Wanaoishi nje ruksa kushiriki Miss Tanzania

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,825
287,845
Wanaoishi nje ruksa kushiriki Miss Tanzania
Deus Gabone
Daily News; Thursday,February 28, 2008 @05:40

WATANZANIA walioko nje ya nchi wamepewa ruksa ya kushiriki mashindano ya Miss Tanzania. Ruksa hiyo imekuja baada ya Kampuni ya Kimataifa ya burudani (INCE) ya Canada kupewa kibali cha kuandaa mashindano hayo yatakayojulikana kama Miss Tanzania Canada.

Akizungumza na gazeti hili leo Dar es Salaam Mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga alisema kibali hicho kwa kampuni hiyo kimetolewa kukidhi lengo kuu la mashindano hayo la kuitangaza Tanzania nje ya nchi kupitia mashindano hayo.

Aliongeza kuwa, Watanzania hao wakiitumia vizuri nafasi hiyo ni rahisi kuitangaza nchi kimataifa kutokana na Watanzania wengi kuishi nje ya nchi.

Alisema, Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanaruhusiwa kuendesha mashindano yao ya urembo na kisha kutuma wawakilishi kushiriki Miss Tanzania. Lundenga alisema, warembo hao watakaopatikana watakuwa kwenye kanda ya Elimu ya juu.

Hii si mara ya kwanza kwa fainali za Miss Tanzania kushirikisha washiriki kutoka nje, mwaka jana alishiriki Miss Tanzania-London Gladys Kalega ambaye alishika nafasi ya kumi kwenye fainali.

Mashindano ya Miss Tanzania yanatarajiwa kufanyika Julai mwaka huu. Mrembo anayeshikilia taji ni Richa Adhia aliyelitwaa mwaka jana.


 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom