Wanaolalamikia 'SINGO MAZA' wasipuuzwe. WANA HOJA

Wanaolalamikia 'SINGO MAZA' wasipuuzwe. WANA HOJA

My toxic trait; mi ni mrahisi kuchukua maonyo kutoka kwa mwanamke kuliko kwa mwanaume. 😀🥹

Tumekusikia single mom, lakini tunasema hivi… pamoja na matatizo waliyonayo single moms, which kila mtu anayo…. Haina haja ya kuwashambulia muda wote, tayari wana burden ngumu ya kulea watoto pekeyao, kwanini kuwaongezea ugumu?

However, kuendelea kuwashikia bango single mothers huku tukiwaacha wanaume waliowazalisha getting away just like that, hatuwezi kusolve tatizo, na tatizo halitokaa lije kuisha.

Mtoto anapatikana baada ya kitendo cha me na ke kufanya sex, huwezi jua wawili waliongea nini kabla ya kumwagiana ndani.

Let’s grow up and be accountable.
 
Kama certified singo maza wa one kid onze earth na anaza kid inze womb naandika hii huku tuchozi tukinilenga coz hakuna kitu inauma kama kuukubali ukweli unaotamani uwe uwongo.

Pamoja na kuwa sipendi vile singo maza tunapopolewa kama apopolewavyo paka mdokoa mboga ila leo nakubali ya kwamba SISI SINGO MAZA NI TATIZO KATIKA JAMII💔💔☹️☹️.

Hapa JF anti-singo mama wanatuangalia singo mamaz kama tatizo katika MAHUSIANO YA KIMAPENZI ila mimi nasema sisi ni tatizo katika maeneo mengi zaidi ya hilo, nayo kwa uchache ni ;

MAKAZINI:Ukiwa na co-worker single mama kazi unayo na akiwa boss basi ndo mmmhuuu.

MTOA HUDUMA.Ukutane na mtoa huduma singo mama kavurugwa halafu ukosee kidogo mfano kakuelekeza jinsi ya kujaza fomu ukosee au uwe wale kama mimi tunaopenda kuuliza uliza maswali.Siku yako lazima iharibike.

JIRANI:Jirani singo mama,yeye na watoto/mtoto wake ni kero kwa wenzie.Vitoto ni kubutuliwa kila saa huku vikifokewa/tukanwa na kukumbushwa jinsi vilivyo vishenzi/mbwa kama baba zao.

KATIKA MISHE:Singo maza sisi ni bomu bovu.Sisi Sio lazima upress button au uvute kile kinini sijui ndo bomu lilipuke..Sisi ndani yetu tayari kuna vitu vinachemka hivyo ukitugusa kidogo tu ni dakika sifuri unajikuta ukanda wa gaza.Utakula matusi na vichambo visivyoendana na jinai uliyoifanya.

Yaani kwa jinsi vichwa vyetu vilivyo resi sio ajabu kukuta kasingo mama kafupi kembamba kamekwida tai ya mbaba kama mwarabu fighter kanataka kupigana nae asubuhi asubuhi kituoni huku kakisema 'mshenzi tu wewe kama washenzi wengine nipige kama wewe mwanaume kweli mmbwaa wewe'.

KAMA MZAZI:.Hapa tunyamaze dakika moja kama ishara ya "kuwaombea" watoto wote wanaolelea na singo maza.
SERIOUSLY:.Sio wote ila asilimia kubwa ya singo maza ni HATARI KWA WATOTO WAO☹️.
Tuache mzaha ila hii ni kweli na ni tatizo kwenye jamii.(Nitafafanua hili kule chini).

MAHUSIANO:Sina cha kuongeza coz mshabwabwaja sana humu vya kweli na vya uongo.

Kabla sijaendelea naomba niseme WAPO SINGO MAZA WASIO NA SHIDA NA MTU.

Baada ya kusema hivyo naomba niendelee kwa kuomba wote tujiulize ni NI KWA NINI SINGO MAZA WAKO HIVI???WHY wanawake wanaolea watoto peke yao wamevurugwa??

Yawezekana nikakosea ila mimi kama mwanamke na pia kama singo maza naamini singo maza tuko hivi kwa sababu UGUMU WA KULEA WATOTO PEKE YETU UMEHARIBU AFYA YETU YA AKILI.Hatuko sawa kichwani.Zingatia UGUMU WA KULEA PEKE YETU.

Hivyo mnavyotuona tunapigana na mandoo yetu ya samaki kwenye madaladala,tunavyozingua kwenye mahusiano,tulivyo washari,na hivyo tunavyotesa na wengine kufikia kuua watoto wao ni kwa sababu sisi wenzenu hatupo sawa kichwani.Hatujalogwa na wala sisi sio watu wabaya ni kwamba sisi ni vichaa(kichaa sio lazima aokote makopo) ndo mana tunafanya matendo ambayo mtu mwenye utulivu wa kichwa hawezi kuyafanya☹️☹️.

Ndugu mwanaume na ndugu mwanamke ambae unalea watoto wako na baba yao sijui kama kuna lugha naweza kuitumia uelewe vile ni MATESO mwanamke kulea watoto peke yake.Mimi naomba uelewe tu ya kuwa ni very stressful kulea watoto bila baba..Ubongo wa binadamu yeyote ukipitia stress kali kwa muda mrefu unaleta shida.Na ulezi wa peke yako ni severe and endless stress.Lazima madish yatuyumbe.

Singo maza tumebeba UCHUNGU,MAJUTO na VISASI.
Iwe kakimbiwa kwa tabia zake mbaya au mwanaume kaamua tu kumtelekeza mwenzie kwa ushenzi wqke singo maza ni singo maza na stress zao zinafanana.

Singo maza wenye visent wana nafuu ila kuna mishale haichagui singo mama tajiri wala masikini.As long as ni singo maza lazima tu ikuchome moyo na uchungu utakaoleta depresion ukupate na vikiwa chronic dish lazima liyumbe then unakua na tabia za kisingo maza then kina Zabzab wanakuja kukuanzishia uzi wa kukupopoa JF.

Sasa basi mimi naomba/shauri kwa vile ulezi wa pekee unapelekea wanawake kuwa mentally unstable ingefaa singomamalism iwe listed kama ugonjwa na harakati za kuutokomeza zianzishwe ili kupunguza idadi ya wanawake wasio sawa kichwani na kubwa zaidi kuzuia WATOTO KULELEWA NA MZAZI ASIE SAWA KICHWANI kwani ni hatari sana mtoto/watoto kulelewa na mzazi mwenye changamoto ya afya ya akili.

Kama zilivyo kampeni za kutokomeza ukimwi na malaria iinuke mamlaka/taasisi ianzishe kampeni ya kutokomeza singomamalism.

1)Kampeni ijumuishe kuwepo Vituo ambavyo singo mama watakua na sehemu ya kwenda kuongea ya moyoni,kusikilizwa,kueleweka na kupata ushauri nasaha wa kuwaweka sawa kisaikolojia.

2)Iwepo namna ya kuhakikisha kila baba anachangia malezi ya mtoto kwa pesa na uwepo.Kuna wanawake jehanamu wanaiishi hapa duniani.Ni wanalea watoto kwa mateso makubwa sana.Unakuta mama anahangaika peke yake na mtoto mwenye uhitaji maalum bila msaada wowote wa kifedha wala kisaikolojia.

3)IPIGWE MARUFUKU KUNYANYAPAA SINGO MAZA:Mnazidi kututia wazimu mnavyotunyanyapaa as if tumezaa na manyani kumbe ni nyie 😄Imagine unapata 'getoroman' wako vizuri tu mnapendana na anaahid kuzeeka na wewe na wanao then ghafla unamkuta anaperuzi JF zabzab kapandishq uzi wenye heading UKIKUTANA NA SINGO MAZA HIT HARDER RUN FASTEST☹️ ghafla unamuona anaanza kukuangalia kiajabu ajabu.☹️😄

JE NI SAWA MWANAMKE TAJIRI AKAJIVUNIA U SINGO MAZA?
Kila mtu ana haki ya kuishi atakavyo ila binafsi naona u singo maza sio kitu kizuri. Inafaa watoto walelewe na baba na mama yao.Hata siku moja mama hawezi kuwa mama na baba na baba hawezi kuwa baba na mama.Maisha yakimfosi mama awe yeye ndo baba na mama lazima kuna changamoto zitatokea.

Mfano mzuri wa jinsi kulea peke yako inavyofyatua akili Muone Faiza ex wa mabuttucks yenu anayelea watoto peke yake alivyofyatuka halafu muone furaha mke wa mabutucks yenu anayelea watoto wake pamoja na baba yao alivyotulia kichwa.Sasa usishangae yule furaha angelea watoto peke yake si ajabu na yeye angevurugwa zaidi ya Faiza na labda asingevaa diaper tu,angevaa na pedi kifuani na vituko vingi zaidi ya Faiza.

Pamoja na kuwa wengine ni ma singo maza wa kujitakia(mimi mmoja wapo) wapo wenzenu wamejikuta singo maza bila kupenda.

Hata hivyo kuna baadhi yetu singo maza mnastahili hayo matusi tunayotukanwa.

How come singo mama mwenzangu ushakua singo maza wa one pupil unaona stress hazitoshi unapanua tena miguu unaongeza anaza pupil and anaza pupil and anaza pupil and eeh..Hapo huna nyuma wala mbele na kila pupil na baba yake wa hovyo.SHAME ON YOU..

Honestly,siwaelewi wanawake wa hivi! huwa mnawaza nini?Unakuta mama yuko bize na ndoo za samaki au beseni la mbogamboga, vitoto vinajilea vyenyewe,mara vibakwe mara vilawitiwe, vinajikuta vinajua tabia zote chafu.Lishe duni,makazi,duni,elimu duni.Mama kavurugwa kila saa ana hasira utadhani kuna alomtuma asitumie njia za uzazi wa mpango.

Wanaume wetu wapendwa,kaka na baba zetu.Nawaomba,ukijua mwanamke hutaishi nae jitahidi sana asipate mimba yako.Tumia condom.Usikubali damu yako ikalelewe na singo mama.Unajua mtoto akilelewa na mzazi ambae hayuko sawa mentally na yeye anaweza kuwa mtu wa hovyo maisha yake yote?Unataka haya yatokee kwa damu yako?

Ikitokea mwanaume umezaa na mwanamke uliyepanga kumuoa halafu mkashindwana huko mbele basi nawaomba,kwa faida ya mtoto,msapoti huyu mama kiuchumi hata emotinally.

Siku zote naamini wanaume mna akili na hekima kuliko sisi wanawake na ninaamini nyie ndio wakumaliza kadhia ya singomamalism.Sijui mtaimaliza vipi coz sisi ndo ambao mkitudanganya kidogo tunachanua chanuuu na kuibukia leba na kitoto mkononi au wengine tunafosi mimba tukidhani itasaidia tuolewe.

Our darling wise men,mkiamua mnaweza bila kuwezeshwa.

Hebu atokee wise man mmoja huko kwa comment atoe wazo la jinsi mwanaume anaweza kuhakikisha hazai na mwanamke asie na malengo nae hata kama huyo mwanamke anataka kumtegeshea mimba halafu aone vile naenda kui bless wikiend yake kesho kutwa.🍾🍸🍺🥂🍴🏧

NB:Mimi ni Pridah nimesahau password yangu☹️View attachment 3600549
ni sahihi ila tujifunze kuwaheshimu. Tushajua kama wana shida, lets not make it a living hell to live in this world.
 
Unapopigana vita ukajua mtesi wako ana silaha aina gani wewe tayari ni mshindi. Kwa wewe kama umeshajua tatizo lenu na wewe labda upo hivyo tayari hapo wewe mshindi. Nakushauri tu utafute mtu akuoe usiteseke bure maana ni kama akili unazo ila unahitaji na za kuambiwa kidogo ili uchanganye na zako. Ndio labda uliachwa au uliacha wewe kwa sasa haijalishii rafik yangu focus na life na u make sure umepata mtu na sio mtu kukufokonyoa tu bali awe wa kukushauri maisha wakati mnasalimishana vikojole and then utayajenga vizur tu. Au kama upo 32yrs to 34 nitafte nikuoe tuzae wengne maisha yasonge.
 
BTW jf characters zinazoplay xx wakati zina makende msifikiri hatuzitambui... We just minding our own business....you know foolin the fool who thinks is foolin you! ! :peepoWink:
 
You don’t come across feminine to me, and this doesn’t feel right.. Japo mafisi yashaanza kushoboka lols Anyways lets proceed..

Badala ya kuwahukumu single mothers kama chanzo cha matatizo yote, jamii inapaswa kujiuliza kwa nini idadi ya watoto wanaolelewa na mzazi mmoja inaongezeka na nini kifanyike kupunguza hali hiyo. Ulezi wa mtoto ni jukumu la wazazi wote wawili, na mzigo unapobebwa na mmoja pekee mara nyingi athari zake huonekana kwa mzazi(single mama) mtoto na hata jamii kwa ujumla. Ingawa kuwa single mother si ugonjwa, msongo wa mawazo unaoweza kuambatana na jukumu hilo ni jambo halisi linalohitaji kueleweka na kushughulikiwa.

Pia tusisahau kuwa wapo single mothers wengi wanaolea watoto wenye maadili na mafanikio makubwa kuliko baadhi ya familia zenye wazazi wawili, hivyo changamoto za malezi zisichanganywe na uwezo wa mtu kuwa mzazi. Swala la uchumi linamgusa kila mtu, wale wanaotelekezewa watoto na hawajajipata lazima stress ziwapelekeshe, na sio wote wanaendeshwa na hizo presha kupelekea kutusi watoto, ni tabia tu, kuna wanandoa kibao wanalea watoto na bado mtoto anaoga matusi wala mama yake hawajaibiki kivyovyote vile kiuchumi juu ya madogo!

Mwisho, mtoto hahitaji wazazi wakamilifu; anahitaji wazazi wanaowajibika kwa nafasi zao, wawe wanaishi pamoja au la.. kuna wababa sio present fathers but responsible know the difference mama kijacho or wereva!
 
20260531_002546.jpg
 
Back
Top Bottom