nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
*** KWELI HII NI KWELI? MBONA UMATI wa WATU KWENYEMKUTANO?
TUESDAY, NOVEMBER 27, 2012
WANAOMPINGA WENJE WAMFANYIA VURUGU WAKATI AKABIDHI MADAWATI, MNYIKA ALIPA AHADI ALIYOITOA MKUTANO WA MWEZI WA 4 KUCHANGIA MADAWATI, MBOWE, ZITO KABWE, HALIMA MDEE, ESTER BULAYA, VICK KAMATA WATAJWA LIST YA WANAO DAIWA. JEH! WALITOA AHADI HEWA KUCHANGIA MADAWATI NYAMAGANA?
TUESDAY, NOVEMBER 27, 2012
WANAOMPINGA WENJE WAMFANYIA VURUGU WAKATI AKABIDHI MADAWATI, MNYIKA ALIPA AHADI ALIYOITOA MKUTANO WA MWEZI WA 4 KUCHANGIA MADAWATI, MBOWE, ZITO KABWE, HALIMA MDEE, ESTER BULAYA, VICK KAMATA WATAJWA LIST YA WANAO DAIWA. JEH! WALITOA AHADI HEWA KUCHANGIA MADAWATI NYAMAGANA?
|
Jumla ya shilingi milioni 56 ikiwa ni ahadi na pesa taslimu zilipatikana kwenye changizo la madawati lililofanyika mnamo mwezi wa nne 2012 ambapo pesa cash iliyopatikana ni shilingi milioni 24 ahadi ambayo haijalipwa mpaka sasa ni shilingi milioni 32. Kujua wanaodaiwa na viwango vya madeni yao kwa ahadi za madawati bofya play ... |
Karibu na robo ya mwisho wakati Mnyika akielekea kuanza kuhutubia joto la timbwili timbwili la vurugu likatokea mara baada ya watu kadhaa waliosadikika kuwa walikuwa wametumwa na maadui wa Wenje ambao wamo ndani ya chama hicho kufanya vurugu kwenye mkutano huo kwa kurusha mawe kwenye kusanyiko hali ambayo ilisababisha baadhi ya waungwana kusambaratika wakihofia usalama wao. |
Mdau akitweta mara baada mvua ya makonde kumwangukia.. |
"Hapa ndipo angalau kuna usalama.." mwananchi akiwa na majeraha yake... |
Mbunge wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza Ezekiel Wenje akitoa maelekezo juu ya madawati hayo ambayo yametengenezwa kwa mtindo kuwa kila moja linauwezo wa kuketisha wanafunzi watatu. Orodha ya shule zitakazo nufaika na mpango huo ni pamoja na Shule ya Lake A na B, Shule ya msingi Nyashana A, B, na C, Shule ya msingi Nyakabungo B, Mabatini A, B na C, Shule ya msingi Nyerere, Shule ya msingi Mandela, Ngwandu A, B, C na D, Nyagulugulu, Nyakato, Mahina, Mtakuja, Pamba, Hongera na nyingine ndani ya wilaya hiyo.... |