fullcup
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 806
- 2,182
Serikali kwa miaka mitano mfurulizo haikuajiri na wala haioni umuhimu huo kutokana na matokeo bora mashuleni. Kuna shule zina walimu watatu wakuajiriwa na saba wakujitolea na zinafanya vema matokeo ya mitihani yataifa.
Kutokana na ufaulu huo serikali haioni umuhimu wakuajiri wakati wanafikia malengo na mwaka huu karibia shule zote zimefanya vema.
Wito wangu ni hawa ndugu wanaojitolea waache mara moja ili tatizo halisi lionekane machoni pa wananchi na serikali.
Wakati shule ya watoto zaidi ya mia tano wakihudumiwa na walimu wawili itwaamusha wananchi na serikali na huenda nguvu ikaelekezwa huko. Nje ya hapo tuangalie mengine yakufanya.
Halafu mbinu yao yakusema wanaojitolea ndo watapewa kipaumbele kisiwapofushe na kujikuta mnafanya kazi miaka na miaka bila ajira huku kitaa mnafahamika kama walimu na mnaishia kula mihogo yakuchoma.
Ili kufikia malengo yetu yakuishi kwakunufaika na elimu zetu ni lazima tufanye kazi na kulipwa kulingana na taaluma.
Bora wakaajiriwa hata wachache lakini wanaolipwa kulingana na taaluma. Leo hata shule na sekta binafsi wanaajiri kwamishahara midogo kisa vijitamaa, tuache ili hata waajiri wapne thamani yetu.