Wanaoitwa Wazee wa Dar es Salaam ambao kila Rais wa Tanzania anatamani kukutana nao ni akina nani?

Wazee wa Dar es Salaam ni wale wenye kizazi cha walionzisha MWENGE WA UHURU.

kwa ufupi Rais yeyote atakaewazalau wazee hawa na atakae uzalau mwenge wa uhuru hawezi kubaki salama.

KILA FALME INA KINGA YAKE, UTARATIBU WAKE NA UTAMADUNI WAKE.

Rudi na ukasome uzi wa historia ya mwenge wa uhuru wanzilishi wake na historia yake. Halafu ndio utajua wazee wa Dar ni kinanani kwenye Tanzania hii.
 
Ninaomba yeyote anayewajua anieleweshe ili mimi na wengine wasioelewa kama mimi tuwafahamu Wazee hawa ambao kila kiongozi anapenda kukutana nao .

Natanguliza shukrani .
Enzi za Nyerere walikuwa ni wazee waliowapokea wapiganiaji wa uhuru na kuwaunga mkono kwenye harakati zao.

Ila kwasasa ni kundi tu la wazee ambalo kama Rais ana lolote la kuzungumza wanatafutwa, anazungumza na taifa kupitia kwao.

Hili linaweza kufanyika kwa kundi lolote.

Unaweza kuita waandishi wa habari, watoto yatima, wafanyabiashara, viongozi wa dini etc na ukazungumza na nchi kupitia kwao.

Wakati wa Magu aliwahi kuongea nao, vile vile na wazee wa Dodoma.

Sasa hivi Samia kwasababu ndio kwanza yupo madarakani ndio maana anakutana na makundi mbalimbali.

Jana akiwa Nairobi alikutana na Diaspora, na akasema akirudi atakutana na wafanyabiashara.

Hivyo binafsi sioni kama ni issue Rais ( hasa mpya ) au mwanasiasa anayetafuta kuungwa mkono kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii.
 
Ni wanachama wa chama cha mapinduzi, hakunaga wazee wa dar ambao ni mchanganyiko wa vyama. utawaona kesho wamevaa kijani, na ili msiwashtukie watakatazwa kuvaa nguo za chama. vinginevyo Rais angekuwa anawaomba kila chama kiwasilishe majina ya wazee watakao udhuri akikao
Ninaomba yeyote anayewajua anieleweshe ili mimi na wengine wasioelewa kama mimi tuwafahamu Wazee hawa ambao kila kiongozi anapenda kukutana nao.

Natanguliza shukrani.
 
Ni wanachama wa chama cha mapinduzi, hakunaga wazee wa dar ambao ni mchanganyiko wa vyama. utawaona kesho wamevaa kijani, na ili msiwashtukie watakatazwa kuvaa nguo za chama. vinginevyo Rais angekuwa anawaomba kila chama kiwasilishe majina ya wazee watakao udhuri akikao
Kuna siku nilimsikia Askofu Kakobe ( enzi hizo ) akisema alishawahi kualikwa lakini alivyoenda akakuta kazi yao ni kusikiliza tu na kupiga makofi.

Baada ya hapo hakushiriki tena. Sasa tunaweza kulaumu lakini kumbe watu wengine hawataki kushiriki wenyewe.
 
Back
Top Bottom