Wanaolalamikia tozo ya jengo nahisi hawana uelewa au sio wazalendo

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Mimi mara ya kwanza nilikua mpingaji mkubwa wa tozo ya jengo, nilipinga sana nikwa najiuliza kwanini tulipie kodi ya jengo hata ambao tumepanga.

Lakini baada ya kujifikiria kwa kina nimeona huu ni upuuzi watanzania tumezoea kulalamika hovyo.

Nimebadilika ninaunga mkono.

Just imagine wabongo unakuta jengo moja wapo wapangaji hata watano ila wote kwa pamoja hawataki kulipa buku kwa mwezi, na muda huo huo wanataka serikali iwape huduma bora za jamii.

Watanzania tubadilike sina hakika kama kuna mtanzania aliyepanga nyumba nzima au anayemiliki nyumba eti anakosa buku kwa mwezi, au sio kwamba akitoa buku kwa mwezi itamuathiri uchumi.

Wapangaji wetu wa uswahili ndo kabisaa nyumba moja wapangaji tisa kweli wote kwa pamoja mshindwe kulipa buku kwa mwezi?

Mambo mengine tuache kulalamika ni heri tulalamike endapo tukiona hela hiyo inatumika vibaya serikalini.

Hii nchi itajengwa na wananchi.
 
Tozo ziegemee kwenye kumkamua Mwananchi!!

IMG_20210821_145411.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom