Wanaoishambulia ACT-Wazalendo kujiunga SUK wajiulize kama CHADEMA hawajapokea ruzuku ya Novemba 2020

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Nimeshuhudia humu mitandaoni makamanda wakimshambulia sana Zitto Kabwe kufuatia chama chake kujiunga na SUK huko visiwani Zanzibar.

Kigezo ni kwamba CHADEMA na ACT-Wazalendo hawayatambui matokeo ya uchaguzi mkuu na wao wanaita "uchafuzi"

Wanachosahau makamanda wa CHADEMA ni kuwahoji viongozi wao kama hawajapokea ruzuku ya mwezi November kutoka Serikalini.

Ikumbukwe kuwa ruzuku ni zao la kura na idadi ya wabunge na madiwani ambao chama kimepata kwenye uchaguzi mkuu.

Natumai Matola na Salary slip mtauhoji uongozi kwa niaba yetu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hapa umewachokoza makamanda wa ufipa. Natanguliza pole kwa mapovu yatakayo kupata.

Lakni kwani ,makamanda mbona wanahangaika sana na mambo ya ACT? Zitto kaweka mambo wazi, kama hujaridhia na maamuzi ya chama,anzisha chama chako.

Hela ya usajili ni kama m20 tu hivi, sasa makamanda mkichangishana inatosha kabsa kuanzisha chama lenu la wavuta bangi. Ova
 
Nimeshuhudia humu mitandaoni makamanda wakimshambulia sana Zitto Kabwe kufuatia chama chake kujiunga na SUK huko visiwani Zanzibar.

Kigezo ni kwamba Chadema na ACT wazalendo hawayatambui matokeo ya uchaguzi mkuu na wao wanaita "uchafuzi"

Wanachosahau makamanda wa Chadema ni kuwahoji viongozi wao kama hawajapokea ruzuku ya mwezi November kutoka serikalini.

Ikumbukwe kuwa ruzuku ni zao la kura na idadi ya wabunge na madiwani ambao chama kimepata kwenye uchaguzi mkuu.

Natumai Matola na Salary slip mtauhoji uongozi kwa niaba yetu.

Maendeleo hayana vyama!
Suppose kuchukua ruzuku ni vibaya.

Two wrongs do not make a right.
 
Kuna jambo huko Lumumba hamlielewi, mnadhani pesa ya ruzuku ni ya kwenu, wacheni kujidanganya, ruzuku ni pesa za walipa kodi wanazokatwa na serikali; hiyo sio pesa ya serikali ya CCM, ni pesa ya wananchi hivyo Chadema wana haki ya kuichukua.
 
Siasa ni sayansi.

Waacheni ACT wazalendo wachape kazi Zanzibar!
Hizi kauli za "siasa ni sayansi" naona unazitumia kuhalalisha uhuni mliofanya kwenye uchaguzi mkuu, sayansi siku zote inahitaji matumizi ya akili nyingi, nyie hizo akili hamna, ndio maana mkafanya maigizo ya kishamba.

Hivyo mlichokifanya nyie haikuwa sayansi iliyothibitishwa na yenye viwango ulimwenguni, ule wenu ulikuwa ni ushirikina.
 
Hizi kauli za "siasa ni sayansi" naona unazitumia kuhalalisha uhuni mliofanya kwenye uchaguzi mkuu, sayansi siku zote inahitaji matumizi ya akili nyingi, nyie hizo akili hamna, ndio maana mkafanya maigizo ya kishamba.

Hivyo mlkchokifanya nyie haikuwa sayansi iliyothibitishwa na yenye viwango ulimwenguni, ule wenu ulikuwa ni ushirikina.
Akikusikia Halima James Mdee atakucheka bwashee!
 
Kwahiyo mmeyakubali matokeo ya uchaguzi?
Hakuna uhusiano kati ya kukubali matokeo na kuchukua ruzuku, matokeo feki ya uchaguzi yalitangazwa na NEC ya CCM, hayo hayatambuliki, pesa za ruzuku ni kodi halali wanazokatwa wananchi wa taifa hili na serikali, hivyo serikali kama wakusanyaji ni wajibu wao kuvipa ruzuku vyama vyote vinavyostahili, na hili ni takwa la sheria sio mapenzi ya CCM, narudia tena hakuna uhusiano kati ya kuyakubali matokeo na kuchukua ruzuku.
 
Back
Top Bottom