Wanaoishi Masaki Vs Manzese, Mbagala n.k

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,667
Tofauti ya maisha; Eti ni dhahiri kuwa kuna tofauti kubwa ya maisha kulingana na maeneo, eti na watu wanaoishi huwa na tabia kulingana na maeneo yao: mfano Mke anayeishi Masaki akimwagiza mumewe utasikia "Honey ukirudi husisahau kuniletea soseji, pizza au kuku' sawa dear" Je eti na sisi tunao kaa Manzese, Mbagala, Vingunguti, Tandale na kwingineko mabonde kwinama' Mke akiwa anamwagiza mumewe utasikia...?
 
Hivi Masaki washapata maji siku hizi au mwendo wa Simtank bado?
 
Huku kwa mnyamani tunaagizwa dagaa, utumbo wa kuku na vichwa,vikikosekana hata miguu ya kuku inatosha
 
Eeh te te tee; Like kwa Baba V, anin - gift, na Red Giant. JIBU: eti utasikia "Wee mwanamume usisahau kurudi na miguu ya kuku, utumbo na mihogo ya kukaanga tia pilipili nyingi." loh!
 
Wa Kwa Tandale kwa mtogole, "Nletee udongo na Perege

Nyie jamaa bana nyie.
Wale wa Kimara na Mbezi kimara wao hawaagizani kitu.

Ukiamka unakuta mama kayayii kashachapa mwendo.

Jioni abakupigia simu anakuuliza etii Kimario, pale Marangu kuna mbuzi nzuri leo?
Ukijibu kwamba wapo wazuri, anakwambia, basi utanikuta hapo...au ushafika hapo tayari??!!

Daaaadeeeki.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom