Wanaoimizwa na kauli ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ujue imewagusa

kichoroba89

Senior Member
Oct 3, 2019
197
225
Waziri Mwakyembe ameongelea kuhusu wasanii kujielimisha hasa wanapokosoa jambo lolote kwasababu ndio vioo vya jamii. Wasanii waendelee kujielimisha ili waweze kukosoa kwa weledi kwani wananchi walio wengi wanawakubali wao kupitia muziki.

Hivi hao wanaokasirika kuhusu kauli ya Mwakyembe kusema wasanii wakajiendeleze zaidi, alimtaja nani hadi watu wanakuja juu kama moto wa kifuu?

Acheni hizo wadau, ukitajwa jina lako payuka lakini kama hujatajwa nadhani upige kimya. Waziri kasema vizuri mtu atashitakiwa pale atakapokwenda kinyume na utamaduni wa kitanzania lakini sio kwa kuikosoa serikali, ila unapokosoa pia kosoa kwa weledi sio kwa matusi halafu unasema umeikosoa serikali, unafikiria matusi nani atakusikiliza zaidi ya kukuweka ndani?

Badilikeni.
 

lukesam

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
10,683
2,000
Kwanini wanaposifia serikali hawaambiwi wakajielimishe kwanza ndio waweze kusifia wanavyovijua? Hao wnaoimba mapambio ya kusifu wameelimika?

Unazijua kazi za mbunge? Sifa ya kuwa mbunge ni kujua kusoma na kuandika tu,je hao nao kama washauri wa serikali na wakosoaji pia ni lini huyo Waziri amewataka wakajielimishe?

Ukiwa mjinga usilazimishe kila mtu afanane na wewe!
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
12,071
2,000
Watu wanaumizwa na maajabu ya Elimu yetu ya watanzania

1. Baba na mama, babu na bibi pia ndugu hawana hiyo Eilimu lakini:-

Ukirudi nyumbani rikizo hao ndio
-washauri wako... olewa na wale, tafuta mke kabila lile, nunua shamba, wekeza hapa nk
-watakao kuonya, usimdharau huyo, acha uhuni, usifanye kibri kazini, Siku zote majuto mjukuu nk

2. Bungeni mathalani
Kumejaa wengi darasa la saba, hawa akina msukuma, kibajaji nawenzao ndio washauri wa waziri huyu na kumpangia bajeti!

3. Viongozi wa dini
-Sijuwi aendapo kanisani anauliza kama mchungaji au wazee wakanisa wana degree ili wampe mafundisho kwa degree zao?
- Anapohudhuria shughuli mbalimbali za kitaifa, kidini, kitaasisi nk wale wachungaji, mashekh na wazee wa kimila huwa wamesoma hayo madegreee?

Kinachowaumiza watu nikuona waliemuamini kuwa msomi mwanasheria amekosa sifa zakisomi tena sana tu

A) kaidharau katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania......katiba inatambuwa uwakilishi wa wabunge darasa la saba....
kwamba
watatunga sheria
Wataisimamia serikali
Watajadili, kushauri na kupitisha bajeti
Wataonya na kusimamia maadili

B) kawadharau
-wapiga kura wake wote wake kwa wanaume
-kawadharau watanzania, wengi wetu hatuna hayo madegree lakini tunamlipa mshahara nk

Huyu ndie mwanasheria msomi na waziri!!!
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
14,161
2,000
kichoroba89,
Kamwambie mumeo imekula kwenu, alipolishwa sumu aliimba mapambio kama haya? Mbona hatukusikia akisema hawezi kupewa sumu na wenye Elimu ndogo, wakati alipewa sumu na PS tu tena form 4 mwenye cert ya uhazili?
 

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,670
2,000
Kamwambie mumeo imekula kwenu, alipolishwa sumu aliimba mapambio kama haya? Mbona hatukusikia akisema hawezi kupewa sumu na wenye Elimu ndogo, wakati alipewa sumu na PS tu tena form 4 mwenye cert ya uhazili?
Imekutachi mkuu, uzi wako huu umegonga mfupa.
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
29,280
2,000
Kijana mmoja msanii mwenye elimu ya hapa na pale yaani darasa la 7 aliimba wimbo wake, akamuimba mtu mwenye degree zake 4 humo kwny huo wimbo.

Aliimba 'mwenye degree 4 baba lao' na kumbe mwenye degree zake 4 ana 'aleji' na wenye elimu ya la 7b na sasa mwanamuziki huyo anatamani kumfuta PHD huyo kwny wimbo wake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom