wa kuwa Rais. Ninaamini kabisa kuwa ninao uzalendo wa kutosha na utashi wa kuleta mabadiliko stahili ndani ya Tanzania. Ninajua jinsi viongozi wa sasa walivyosahau maendeleo ya watu na kujikita katika maendeleo ya vitu. Ninajua pia kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika. In fact, ninajua kila kitu. Sihitaji kuambiwa hayo.

  Pia inawezekana labda Mwalimu Nyerere alikuwa anatuzuga tuu kwamba Ikulu si pa kukimbilia. Lakini siku hizi watu wanapakimbilia. Watu wanapakimbilia kutimiza hata ndoto zao za kuwa Rais wa Tanzania. Si kila mtu ana "dream" yake bana? Hata wakati Christiano Ronaldo akiwa Machester United ambayo ni moja ya timu kubwa duniani alikuwa na ndoto ya kuchezea Real Madrid. Na alifanikiwa kutimiza ndoto yake.

  Kwa hiyo, na mimi nimeamua kutangaza rasmi na tena mapema kabisa kuwa nautaka Urais! Ndio, nautaka Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Na ukinipinga utakuwa ni mhaini wa demokrasia ya ushindani. Wewe vipi? Unautaka Urais? Utatangaza lini nia? Kama huutaki Urais unataka nini? Kuendelea kuwa kama ulivyo?

  Inawezekana huutaki Urais kwa vile hujui kama nchi yetu inahitaji uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa (transformation) badala ya mabadiliko ya juu juu (cosmetic changes). Inawezekana huutaki Urais kwa sababu unajua wazi kuwa mabadiliko makubwa yatahitaji maamuzi magumu yakayowaudhi watu wengi wakiwemo wafadhili wetu.

  Inawezekana pia huutaki Urais kwa sababu hujui rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi yetu yetu na kwamba lazima maamuzi magumu yachukuliwe kuzuia na kutokomeza kabisa ufisadi.

  Mimi najua yote hayo na ndio maana nimeamua kutangaza kuwa nautaka Urais. Tofauti na wengine waliokwishatangaza kuutaka Urais wala sihitaji idhini ya chama chochote kuwa Rais wa nchi hii. Nautaka Urais na nautaka fasta! Ukipinga uamuzi wangu wa kuutaka Urais utakuwa ni mhaini wa demokrasia ya ushindani.
   
 5. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  LIKES,
  Prezdaaaaaaaa Z.Z.Kabwe
   
 6. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,061
  Likes Received: 3,984
  Trophy Points: 280
  Hamna mtu anayempinga Zitto kugombea Urais ila ni kubwabwaja na kulalama kwake tu kunapomuondoa staha na stadi! kuna njia muhafaka za kufuata ili awe Rais! sasa yeye anapotumia majukwaa au vyombo vya habari kuonyesha nia yake tena kwa muda usio muhafaka, anatafuta nini? ku-distort concentration ya Wanachadema katika mambo ya muhimu haswa kipindi hiki kigumu cha uchaguzi? Ustaarabu wa kujijua yeye ni kiongozi wa CHADEMA kitaifa si kitu kikubwa na labda nimuulize anauweka wapi? Au ndoto zake zinakosa simile ya kujua subira huvuta kheri? au anatafuta huruma au vijisababu halafu asepe kutoka ndani ya chama na kukidhoofisha? maaana anavyoonekana ni kama vile mtu aliye na umimi na yuko tayari hata kuondoka chamani kama ndoto zake hazitafanikiwa! Ningekuwa yeye mimi nisingetoka hadharani mapema namna hii haswa ikizingatiwa hata umri wa Urais haumpi nafasi na nisingekuwa mimi wa kulazimisha ubadilishwe ilhali ni conflict of interest!
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  kweli ni mzalendo, alitetea sana madini kabla hajaenda kutembelea migodi, baada ya hapo akawa kama kanywa gundi.

  Anyway, sie wapiga kura tuleteeni mnayempendekeza katika chama chenu, tutajua tumnyoe nani na nani tumsuke.

  Labda aombe sana katiba ibadilishwe fasta na wakubali kupunguza umri wa kugombea uraisi, au anataka kugombea 2025?
   
 8. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  Prezidar Dk Zitto Kabwe, inabidi arudi shule angalau aukwae udockta labda tutamfikiria alafu inadibi haoe ili tujue anavyoongoza familia isije akawa Rais huku mkewe awe anamdunda kama yule aliyevunjwa nguu mwaka mzima anachechemea yule Mzee Kiwira
   
 9. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mnyakyusa wawapi wewe unapost thread za kiumbea umbea hakuna mtu anayempinga Zitto kugombea uras, hata Zitto anajua hilo kwamba hakuna kitu kama hicho. Mambo ya kupingana yako huko kwenu kwenye Magamba mnalisha hata sumu, manataka mlikomalie kwamba liko pia CHADEMA Mshindwe na kulegea kwa jina la mzee wa upako!
   
 10. m

  mwakajilae Member

  #10
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama hujui siasa,hukijui chama siyo lazima uchangie,usitutukane wanyakyusa,baki kuwa shabiki baadala ya kudadisi,kufikiri na kujibu.uliza Mwakajila utamjua kwa hoja zake na siyo ushabiki wako.muulize mzee wa upako unayemsema na wengine wengi hapo mkoani.
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Jamani mwacheni Zitto wa watu apumzike.Kila kukicha wasio na cha kufanya ni kumjadili hapa.
   
 12. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Notification.
  One LIKE received from Chilli.
   
 13. N

  Ndusty JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  masuala ya kukimbilia kwenye media kujitangaza as if tayari chadema washamteua kugombea uraisi ni uzushi mtupu.sawa ana haki ya kugombea uraisi lakini sio kwa staili hii.licha ya kwenda tofauti na taratibu na sheria za chama chake pia ni wakati ambao haukuwa muafaka kufanya vile.Naamini kabisa kwamba Zitto kuna kitu anakitafuta ndo maana kaileta issue ya Uraisi.kwa anaye fuatilia maneno ya zitto recently atakubaliana na mimi kwamba zitto is up to something.anajaribu kutaka kuwapumbaza wananchi ili apate backup.Time will tell..
   
 14. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Zitto is really doing a great job, naona kata alizozungukia amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutwaa viti vya udiwani. Kirumba-Mwanza, Kiwira-Mbeya na Lizaboni-Songea.
   
 15. M

  Micmato New Member

  #15
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  My bro zitto naomba ututake radhi haraka sana cc wanacha wa chadema, na wengi wao tupo kwenye mitandao ya kijamii, style ulio kuja nayo kama ni mtu wa kusoma alama zanyakati najua umepata jibu. Sisi siokua atujui unavyo bimbilika tunajua sana lkn muda bado ujafika bado tuna kazi yaku kijenga chama kwanza mfn wewe umetangaza nia mnyika nae atangaze nia vivyo mdee, mbowe, wenje. Means hata awa pia wanauwezo,uzalendo na sifa bro naomba uwe mpole nyinyi nihazina yetu ya badae. Kwakumalizia tu kumbe yote uliokua ukifanya kumbe unautaka urais bro sijafurahi kabisa naomba ututake radhi bro
   
 16. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #16
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mwakajilae, siasa zipi unazozijua wewe? Siasa za kuanzisha thread za kizushi na fitina ndani ya chama makini? Wanyakyusa ni waelewa sana hawana umangimeza kama wewe gamba pandikizi unayetaka kujipatia umarufu kwa kudandia treni kwa mbele eti ooh "Wanaompinga Zitto kuutaka urais ni wahaini wa demokrasia ya ushindani" Nasisitiza Zitto ni jembe na tegemeo ndani ya CHADEMA, Sana sana thread za magamba munazoziansha dhidi Zitto humu ni kumfitinisha na CHADEMA, kwa mtindo wa kudandia treni kwa mbele. Ninachokijua mimi wakati ukifika Zitto ataruhusiwa kuchukua form ya kuomba kupitishwa na CHADEMA kuwania nafasi ya uraisi, kaa ukijua hata wewe pandikizi la Magamba (Makajila) wakati utakapofika utaruhusiwa kuchukua form ya kuomba kupitishwa na chama makini kwa siasa za TZ CHADEMA. Kitakachogomba kwako Mwakajila je, kura zitakutosha kuwania nafasi hiyo? Narudia tena Mwakajila acha kudanda treni kwa mbele ushindwe na kulegeaaaa!!!!:yell:
   
 17. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #17
  Dec 30, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Chadema kama kinavyojipambanua kama chama cha democrasia na maendeleo ni lazima kipitie katika msuguano wa mawazo ili kijitengeneze na kipate mwelekeo. Lazima kuwe na uhuru wa mawazo kila mtu aongee kwa uwazi bila kutishwa aongee kile anachohisi ni sahihi na chenye faida kwa chama bila kuitwa msaliti au pandikizi. Chadema hakitaweza kuendelea kama hakutakuwa mawazo mgongano ndani ya chama. Mawazo haya lazima yashindanishwe kwa hoja za kimsingi zitakazo kinyanyua chama watu wawe huru kutoa mawazo yao juu ya mwelekeo wa chama.


  Watu wawe huru kuchukua fomu kugombea uenyekiti, ukatibu mkuu na tiketi ya uraisi bila kutishwa kuitwa pandikizi au msaliti. Kila mtu awe na uhuru huo ndio demokrasia yenyewe kila mtu ashindanishwe na mwenzake atakayeshinda kwa hoja ndio apite na awe kiongozi. Chadema lazima kipitie mitafaruku ya kimtizamo ni hatua muhimu. Habari ya zidumu fikra za mwenyekiti na katibu mkuu ziishe.

  Vijana wa Taifa hili mnauwezo wa kubadilisha vyama vyetu na nchi yetu kama mtakuwa tayari kubadilisha mitazamo hii iliyomea kwa viongozi wetu kwa muda mrefu kama kweli tunataka kujenga Taifa la kidemokrasia. Ni ukweli kwamba Demokrasia katika nchi kwa upana wake huanza katika Vyama. Vyama vyetu vinapokuwa vya kidemocrasia na wanachama wake wanapokuwa huru kutoa mitazamo yao bila kutishwa na kuitwa mapandikizi, kunapokuwa na uchaguzi huru kila mtu akiwa na nafasi ya kugombea nafasi yeyote katika chama bila kubughuziwa tutakuwa na nafasi kubwa ya kujenga demokrasia yetu katika Chama.

  Namuomba Zito kabwe aendelee na harakati zake za kukiweka chama sawa ili kiwe cha kidemocrasia zaidi. Hii itasadia vijana wanaokuja kupata nafasi ya kushirika uongozi wa juu katika chama ni lazima uhuru huu upiganiwe. Msikubali kulishwa maneno lazima mfikiri.

  Chama cha demokrasia na maendeleo ni lazima kiwe reformed hii sio tu kwa manufaa ya Chadema bali pia kwa manufaa ya nchi kwakuwa ni lazima tuwe na vyama imara ili tupate serikali iliyobora na ya kidemocrasia.

  Chadema ni lazima kiwe na wanachama wanaofikiria sio wanaofuata mkumbo au mashabiki ili kijibadili na kusonga mbele. Mimi nafikiri Zitto kabwe malengo yake sio kukivunja Chadema bali kuki reform.

  Kwahiyo wanachedema punguzeni hasira na mmsikilize mtazamo wake. Mtakapo msikiliza mpambanue na kumjibu lakini ninachoona kwamba huyu jamaa ni reformer. Pengine anaweza kuleta mwelekeo katika chadema akipewa nafasi.

  Tuna umuhimu mkubwa wa kutengeneza viosonary leaders katika Taifa hili na kuruhusu watu wenye mawazo mapya kuingia katika system ili kuleta mapinduzi.

  Chadema ni lazima ibadili mtazamo wake na uendeshaji wa siasa zake. Ili tusijejenga chuki katika Taifa hili. Mtu kuwa CCM sio adui na wala mtu kuwa Chadema sio adui. Ni lazima tuangalie mazingira upya ya siasa zetu. CCM wanapaswa kujua kwamba nchi hii sio mali yao chama chchote kile kina haki ya kuliongoza Taifa hili kikipewa idhini na wananchi. Kitendo chochote cha kutaka kuzima demokrasia, kutumia nguvu ya polisi kuzima harakati za watu kutumia vyama vyao kuweza kuingia madarakani kutumikia Taifa lao ni uhaini. Kuingiza vibaraka kutaka kuwaharibu harmony and order katika vyama ni uhaini na ni ukiukwaji wa katiba wa uhuru wa vyama kwanini mnataka mbaki peke yenu? Vyama vyote vya nchi hii vina haki kuongoza nchi. CCM kwa kuendelea kufanya hivi mtaharibu nchi.


  Ni lazima tuendeshe siasa zetu katika misingi ya kuheshimiana. Tuweke akilini misingi bora ya vyama vyetu vya siasa ndio vinavyopelekea serikali bora. Ni lazima tuondoe hili suala la kuingia kwenye siasa kwa manufaa binafsi. Kila mtu apewe nafasi ya kuongoza kama ni kipaji chake na ana uwezo ni lazima tujenge mazingira ambayo kila mtu ataweza kushiriki katika uongozi wa kisiasa bila uoga. Bila kuogopa matusi ambayo yatamvunjia heshima yake. Kwahiyo tunahitaji Taifa hili lisonge mbele lakini bila vyama imara itakuwa ndoto. Juhudi zetu ni lazima iwe kujenga vyama hivi katika misingi ya kidemokrasia. Ili kila mtu awe na uwanja mpana wa kushiriki katika uongozi wa nchi yake bila kuogopa.
   
 18. m

  mishalejuu Senior Member

  #18
  Dec 30, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaCHADEMA are full of HATE! tunakimaliza chama wenyewe..... A winning strategy would be to let some one who is likeable, selectable and with high impact factor socially to run for the CHADEMA presidency. short of this, it will be a serious loosing gamble! CCM wataendelea kutawala.

  mtoa mada yuko sahihi kabisa naunga mkono!
   
 19. m

  mishalejuu Senior Member

  #19
  Dec 30, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DU! mkuu haya maneno yako yahifadhiwe katika archive....MODs take action please!
   
 20. M

  Mr Emmy JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2013
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,201
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Kuna kundi dogo la watu ambalo linaonekana kuwa na mawazo mgando na kuwa na mtizamo hasi na Kijana wa ZZK hata kama akichangia jambo la maana kwa taifa letu. Kundi hilo linatamani kusikia tu kuwa Mh Zitto Kabwe kwa ridhaa yake mwenyewe ameamua kujivua nyazifa zake zote ndani ya chadema na pia kujivua uanachama wa chama hicho.

  Hebu tuweni wazalendo Zitto naye ni Binadamu hata kama anahatarisha masilahi ya watu ndani ya chadema msimsakame kama wezi wa EPA na wafujaji wa fedha za maendeleo ya miradi ya afya, maji, elimu na kilimo.

  Zitto kama mpigania rasilimali za taifa tumuunge mkono pale anapostahili na tumkosoe pale anapopotoka kwani naye ni Binadamu kama walivyo viongozi wengine ndani ya chadema na CCM@

  kumsakama zitto kwa kashfa na shutuma zisizozakweli zinaboboma democracia ya kweli ndani ya nchi yetu. Tuungane pamoja kuwalaani wanaotamani kusikia Mh Zitto amejivua uwanachama wa chadema
   
Loading...