Wanaombeza Rais Magufuli wanaumbuka, tumuombee Rais wetu

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,982
4,457
Magu anajitahidi sana kupambana na hali ya maendeleo ya Tanzania kadiri awezavyo. Lakini wanazi sugu wa upinzani wanabeza na kuona kama nguvu ya soda,hili lilianza tu alipoingia madarakani kwa kukatiza safari zisizo na msingi kwa ajili ya kubana matumizi, kutembelea miradi gafla wengi walidai nguvu ya soda lakini bado mpaka leo nguvu ipo.

Mwendo kasi ulivyoanza wakadai nauli kubwa hawatapanda lakini sasa ni tegemeo kwa kila abiria wa Kimara na Mbezi.

Ununuzi wa ndege vivyo hivyo
Ufufuaji wa shirika la reli vivyo hivyo hasa kujali mikoa ya kaz kwa kipindi hiki lakini bado wanabeza na kusema atashindwa tu.

Kwa sasa kuna barabara nyingi sana na miradi mikubwa bado haijakamilika mpaka namwonea huruma huyu mzee ataweza kweli? Lakini alisema mwenyewe kuwa nchi ina HELA.

Ewe mtz unataka afanye nini utakachokipenda? Au hadi muwekewe pesa mfukoni? Binafsi kwa mambo ambayo amefanya hakuna haja ya kampeni 2020 hii ndio serikali ambayo haina ahadi za mdomoni.

Kila binadamu ana mapungufu yake hakuna mkamilifu hata m1 kama Magu naye anayo hatupaswi kumlaumu sana anapopendelea nyumbani kwake kwa kias na kubagua sehem flan ni kawaida na tumuombee iyo chuki imtoke..

Ashukuriwe kupeleka treni Moshi mana itasaidia sana kwa kanda hiyo. Lakini wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema ni kama kumtupia mfupa mbwa anaekukimbiza ili umpoze na kumnyamazisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu nachukia Kama kumsifu mtu
kwanini tusijisifu wenyewe hadi Usifie mtu mwingine

Huu ni upimbi
 
Kiongozi anapotekeleza maslah ya inchi hapaswi kusifiwa hata kidogo kwasababu ndio kazi anaypaswa kufanya.

Kiongozi akivunja sheria za nchi tunapaswa kuchukua hatua muhimu kuhakikisha kwamba anafuata taratibu za kisheria zilizopo...kinyume chake hakuna sababu ya kuwa na kiongozi.

Period.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi tatizo langu na serikali hii ni kudanganya watu najiuliza kwanini wanakuwa waongo sana hata kwa vitu vya kawaida.
Utaskia nchi ina pesa nyingi tunajenga kwa pesa zetu. Wakati hakuna mradi mkubwa hata mmoka ambao haujengwi kwa mkopo kuanzia SGR na hizo fly overs.
Issue kama manunuzi na undeshaji wa Air Tanzania imehamishiwa office ya raisi ili isikaguliwe na ukweli kujulikana. Hapa lazima kujiuliza kwanini anafanya hivi?
Kuna mambo kibao yanafichwa ndiyo yananipa mashaka kama kweli things are really good as they seem to be.
Mimi ninachokiona hapa serikali inafanya marketing na promotion ya kiti cha raisi ndiyo maana kwa juu juu anaonekana he is thr best.
Hakuna raisi aliyewahi kupromotiwa kama JPM maana kuanzia wenyeviti wa mtaa mpaka mawaziri wanampromote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Jambo moja. Watu wanalalamikia Sana na Mambo wanayofanyiwa na vyombo vya dola husasan traffic na polisi. Lakini hakuna kinachofanyika. Tunaona sehemu zingine ka wizara ya afya yakitokea malalamiko Basi wahusika haraka uingilia Kati. Lakini si kwa jeshi la polisi. Malalamiko Ni mengi Sana tena kila kukicha. Ninachoogoba Mimi Ni kuwa Kama dhulma imetamalaki na wahusika wakawa kimya. Basi Mungu huwa anajibu na kwa kupambana na mkubwa wao
 
Tatizo Lumumba "boom" likitoka mnajionyesha kabisa. Yani mnapost kwa pamoja halafu topic Ile Ile moja mnafanya kubadili heading tu.

Shame on you.
 
Magu afanye yake asepe..aje mwingine..hivohivo....
Hii nchi haiishii hapa..ipo na itakuwepo milele na milele....Magu kufanya mazuri ni sawa kuna mambo anajitajidi..kinachonichekesha na kunishangaza ni kutukuzwa kama Mungu....sasa hivi kila kiongozi akiongea..lazima ataje Magu hata maeneo ambayo ni irrelevant kabisa...na inatengenezwa picha as if huko nyuma hii nchi ilikua haipo au yote yaliyofanywa nyuma ni mabaya..na as if baada ya Magu...Tz pendwa haitaenda....
Magu afanye kwa utashi wake na kipindo chake then apishe ......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona kama kuna mambo makubwa sana hayako sawa. Kila siku tunaambiwa miradi yetu inafanywa kwa kutumia pesa zetu wenyewe kwa kuwa mapato yetu yameongezeka kwa kuwabana mafisadi. Sasa najiuliza:- Takwimu zinaonyesha kwamba kwa miaka yote Nyerere aliyokaa madarakani, akaja Mwinyi, Mkapa, na Kikwete, deni letu lilipanda likafikia trilioni 40 na zaidi kidogo. Sasa, kwa MIAKA MINNE TU ya awamu ya tano, hilo deni limetoka hapo trilioni 40 limefika trilioni 64 yaani ongezeko la trilioni 24 (zaidi ya nusu ya deni lililotengenezwa na marais wanne waliokaa si chini ya miaka kumi madarakani kila mmoja). KWA NINI DENI LIONGEZEKE HIVI KAMA HIYO MIRADI INATUMIA PESA ZETU WENYEWE? Kama tunatumia pesa za mikopo, kuna shida gani kusema ukweli? Je, kama kasi ya kuongezeka deni hili itaendelea hivi hivi kwa miaka mitano mingine iliyobaki, nchi yetu si itafilisika kabisa maana makusanyo yote ya kodi yatatakiwa kutumika kulipa deni peke yake? Ndio maana nasema kuna mahali mambo hayako sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom