Wanaoifahamu Iringa DC, mumsaidie huyu mwalimu ajira mpya aliyepangwa huko

MTABO

Member
Mar 6, 2014
95
57
Mwalimu kapangiwa:
  • Mkoa wa Iringa
  • Iringa DC
  • PAWAGA secondary school
anahitaji kujua kuhusu haya:
  • mahali zilipo ofisi za halmashauri husika.
  • nauli kutokea mkoani hadi ktk halamashauri husika.
  • mahali ilipo shule uliyopangiwa.
  • nauli kutoka halamashauri mpaka shuleni ulipopangiwa.
  • uwepo wa huduma kama umeme, maji, nk
  • sio mbaya akijua kama huduma ya 3G ipo au haipo awapo shuleni, kwani amenunua simu ya smarphone kwa ajili ya ku-google concepts.
 
Umeme upo na Huduma ya 3g utapata mkuu!
Utakula ubwabwa sana pande hizo!
anyway hunabudi kumshukuru Mungu kuna watu wametupwa mbali hadi huruma!

pawaga mbona shavu sana
 
Umeme upo na Huduma ya 3g utapata mkuu!
Utakula ubwabwa sana pande hizo!
anyway hunabudi kumshukuru Mungu kuna watu wametupwa mbali hadi huruma!

pawaga mbona shavu sana
vipi. ofisi za Iringa DC zipo Iringa mjini, au zipo sehem nyingene ndani ya Iringa DC.
 
Hakuna baridi huko ni joto Kali sana ndio maana wanalima mpunga,nauri ni 3500 kutoka mjini ni sehemu nzuri sana kama unapenda mambo ya kilimo
 
Hakuna baridi huko ni joto Kali sana ndio maana wanalima mpunga,nauri ni 3500 kutoka mjini ni sehemu nzuri sana kama unapenda mambo ya kilimo
asante sana mkuu.
ila nitatumia muda gani kutoka iringa mjini mpaka pawaga.
 
Duh, shukuru sana Pawaga mkuu ni big deal, fundisha while unalima mpunga. 3D voda utaipata kama kawa. Mjini kabisa huko.
 
Duh, shukuru sana Pawaga mkuu ni big deal, fundisha while unalima mpunga. 3D voda utaipata kama kawa. Mjini kabisa huko.
vipi kuhusu kutoka iringa mjini hadi pawaga, kuna mwendo wa muda wa masaa mangapi?
 
Back
Top Bottom