Wanaolalamikia Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya tuongee hapa kidogo

Daah I support CCM Ila sio Kwa kutuletea mtu kama mchopanga , Niki wa pili na Basila Mwanukuzi,

Jamani inamaana huko mitaani hakuna watu competent??

No wonder why nchi yetu ni masikini mwaka wa sitini huu,

Maana hatuna viongozi wenye ubunifu wa kutatua changamoto zetu.

Inasikitisha mno.
Mkuu hao watu uliowaaja unawajua vizuri au kwenye TV tu?

Mbona kwa Sabaya na Bashite hamkuchonga kiasi hiki?
 
We utateuliwa lini?bwana mushi au hutaki uteuzi

Ova
Kasome vizuri andiko lake,ikibidi urudie Mara tatu unaweza kuokota apo kitu cha maana,na zaidi kuelewa ni meseji gani alitaka iwafikie vijana.

Akili ni kujifunza.
 
Kuna watu wanalalamika kuhusu Uteuzi wa Ma DC. Hebu tuongea Kidogo hapa.....

Na Thadei Ole Mushi

1. Kuwa Mwigizaji au Msanii Hakukunyimi kuwa na sifa za kuwa Kiongozi. Tena Mwigizaji anaweza kuwa Kiongozi mzuri. Kinachoangalia ni uwezo wake katika kufanya vitu. Nilisema wiki Chache hapa zilizopita ni vigumu Sana kufanya vetting kwa vijana wanaosifia tu kuanzia January hadi December. Watu wanahoji why Nick wa Pili lakini niwaambie Nick ni msomi mzuri Sana na ameshaonyesha kuwa ana kitu Cha Ziada. Niliwahi kuandika kuhusu Chine's Mediocrity kuwa ili uwe Kiongozi angalau lazima uwe una kitu ulishakifanya Nick na Mchopanga kawapita wengi katika Hili tuwaacha tuwapime katika Majukumu.

2. Issue ya Uteuzi wa Rais ni kwamba Rais huangalia yupo comfortable kufanya Kazi na nani. Kumbukeni hawa ni wawakilishi wake..... Ukiachana na masuala ya Vetting Rais hupenda kufanya Kazi na watu anaoona kuwa hawa wanamfaa katika mazingira anayoyataka yeye. Hapa Kuna Utashi binafsi wa Rais.

3. Kuhusu Vijana wa Upinzani kuteuliwa ni jambo Zuri. Ni Kweli kwamba kwa siku za karibuni nimekuwa nikisema kuwa hawa vijana wanaotokea upande wa Pili wanapimika na Mara nyingi wapo Smart sana kuliko huku kwenye Jembe na Nyundo. Kitalu Chao kipo vizuri Sana na hapa ndipo HUWA nasema screening ya Vijana wa CCM Izingatie weledi sio Uchawa. Niliwahi kushauri kuwa CCM ianze kuchukua vijana walio machachari Kutoka vyuoni kama wanavyofanya Chadema badala ya kuwachukia na kuwaacha wakaangukia kwenye mikono ya Upinzani.

4. Kwa wale ambao BADO Wana matumaini ya kuwinda U DED na U DAS waanze kufikiria Kazi nyingine za kufanya. Ipo hivi Para A1 (21) ya Standing Orders ya 2009 kama kanuni za kudumu za Utumishi wa Umma........inasema "District Administrative Secretary" means a public servant in-charge of administration in a district; Ikimaanisha kuwa ni mtumishi wa umma atakayewajibika na shughuli za kiutawala ofisi ya Mkuu wa Wilaya.....Kwa kifupi kabisa huyu ni mtumishi wa umma ambaye upatikanaji wa upo wazi kabisa. Mama SAMIA anaonekana kuwa mfuasi mzuri wa kanuni na Sheria za nchi. Hivyo kama haupo kwenye Utumishi wa Umma hadi sasa maana yake U-DAS na U- DED ushakupita. Anza kutafuta Kazi nyingine ya kufanya kama Polepole anavyosema kwenye video hii

6. Angalau sasa Mwenyekiti na Katibu wa UVCCM wamegraduate toka ngazi Moja kwenda nyingine. Nimekuwa nikisema Sana kuhusu hii kumuiya kutoivisha viongozi watakaograduate kutoka level Moja kwenda nyingine nikifanya Comparison na Chama kikuu Cha Upinzani. Kwa Miaka kadhaa hawa vijana walikuwa baada ya Utumishi wao kwenye kumuiya ya Vijana walikuwa wakipoteza kabisa kwenye Ramani tunao kina Sadifa, Beno Malisa na wengineo hawajulikani wapo wapi huku kina Katambi, Henge na wengineo wakigraduate. Haya ni mafanikio ya UVCCM inaanza angalau kuivisha viongozi wa Kutumika maeneo mengine.

6. Naongea Sana kuhusu Self Actualization kwa vijana. Taifa letu limekumbwa na pepo la kila Mtu kutaka kuitwa Mheshimiwa. Kwa mataifa mengine hasa yaliyoendelea vijana hawana thinking hiyo. Wengi Wana matamanio ya kutimiza Ndoto zao kwenye biashara, Kwenye fani walizosomea nk. Kama vijana wakilielewa Hili wanaweza kulisaidia Taifa vizuri zaidi kuliko kuwaza kuteuliwa. Na hapa ndipo ninapotaka wengi wadondoshe dhana ya UCHAWA wavae uhalisia wao na waonyeshe Wana vitu Gani vya Ziada.

7. Ni makosa makubwa kudhani kigezo Cha kuteuliwa ni Kumtukana Mbowe na Chadema au ni kuimba nyimbo za kampeni Sana, au ni kusifia Tu. Kuna mambo mengine ya msingi ambayo huangaliwa. Ndio maana unaona sura Mpya ambazo hazijawahi kusema hata CCM hoyee mahali.

8. Soon tutaanza kuona Sura halisi za watu, Expectations sasa zimeisha kabisa. Akili zitarudi kwenye fuvu la kichwa. Lilikuwa ni Suala la Muda tu.

Tufundishane Adabu

Ole Mushi
0712702602.
"Kanzu mpya,shehe ni yule yule"
 
Kitu cha muhimu hapa ni kwamba, rais ana mamlaka ya kikatiba na kisheria kuteua na kutengua anayemtaka Ukuu wa Wilaya.

Kama unaona anaoteua hawafai, cha kufanya ni kubadili mfumo ili rais asiteue, Wakuu wa Wilaya wapatikane kwa kupigiwa kura na wananchi, au cheo kifutwe kazi zifanywe na watendaji wengine.

Kimantiki na kisheria, haina maana kumpa rais nguvu za kikatiba na kisheria kuteua anavyotaka, halafu akiteua anavyotaka kumuingilia na kumpangia ateue vipi.
 
Nasari alikuwa CHADEMA,ndiko alikopikwa akaonekana leo anafaa,Mashinji alikuwa Katibu Mkuu Taifa -chadema.
Walikuwa. Upinzani waliuacha walipohamia CCM.
Kwa maoni yangu, hata walipokuwa CHADEMA hawakuwa wapinzani bali walivaa tu koti la upinzani.

Amandla...
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom