Wanaoihujumu Yanga ni Bwana Chacharito, Baraka Desdeudit na Salum Mkemi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,399
Tokea kujiudhuru kwa aliyekua mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji mambo ndani ya klabu hiyo yameendelea kuwa ovyo baada ya kundi la wajanja wachache kutumia nafasi hiyo kupiga hela nje nje.

Jezi mpya za Yanga zinazotengenezwa na mshonaji nguo Speshoz kupitia jina la Bongoz zinauzwa kama njugu kwa wanachama wasiojua kuwa klabu yao haipati chochote.

Jezi hizo ni mpango wa mjumbe wa kamati ya utendaji, Salum Mkemi ambaye awali Manji alimsimamisha uanachama wake kabla ya kurejeshwa na Katibu Mkuu Mkwasa, anauza jezi hizo kama njugu kwa bei ya elfu 35 kwa pea moja, na mauzo ya jezi hizo anajua yeye mwenyewe Mkemi anakopeleka.

Biashara hiyo inafanyika hadharani, viongozi wa Yanga wanatazama kiongozi mwingine akijipatia fedha ambazao kama zingeingia kwenye mfuko wa klabu basi zingeweza kusaidia matatizo madogo madogo ya kiutawala.

Duniani biashara ya jezi ndo huviingizia mapato makuba vilabu, lakini kwa Tanzania ni tofauti wanaofaidika ni wengine kupitia majina ya taasisi hizo, kidogo Simba na Azam wamepiga hatua kwa kufungua maduka yanayouza vifaa vyao.

Wakati hilo la jezi likiwa na takribani miezi mitatau sasa tangu kuanza kuuzwa, watendaji wengine wameendelea kudaia percent kwenye usajili wa wachezaji.

Salim Hoza aliyetua Azam alikubaliana na uongozi wa Yanga kusaini kandarasi ya kuitumikia kwa makubaliano ya kutanguliziwa mil 5 kisha kumaliziwa baadae pesa yake nyingine ya usajilli, ajabu mtu anaefahamika kama Godlisten Chacharito alipewa jukumu hilo na kumpa Hoza mil 4.5, akizuia laki 5, hali iliyomfanya mchezaji huyo kuamua kutimikia Azam kimya kimya.

Mwaka jana Yanga ilipigwa faini kwa kuchelewa kukamilisha usajili na TFF baada ya kumalizika siku 68 za usajili ilijikuta haijafanya usajili kwenye mtandao na kama si huruma ya TFF basi timu hiyo ilipaswa kushushwa daraja na si kutozwa fainai.

Aliyekua Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Desdeudit alishidwa kufanya usajili wa Hassan Kessy pia ukiwa na pingamizi liliopelekea mchezaji huyo kuchelewa kuitumikia Yanga mpaka kesi yake ilipotolewa uamuzi na kamati husika, kwa kupigia faini Yanga kwa kumsainisha mchezaji mkataba ili hali mkataba wake ukiwa haujamalizika.

Baada ya Niyonzima kushindwana na uongozi wa Yanga jumatatu usiku, uongozi ulipanga kutoka taarifa kwa umma mapema juu ya suala hilo, lakini kabla hilo halijafanyika Baraka Desdeudit alimpigia simu Niyozima na kumuambia asajili Simba haraka, kwani kuna mpango wa kukutangaza kuwa tumekuacha.

Kwa maana hiyo Niyonzima alisaini haraka Simba kuogopa kutangazwa katemwa, sababu kungemshushia hadhi yake, ila aliyetoa siri hii kwa mchezaji huyo ni Baraka Desdeudit ambaye hata mie kwa sasa sielewi cheo chake ndani ya Yanga ni nani, maana alikua akikaimu Ukatibu, kabla ya Mkwasa kuajiriwa.

Wana Yanga naomba tujulishwe nafasi ya Chacharito na Baraka Desdeudit ndani ya klabu, maana vyeo vyao havijulikani na inasadikika ni mamluki wanaotumika kuidhofisha Yanga.

Ni ukweli usiofichika, mpaka sasa Yanga haijafanya usajili wa maana, Niyonzima kaondoka, Kamusoko, Bossou, Ngoma, Oscar, Barthez mikataba yao imemalizika, wakati viongozi wengine wakihangaika kwa chochote walicho nacho kuweza kuwapata wachezaji hao, wanapopewa jukumu hilo wanageuka madalali.

Kutoka kwenye ushangiliaji mpaka kupewa majukumu makubwa ya usajili ndani ya Yanga hiki ni kituko kingine, anapata wapi staha kama alikua mshabiki muongea ovyo? Yanga haina siri tena kutokana na kila aliyepo kutaka kuonekana anajuana sana na wachezaji, viongozi wakati uhalisia ufanisi wa kazi hakuna,

Taarifa za klabu ya Yanga sasa zinapatikana kwenye mitandao yao (blogs) na akaunti zao binafsi Instagram, twitter na facebook, whatsapp wana Yanga wangapi wanaweza kupata taarifa hizo kwa kusoma kwenye akaunti zao?

Aah ngoja niishie apa kwa leo, kwa aina hii ya viongozi hao waliopo klabu ya Yanga kwa sasa sioni maendeleo yoyote, kama maendeleo ni Ubingwa wa Ligi Kuu si sawa, sababu ubingwa huo ulishachukuliwa zaidi ya mara 27.
 
hakuna kitu imeniuma kama kuondoka kwa NIYO
 
Yanga safari hii wakubali tu yaishe,watafungwa kama watoto wadogo
cc OKW BOBAN SUNZU,Erythrocyte
 
Wachawi wa maendeleo ya vilabu vya Simba na Yanga ni viongozi waganga njaa.

Vilabu ni vikongwe lakini havina hata viwanja vya mazoezi.....!!!!!

Hivi vilabu havitakuja kuendelea kamwe kwa hawa viongozi wetu wenye uswahili waliopo.

Pamoja na kuwa ni mshabiki wa Yanga lakini huwa nashanga sana mchezaji anayeacha kwenda Azam halafu anasini Simba au Yanga.
 
Huu ni uzushi wa kiwango cha lami huyo hoza kaka yake ambae ni meneja wake amekanusha hiyo kitu na pesa alizopewa kapewa kwa risiti ya club alipofuatwa na azam akarudisha ml5 pamoja na gharama za ndege za aliokwenda mwanza kumsainisha acha unafiki mkia wewe
 
Mkuu kaka yake gani Abou..? Nikupe namba yake umuulize vizur..?
 
Mchawi wa Yanga ni Jonas Tiboroha

Subirini taarifa zake zitakuwa wazi siku si nyingi. Mipango yote ya akina Niyo na Ngoma ni yeye anasuka na Kaburu
 
Punguzeni majungu,Niyonzima ameondoka sababu Simba wamempa dau kubwa kuliko Yanga.Dr Tiboroha aligombana na Niyonzima na ndio alitaka kumuondoa Niyonzima Yanga Manji akaingilia kati na kumfukuza,leo mnaleta story Dr Tiboroha ndio ammempeleka Niyonzima Simba
 
Mchawi wa Yanga ni Jonas Tiboroha

Subirini taarifa zake zitakuwa wazi siku si nyingi. Mipango yote ya akina Niyo na Ngoma ni yeye anasuka na Kaburu
Huyu kenge si alijifanya kumtimua Niyonzima kipindi flani leo kageuka malaika kwa Niyonzima dah
 
Mkuu kaka yake gani Abou..? Nikupe namba yake umuulize vizur..?
Ya kazi gani unafikiri yale mambo ya kukabidhiana hela kama zawadi yapo yanga sasa hivi? Huyo niyonzima mwenyewe kaondoka yanga sbb ya madalali hao mikia wenyewe wanajuta saaa hivi jinsi walivyopigwa baada ya yanga kumpa makavu
Yule hoza alipewa ml 5 hata kaka yake amethibitisha lkn tamaa ya familia ndio iliyoharibu baada ya azam kwenda na dau kubwa zaidi halafu cash sio nusu kama yanga mengine majungu tu na umbea.
Tiboroha ndio kidudu mtu na mnafiki kaka wewe hata msuva alitaka kumpeleka mikia kwa kisingizio anakwenda nje alifikia mpaka kwenda kuvunja mkataba kwa kisingizio cha kutolipwa miezi mitatu akagongwa mwamba baada ya kukuta hakuna madai ya mshahara
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom