Wanaojali, na wakarimu bado wapo kwenye ulimwengu huu uliojaa wenye chuki, na wabinafsi

Sheffer95

Senior Member
Mar 16, 2020
197
460
Leo nimekaa nimetafakari sana jambo na kuona bado tunaweza kurudisha tabia njema, ukarimu na ustaarabu ambao ndio ilikuwa sifa kubwa ya sisi watanzania ikitutofautisha na watu wa nchi nyingine
Kila uchwao changamoto ya ajali za barabarani imekuwa kubwa sana kila leo tunapoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali hizi na bado tutaendelea kuwapoteza kama tusipo amua kwa dhati kabisa
Hii imenikumbusha wakati fulani nilikuwa nasafiri kwa basi ndogo zile coaster kutoa sehemu moja kwenda nyingine na katikati hapo kulikuwa na vituo vya trafic polisi kama sio 4 au 5.
Katika vituo vyote hivi hawa trafiki walikuwa wakisimamisha gari na kuchukua posho au Rushwa kutoka kwa mwenye gari kitu ambacho si sahihi maana wao walikuwa hawakagua hata gari au kuuliza hali za abiria ndani walikuwa wanajali kuhusu wao tu hawaoni hata kama pengine gari haifai kuendelea na safari au la

Ila katika kituo fulani cha trafiki tulisimamishwa na akaja afande fulani wa kike mrembo aliyevalia maridadi akionekana kwa kiasi chake ni mtu anayejali kidogo maana aliiingia kwenye gari akalikagua akuuliza abiria kuhusu safari so far na pia kutupa elimu kuhusu tahadhari na usalama barabarani na namna bora za utoaji taarifa inapotokea changamoto yoyote hakika abiria tulipata faraja sana kwamba bado wapo watu wengi wanaotimiza wajibu wao bila kusimamiwa, wanajali na kiukweli alipigiwa makofi mengi sana
Moyoni mwangu nilijisemea pengine tungekuwa na watu wengi kama hawa na pengine kungekuwa hata na tuzo za kiserikali kwa kila sekta za umma pengine tungekuwa ni moja ya nchi bora sana, lakini ubaya ni kwamba mazuri machache yamefunikwa na maovu mengi hivyo kufanya watu wachache wenye bidii kama hawa wasionekane

Naamini huu ndio utanzania na ustaarabu wake, watanzania tunaweza kurudisha ustaarabu wetu pamoja na uwajibikaji wetu katika idara na nafasi tulizonazo
Ahsante🙏💪
 
Huyo dada ni boss mgao wake unatokea upande mwingine.

Tunaojali tupo wachache sana na kwenye jamii hatuthaminiwi.
Pole na hongera sana endeleeni na moyo huo huo wa ukarimu, changamoto zisibadili moyo wako. Usitende mabaya au kukatisha kufanya mazuri kisa wengine wamekufanyia vibaya
 
Wazuri wote wanakufa mapema ila sisi mamafia ,majambazi ,wakabaji,wezi ,Wala rushwa na wazurumati tuna miaka mingi Sana ya kuishi na kuitesa dunia na wanyonge wote wanaokaa kiboya kiboyaa ....

Hapa duniani ni vita tu ustarabu ni huko kaburini ukiwa pekee yako...

Ubaya ubaya tu
 
Wazuri wote wanakufa mapema ila sisi mamafia ,majambazi ,wakabaji,wezi ,Wala rushwa na wazurumati tuna miaka mingi Sana ya kuishi na kuitesa dunia na wanyonge wote wanaokaa kiboya kiboyaa ....

Hapa duniani ni vita tu ustarabu ni huko kaburini ukiwa pekee yako...

Ubaya ubaya tu
Hebu tujiulize kizazi cha miaka 20 au 50 kitakuwaje hao ndio wajukuu wetu na vitukuu vyetu maana kwa tabia hizi zilizopo za watoto kutojali wazazi, wazazi kutojali watoto, ndugu kupokonya mali zisizo zao, wanasiasa kununua vitu kwa bei isiyo halisi, ubinafsi, unafki na kufurahia matatizo pengine hata vifo na majanga ya wengine.

Hakika tuna safari ndefu na ngumu sana mbeleni
 
Back
Top Bottom