Wanaokerwa na matangazo ya bahati nasibu/kamari toka mitandao ya simu tukutane hapa

CRYPT

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
332
702
Vodacom Tanzania mnakera sana na hizi sms za bahati nasibu, unaamka asubuhi tu unapanga ratiba zako za kwenda kutafuta mkate wa kila siku mara ujumbe unaingia kwenye simu, unakimbilia simu ukidhani ni mchongo wa kazi au interview unakutana na sms ya mojaspesho 😡. Mchana hujakaa sawa instamoja wametuma, ukigeuka huku boompesa nao wanakutumia. Hii imekua kero na TCRA wako kimya kama vile hawaskii malalamiko haya.

Mimi nimeamua kila wakinitumia sms hizi napost katika uzi huu kama ishara ya kupaza sauti yangu juu ya kero hii toka mitandao ya simu. Kama na wewe unakerwa ungana nami kupaza sauti yako
 
Jumapili 23/6/2019 saa nane mchana

1136127
 
Hawa Boompesa sijui niwafanyaje yani nimechoka ikiingia sms wala sijisumbui kuifungua na delete moja kwa moja
 
mimi voda nimeshawachoka kila saa shinda afcon tembelea fb page yetu,,,,pumbavu,,
mimi mwenyewe FB sipo,,
 
Mteja wa mtandao wowote wa simu kama Vodacom unayo haki ya kupinga kupokea matangazo fulani. Kama hawajatoa namba ya kutuma ujumbe wa kujitoa basi piga 100 au pitia dawati la huduma kwa wateja.
 
Mteja wa mtandao wowote wa simu kama Vodacom unayo haki ya kupinga kupokea matangazo fulani. Kama hawajatoa namba ya kutuma ujumbe wa kujitoa basi piga 100 au pitia dawati la huduma kwa wateja.

Huduma kwa wateja wanadai hawana uwezo wa kuzuia usipokee sms hizo. Hiki ulichoandika hapo juu umeshawahi kukifanyia kazi au unahisi tu ukipiga huduma kwa wateja wanakutoa kama admin anavokutoa kwenye group?
 
Hongera! Umejishindia laki 5. Kupata zawadi hii tuma tsh1000 kwenda namba ya kampuni 155888
Kumbukumbu namba namba zako 3 za bahati

Vodacom Tanzania mnakera sana na hizi sms za bahati nasibu, unaamka asubuhi tu unapanga ratiba zako za kwenda kutafuta mkate wa kila siku mara ujumbe unaingia kwenye simu, unakimbilia simu ukidhani ni mchongo wa kazi au interview unakutana na sms ya mojaspesho 😡. Mchana hujakaa sawa instamoja wametuma, ukigeuka huku boompesa nao wanakutumia. Hii imekua kero na TCRA wako kimya kama vile hawaskii malalamiko haya.

Mimi nimeamua kila wakinitumia sms hizi napost katika uzi huu kama ishara ya kupaza sauti yangu juu ya kero hii toka mitandao ya simu. Kama na wewe unakerwa ungana nami kupaza sauti yako
Kwangu zinakuja mfululizo hadi nawaza niziblock, ila nakuta siwezi kuziblock kutokana na hamna sender number.
 
Mimi Vodacom wananikera mpaka basi! Kila ukisikia sms imeingia kwenye simu ukiangalia - sms kutoka Vodacom. Yani wakati mwingine mpaka mara 8 kwa siku 1. Agrrrr...nakerwa sana. Nina mpango wa kuitupa line yao sababu hii tu.Hovyo kabisa.....
 
Back
Top Bottom