Wanaoishi kwenye vurugu za ndoa wasiajiriwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaoishi kwenye vurugu za ndoa wasiajiriwe?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 23, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wanawake ambao wana vurugu za kindoa na hasa kufujwa na waume zao, huwa wanapoteza saa nyingi za kazi kwa kiasi cha asilimia 40 ukilinganisha na wanawake ambao ndoa zao hazina vurugu. Muda huo hupotezwa na kule kutokuja kazini kutokana na vipigo au madhara mengine na pia kutokuwa kazini kiakili kutokana na mateso.

  Wanawake ambao wako kwenye uhusiano au ndoa zenye vurugu huwa wanakabiliwa na matatizo ya kushindwa kuwa wazingativu, ufanyaji kazi wa polepole na pia kushindwa kabisa kufanya kazi katika baadhi ya nyakati.

  Ingawa matatizo haya yanatazamwa kwa wanawake, lakini pia kuna idadi ya kutosha ya wanaume ambao hushindwa kazi zao kutokana na matatizo ya ndoa na zaidi ni kwa wanaume walioshikwa na wake zao na ambao hawafurukuti mbele ya wake zao.

  Kutokana na kushikwa na wake zao, muda wao mwingi huutumia kuwafikiria wake zao au wapenzi. Lakini pia badala ya kufikiria kuzalisha hufikiria kupata zaidi ili kuwaridhisha wake au wapenzi wao .

  Kwa hiyo unapotaka kuajiri mtu inabidi pia uchunguze kama hafujwi au hajashikwa na mpenzi au mkewe. Kama ukigundua kwamba, ameshikwa au anafujwa, basi ujue kwamba kuna hasara inakuja upande wako
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,389
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  mkuu uko rught
  ila ni aina gani za ndoa unajua kuna ndoa nyingi zinafungishwa kanisan za majini lakini kutokana na wchungajiwengi kutokuwa na uwepo wa utambuzi wanaishia kuwavalisha pete majini..so hawa ni ngumu maana ujue shetan anamiliki dunia na wale wabaya wengi ndiowanaoishi maisha ya neema humuduniani ...
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Sep 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nimekupata mkuu, lakini, Je wale wanaoishi bila ndoa lakini maisha yao ya kinyumba yakawa na vurugu, inakuweaje?....................
   
 4. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hapo umenena mkuu, vurugu za ndoa husababisha hata uchumi wa nchi kuyumba.........
   
Loading...