Wanaompinga wenje wamfanyia vurugu wakati akabidhi madawati

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
*** KWELI HII NI KWELI? MBONA UMATI wa WATU KWENYEMKUTANO?


TUESDAY, NOVEMBER 27, 2012

WANAOMPINGA WENJE WAMFANYIA VURUGU WAKATI AKABIDHI MADAWATI, MNYIKA ALIPA AHADI ALIYOITOA MKUTANO WA MWEZI WA 4 KUCHANGIA MADAWATI, MBOWE, ZITO KABWE, HALIMA MDEE, ESTER BULAYA, VICK KAMATA WATAJWA LIST YA WANAO DAIWA. JEH! WALITOA AHADI HEWA KUCHANGIA MADAWATI NYAMAGANA?



chadema+2.jpg
Jumla ya shilingi milioni 56 ikiwa ni ahadi na pesa taslimu zilipatikana kwenye changizo la madawati lililofanyika mnamo mwezi wa nne 2012 ambapo pesa cash iliyopatikana ni shilingi milioni 24 ahadi ambayo haijalipwa mpaka sasa ni shilingi milioni 32. Kujua wanaodaiwa na viwango vya madeni yao kwa ahadi za madawati bofya play ...

chadema+3.jpg

chadema+5.jpg
Karibu na robo ya mwisho wakati Mnyika akielekea kuanza kuhutubia joto la timbwili timbwili la vurugu likatokea mara baada ya watu kadhaa waliosadikika kuwa walikuwa wametumwa na maadui wa Wenje ambao wamo ndani ya chama hicho kufanya vurugu kwenye mkutano huo kwa kurusha mawe kwenye kusanyiko hali ambayo ilisababisha baadhi ya waungwana kusambaratika wakihofia usalama wao.

chadema+7.jpg
Mdau akitweta mara baada mvua ya makonde kumwangukia..

chadema+8.jpg
"Hapa ndipo angalau kuna usalama.." mwananchi akiwa na majeraha yake...
chadema+1.jpg
Mbunge wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza Ezekiel Wenje akitoa maelekezo juu ya madawati hayo ambayo yametengenezwa kwa mtindo kuwa kila moja linauwezo wa kuketisha wanafunzi watatu.

Orodha ya shule zitakazo nufaika na mpango huo ni pamoja na Shule ya Lake A na B, Shule ya msingi Nyashana A, B, na C, Shule ya msingi Nyakabungo B, Mabatini A, B na C, Shule ya msingi Nyerere, Shule ya msingi Mandela, Ngwandu A, B, C na D, Nyagulugulu, Nyakato, Mahina, Mtakuja, Pamba, Hongera na nyingine ndani ya wilaya hiyo....

 
Huyu Wenje 2015 harudi.Amejisahau sana wacha wananchi wamwonyeshe kabla hata ya huo mwaka
 
Chama cha wauaji hakika pure freemason kazi ya masonoic ni kama hii ya chadema mimi nimekua mwanza chadema mwanza wanachedema wengi wameasi hasa wakurwa na wamehamia ADC kuna mtaa mmoja mwanza chadema wote wamehamia huko
 
huyo mtu aliyetumwa kuweka wingu alipaswa kuwekewa wingu vivyo hivyo hongera saaana kamanda wenje kwa kufait mwenyewe na kufikisha madawati vyema
 
Sijui kama unajua unacho kiandika!

Chama cha wauaji hakika pure freemason kazi ya masonoic ni kama hii ya chadema mimi nimekua mwanza chadema mwanza wanachedema wengi wameasi hasa wakurwa na wamehamia ADC kuna mtaa mmoja mwanza chadema wote wamehamia huko
 
Wenje atarudi kama kawaida tunampenda sana nyamagana hakuna cha ADC wala magamba msiwadanganye watu sisi tuko mwanza na hali tunaiona Wenje ni kifaa.
 
Chama cha wauaji hakika pure freemason kazi ya masonoic ni kama hii ya chadema mimi nimekua mwanza chadema mwanza wanachedema wengi wameasi hasa wakurwa na wamehamia ADC kuna mtaa mmoja mwanza chadema wote wamehamia huko

Yeaah hichi chama kipo tayari ata kuuwa ili wapate madaraka tu
 
kwasababu alikubali kutumwa basi alijiandaa na side effects zake
 
Pamoja na pumba zote bt ukweli umejitenga kwamba WENJE ameonesha kuwa msaada mkubwa katika shule zetu walalahoi kwa kuleta madawati watoto wa masikini wasome wakiwa wamekaa, safi sana!!! Miaka 50 ya uhuru shule hazina madawati, pata picha tungekuwa na akina wenje 100 ingekuwaje?? nadhan hata walimu isingekuwa tatzo!!!!
Jamani tuwateme hao magamba
 
hamtaki kuona mwenzenu akifanikisha ahadi yake??? Huo ni upinzani wa kijinga ndomana hatiendelei
 
Huyu Wenje 2015 harudi.Amejisahau sana wacha wananchi wamwonyeshe kabla hata ya huo mwaka

Ndugu yangu hata kama huna akili , inakupasa kutambua mema amabyo wauungwana huitendea jamii.Kugawa madawati ni kujisahau?kumbuka mojawapo ya janga katika sekta ya elimu hasa shule ya msingi, ni upungufu wa madawati uliokithiri.sasa kugawa madawati huoni ni jambo jema katika dunia ya watu wastaarbu na wapenda mema?na wananchi wa kweli kwa kufanya hili hawwezi kumwadhibu wenje kugawa madawati, bali atakayefanya hivyo ni mhalifu na nguvu ya umma imemdhibiti.tafadhali kwenye mema tusipende kushabikia uhalifu kama si wazalendo.Inaonekan mdau we si mtanzania, ni wale wakimbizi wasioitakia tanzania mema na amani
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom