Wanaoingilia njia ya Mabasi Yaendayo Kasi DSM washtakiwe kwa kuhujumu uchumi!!!

fredito13

JF-Expert Member
Sep 3, 2012
213
146
Inashtua kiasi kuona baadhi ya madereva kwa kukosa utashi wa kidereva wanavamia njia za mabasi yaendayo kasi kila mara wanapoona kuna foleni ndefu! Uvamizi huu umepelekea baadhi ya mabasi hayo kugongwa au kupunguza spidi pale inapotokea gari (hasa daladala) lililovamia njia linahangaika kutoka!
Hakuna dereva wa DSM asiyejua kuwa barabara zile zimetengenezwa kwa ajili ya mabasi maalum ya kwenda kasi! Uvamizi hua ni wa makusudi kabisa kwa dereva kujua hata kama atakutwa, basi ataishia kutozwa faini ndogo tu ambayo haimuumizi kichwa!
Ili kuulinda Mradi na kufanya uwe endelevu, na pia kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu, napendekeza serikali ianzishe adhabu kali kwa wale wote watakaopatikana wakitumia njia hiyo. Adhabu pendekezwa ni pamoja na

1. Kutaifisha gari itakayokutwa inatembea au kugonga mabasi yaendayo kasi kwenye njia yake
2. Kifungo kisichopungua miezi 6 kwa dereva husika kwa kosa la kuhujumu miundombinu ya usafiri na uchumi wetu. Lakini pia kuhatarisha maisha yake mwenyewe na abiria/watumiaji wa barabara kwa makusudi!

Makosa haya yasiwe na adhabu za faini ila yote kwa wakati mmoja au adhabu moja moja!

Vinginevyo, ndani ya miaka mitatu mradi ule utakua historia tu!!!
 
Wenye kuuua mradi ndo wenye daladala. Madereva hao wanyang'anywe leseni na wasipewe maishani
 
1462363722288.jpg

Kama hivi mkuu.
 
Wenye kuuua mradi ndo wenye daladala. Madereva hao wanyang'anywe leseni na wasipewe maishani

Hatuna mfumo mzuri wa kuzuia leseni! Leo hii nikinyang'anywa leseni na traffic pale Mikese Morogoro, nikifika Moro town natoa taarifa ya kudondosha leseni yangu na hapo hapo naenda TRA kufuatilia ingine! Ndani ya 48hrs Nina leseni mpya na ile ya zamani nawaachia traffic! Adhabu Za kifungo na kutaifisha mali zitaturudisha kwenye mstari
 
Back
Top Bottom