BRELA inakimbiza wawekezaji

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,561
BRELA INAKIMBIZA WAWEKEZAJI.

Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241

Mfumo kama mfumo wa kusajili kampuni ni mzuri na unarespond haraka ila watendaji bado kabisa.

Nitatoa mfano na sina shaka kila mdau ambaye anasajili ama amewahi kusajili kampuni au biashara kupitia mfumo mpya wa Brela atakubaliana nami.

Ni hivi, unakamilisha docmnts na kusubmit online Brela. Unasubiri majib na baada ya muda unajibiwa ufanye marekebisho(Additional Information/correction is required.

Unafanya marekebisho yote uliyoelekezwa na unasubmit upya. Baada ya siku au siku mbili dcmnt zinarejeshwa tena kuwa ufanye tena marekebisho(Additional Information/correction is required.

Kinachouma sana na kukera sana ni kwamba haya marekebisho unayoambiwa ufanye kwa hii mara ya pili ni MAPYA. Kwa maana dcmnt zilivyorejeshwa mara ya kwanza hayakuwa matatizo ila mara ya pili yameonekana ni matatizo.

Unarekebisha mara ya pili na kusubmit tena. Unasubiri tena siku ama siku mbili au zaidi. Inarudishwa tena ikihitaji marekebisho(Additional Information/correction is required.

Haya ya mara ya tatu nayo unakuta ni MAPYA. Maana yake hayakuonwa uliporudishwa mara ya kwanza, hayakuona uliporudishwa mara ya pili yameonwa mara ya tatu.

Unarekebisha tena na kusubmit. Unasubiri tena siku ama siku mbili au zaidi. Inarudishwa tena ikihitaji marekebisho(Additional Information/correction is required.

Haya ya mara ya nne nayo ni marekebisho MAPYA.
Maana yake hayakuonwa uliporudishwa mara ya kwanza, hayakuona uliporudishwa mara ya pili, hayakuona uliporudishwa mara ya tatu, sasa yameonwa mara ya nne.

Mchezo unaendelea hivyo mpaka mwezi au zaidi. Halafu unasikia Mtendaji Mkuu wa Brela inaiambia Serikali, Dunia, na Wawekezaji kuwa sasa Tanzania Brela inasajili Kampuni na Biashara ndani ya saa 24. Ni aibu sana.

Hoja sio kwamba marekebisho yasifanywe ama usajili ufanyike bila sifa kutimia, Laa hasha.

Hoja ni kwamba, huyu anayesoma dcmnt na kuzirejesha anashindwaje kupitia dcmnt nzima yote kwa umakini, akaorodhesha yoooote yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho, ukairudisha ili yote yafanyike kwa pamoja.

Inakuwaje marekebisho yasionwe dcmnt ziliporudishwa mara ya kwanza yaje kuonwa mara ya pili na ya tatu na kuendelea.

Na bora ingekuwa kwamba kile ulichoambiwa kurekebisha umekirekebisha vibaya kwahiyo unatakiwa ukirekebishe vizuri zaidi, hapana. Hiki ulichoambiwa kurekebisha kinaachwa kwa maana kuwa umekirekebisha vizur unaletewa kipya kabisa ambacho hakikuwa kimeonwa mara ya kwanza, ama ya pili, ama ya tatu. Ni kero, usumbufu, na aibu kwa watendaji.

Msichojua ni kwamba wengi wanaosajili Makampuni na biashara ni Wawekezaji.

Anakuja mwekezaji kutoka nje unamuhakikishia kuwa ndani ya siku moja,mbili,tatu utakuwa umemsajilia Kampuni. Anasubiri siku, wiki, wiki mbili, tatu, mwezi mwezi na zaidi hakuna kitu.

Mimi kama Wakili, ama mtu mwingine aliyepewa kazi ya kusajili siwezi kukubali kuaibika kwa mteja wangu. Nitamwita, nitamuonesha majibu ya Brela kwenye system. Nitamuonesha marekebisho mapya ambayo hayakuwa yameletwa mwanzoni yanavyoletwa kila baada ya siku mbili au wiki.

Ataelewa kosa sio langu ni la BRELA. Ataondoka sababu hawez kusubiri zaidi anaingia gharama kubwa za Malazi. Ataenda kufungua Kampuni Rwanda au Kenya ambako kwa dhati yake kampuni inasajiliwa ndani au chini ya Saa 24. Hivi ndivyo tunavyopoteza wawekezaji kupitia Brela.

Lakini ni kero zaidi sababu kila marekebisho yanahitaji wanahisa ama wakurugenzi wasaini. Utawaita kusaini mara ngapi. Na vipi kama walisaini wakaondoka na kwenda mbali.

Kuna mda unawaza labda pengine aliyepitia kazi mara ya kwanza siye aliyeipitia mara ya pili, na siye aliyepitia mara ya tatu, pengine ndo maana kila mtu ametaka marekebisho yake tofauti.

Kama ndivyo, basi hiki ndicho kirusi chenyewe. Ina maana Brela haina STANDARD moja ya kazi kiasi kwamba kila mtu ana marekebisho yake. Yaani marekebisho sio STANDARD bali mtazamo wa mtendaji. Utumishi wa hovyo na wa Kijima kabisa.

Inakuwaje jambo ambalo jana mtendaji fulani alipitia na kuliona sio la marekebisho, mtendaji aliepitia leo akaona ni la marekebisho, na mwingine anayepitia kesho kutwa akaona jingine ambalo wa jana hakuona, na mwingine wa mtondogoo akaona jingine ambalo wa juzi hakuona, hivyo na hivyo na kuendelea. Wallah kazi haziwezi kufanyika hivyo. Huu ni mchezo na masihala.

Au mpaka mtu amuone mtu, ujinga mtupu. Waulizeni wadau wa usajili hasa Mawakili na Wanasheria kama hiki nilichoeleza ni tatizo ama hapana mtapata majawabu.

Tunataka mtu akisubmit kazi, mtendaji anayeshika hiyo kazi aipitie kwa umakini na kuainisha marekebisho yooote lwa pamoja(kama yapo), na asiache hata moja.

Kisha arejeshe hiyo kazi ili yafanyiwe marekebisho na mhusika. Kama yamerekebishwa vizur mpatie Certificate. Kama sio mrejeshee tena yale yale yamaliziwe na sio umletee mapya.

Ukileta mapya tafsiri yake ni kwamba ile mara ya kwanza hukupitia kwa umakini. Ulizembea na hiki ndicho tunachopinga kwa nguvu zote. Kampuni itachukua mwezi na zaidi kusajiliwa.

Pengine hamjui umuhimu wenu katika Uwekezaji Tanzania. Ni hivi, Brela ndio mlango ama hodi ya uwekezaji. Sababu mwekezaji hawezi kwenda hata TIC au Immigration kama hana certificate ya Brela. Mwekezaji lazima aanzie Brela kwanza ndo aende kwingine.

TAFADHALI Brela Acheni Kukimbiza Wawekezaji.

Zaidi, soma: BRELA ( Business Registration and Licensing Agency) kuna matatizo makubwa! Waziri wa Viwanda na Biashara tunakuomba uingilie kati haraka!

Pia soma >Ufafanuzi juu ya madai ya BRELA kukimbiza wawekezaji
 
Inasikitisha sana kwa kweli BRELA Mimi binafsi niliwahi kuongea na kiongozi mmoja mwandamizi wa BRELA alichonijibu ulikua ujinga maana alikua anaongea na mimi kama vile anaongea na mimi kama mtu ambaye hajui chochote katika dunia hii. Yaani kwa kifupi alishindwa kutatua shida yangu, akashindwa kunipa majibu na kubaki anarukaruka tuu sababu anajua anachokifanya sio sawa ila anazidi kukitetea.

Tunajua mmekatiwa mirija ya seminar na safari zisizokua na tija, overtime na pesa nyingine nyingi mlizokua mnaidhinishiana. Mnachotakiwa kujua ni kwamba mirija haijakatwa kwenu tuu bali ni kwa kila mtanzania aliyekua anakula haramu aliyoihalalisha kwa tamaa zake.
Sasa msiendelee kuwakwamisha wawekezaji sababu hawa ndio wanakuja kuwapa watu ajira na kuongeza pato la taifa

BRELA sio kwamba hawajui hili tatizo, wanalijua sana na wanajua likitatuliwa hawatapata mwanya wa kupata chochote kitu kwa wateja.
Na kitu ninachojua mimi ni kwamba huu uhujumu unafanywa wale maofficer wa chini wanawasiliana moja kwa moja na wateja wakisaidia na supervisors wao.
Hiyo online system yenu mnayopambana kui customize ili muendelee kuwabana wateja inawaumiza wao leo lakini itakuja kuwaumiza nyie kesho. Acheni hizo mambo

Wakurugenzi, Makatibu wakuu, Mawaziri wengi hawajui hii michezo wanaamini wanayokubaliana kwenye vikao ndiyo yanayotekelezwa kumbe huku chini wateja wanaumia sana.... wa kuweza kuvumilia usumbufu wa kusajili kampuni miezi6 hadi mwaka wanavumilia, na wasioweza wanapeleka mitaji yao nchi zingine zisizokua na hii bureaucracy

Inasikitisha sana kuona serikali inatumia nguvu na pesa nyingi ku automate systems ila wajuzi wa yale mambo ya kitukidogo wanashauri parts za system ziwe manual kwa sababu za hovyo kabisa. Ukweli ni kwamba hawataki kulifanyia kazi maana system ikikaa vizuri itawanyima ulaji. Mamlaka nyingi zimegeuka kuwa vijiwe vya kuhujumu juhudi za serikali.

Yaani baada ya rais John Pombe Magufuli kuwashinda wahujumu wa nje ya system, sasahivi wale anaowajali na kuwapa kazi, na kuwalipa mishahara tena mapema kabisa tarehe 21 ya kila mwezi ndio wamegeuka wahujumu wakuu.

Taasisi zilizokua zinaongoza kuitukanisha serikali kwa wawekezaji wageni na wazawa 2020 ni BRELA, TRA, TIC, ARDHI-Uwekezaji na Halmashauri zetu. Yaani ingekua wakupewa medal hawa ndio top5 ya wanaoongoza kutuhujumu watanzania, wageni, mamlaka ya rais na nchi kwa ujumla.

Hebu fanyeni kazi buana. Mnatukwaza wenzenu maana bila uwekezaji sio sisi wala nchi inaweza kuendelea.

fundi25 nasema uongo ndugu yangu?

Cylia
 
Nilishawahi kukutana na hiyo kadhia nikakamilisha baada ya wiki tatu.

Ila nadhani inategemea nyaraka zako kazipokea ofisa yupi. Mimi kuna mfano niliwahi sajili moja kwa siku mbili haikua na tatizo kabisa.

Ila nachoona wanapaswa kufanya ni hiki application ikitumwa brela ofisa atayeipokea mwanzo awe huyo huyo mpaka itakapotoka kwenye stage ya recommendations, itapunguza aina hiyo ya matatizo.

Otherwise online registration ni idea nzuri kabisa, ila wajitahidi kurekebisha hilo tatizo kwani linasumbua Sana na hasa ukiwa na client ambaye ni very demanding. Naelewa Sana unachozungumza mkuu.

Niliwahi pia kuandika uzi kuhusiana na hilo.

 

Hii ilifikia wapi kwanza muheshimiwa?au uliitwa chamber ukatokea mlango wa uwani kimya kimya?
 
Inakuwaje marekebisho yasionwe dcmnt ziliporudishwa mara ya kwanza yaje kuonwa mara ya pili na ya tatu na kuendelea.
Afadhali wewe kila unaporudishwa unapewa makosa mapya.

Mie nilirudishwa mara nne kwa kosa hilo hilo,kila nikirekebisha jamaa anajifanya kama hakuona nilichofanya

BRELA ni ya kuvunja na kuleta watu wapya mpaka mfagizi, tutapata tabu kwa muda tu, lakini watatusaidia
 
Jamaa hawajielewi kabisa wanapaswa kuondolewa wote waweke watu wanaojua kazi vizuri.

Magu ameshasema watu wanaikwamisha kazi watolewe,w aanze na kiongozi wao hapo Brela wamng'oe awekwe mtu anayejua kusimamia kampuni zisajiliwe haraka watu wanataka kufanya kazi walipe kodi
 
Serikali inataka kuwa mpya kwa Watendaji walewale.

Hakuna tofauti na vita ya rushwa...Watendaji ni wale wale...WALE WALE (in Dokta Remi's voice).
 
Jamaa hawajielewi kabisa wanapaswa kuondolewa wote waweke watu wanaojua kazi vizuri.......
Magu ameshasema watu wanaikwamisha kazi watolewe......
waanze na kiongozi wao hapo Brela wamng'oe
awekwe mtu anayejua kusimamia kampuni zisajiliwe haraka watu wanataka kufanya kazi walipe kodi
Halafu jambo jingine naona wanapaswa kufanya ni kuigeuza Brela kuwa wakala wa manispaa kwamba zile leseni za manispaa ziwe zinatolewa hapo hapo Brela wanawapelekea hela zao manispaa, kuliko ukishamaliza brela kupata CR unakwenda tena manispaa kuanza mchakato mwingine upya inachosha in some ways.
 
Afadhali wewe kila unaporudishwa unapewa makosa mapya.
Mie nilirudishwa mara nne kwa kosa hilo hilo,kila nikirekebisha jamaa anajifanya kama hakuona nilichofanya
BRELA ni ya kuvunja na kuleta watu wapya mpaka mfagizi,tutapata tabu kwa muda tu,lakini watatusaidia
Wanataka rushwa hao, ukimwona pembeni hayo makosa hutoyaona
 
Afadhali wewe kila unaporudishwa unapewa makosa mapya.
Mie nilirudishwa mara nne kwa kosa hilo hilo,kila nikirekebisha jamaa anajifanya kama hakuona nilichofanya
BRELA ni ya kuvunja na kuleta watu wapya mpaka mfagizi,tutapata tabu kwa muda tu,lakini watatusaidia

Tena hao watu wapya wawe ni wanaccm, maana ndio wazalendo.
 
Sisi tuliambiwa tuko vizuri na wawekezaji wanamiminika ukizingatia corona ilipotezwa kwa maombi na fursana kutoka Antananarivo au nasema uongo ndugu zangu?
Nakumbuka wakati ule wa kupiga kura kuna watu hapa JF walipiga picha makaratasi kwamba wamemchagua Tundu huku wakiwa na kadi za CCM pembeni ya karatasi za kura na kidole chenye wino

Sasa wale ndio baadhi ya hawa wanaoendeleza hujuma ndani ya mifumo ya serikali
 
Mkuu uko sahihi kabisa. Nina miezi kadhaa nafanya annual return isiyokamilika. Kila mara unaambiwa ufanyie marekebisho/nyongeza ambazo toka mwanzo hazikuonekana. Yaani ni kama mnafanya mchezo wa kujibizana usiokwisha
 
Back
Top Bottom