kichoroba89
Senior Member
- Oct 3, 2019
- 197
- 57
Waziri Mwakyembe ameongelea kuhusu wasanii kujielimisha hasa wanapokosoa jambo lolote kwasababu ndio vioo vya jamii. Wasanii waendelee kujielimisha ili waweze kukosoa kwa weledi kwani wananchi walio wengi wanawakubali wao kupitia muziki.
Hivi hao wanaokasirika kuhusu kauli ya Mwakyembe kusema wasanii wakajiendeleze zaidi, alimtaja nani hadi watu wanakuja juu kama moto wa kifuu?
Acheni hizo wadau, ukitajwa jina lako payuka lakini kama hujatajwa nadhani upige kimya. Waziri kasema vizuri mtu atashitakiwa pale atakapokwenda kinyume na utamaduni wa kitanzania lakini sio kwa kuikosoa serikali, ila unapokosoa pia kosoa kwa weledi sio kwa matusi halafu unasema umeikosoa serikali, unafikiria matusi nani atakusikiliza zaidi ya kukuweka ndani?
Badilikeni.