Wanaohukumiwa vifo na vifungo vya maisha wanufaishe taifa badala ya kunyongwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaohukumiwa vifo na vifungo vya maisha wanufaishe taifa badala ya kunyongwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babylon, Sep 23, 2009.

 1. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kutokana na mifumko ya magonjwa yaliyojitokeza katika ulimwengu huu tulionao leo, ingekuwa jambo la busara kama nchi yetu ikafikiria njia za kuwatumia waliohukumiwa vifo ,wafungwa wa maisha ,majambazi na wabakaji ,watumike kwa kulifaidisha taifa ,kwa nikutolewa fursa kwa wachunguzi wa MAABARA kuwatumia katika majaribio ya madawa wanayotengeza kwa ajili ya tiba au kinga kwa binadamu mara tu zinapovumbuliwa na kuonekana tayari kwa majaribio kwa binadamu.
   
 2. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Asee hii kali kwelikweli yaani tunawageuza wanakua ka "panya" tatizo ukishakubali hapo unasikia haki za binadamu ziheshimiwe.....
   
 3. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  sasa haki ya mwenye kuliwa ipo wapi? na wapenzi wake yani familia, isitoshe wanalazimiswa kulipa kodi ambayo pia huenda kwa hao wafungwa au wahalifu waliokulia ndu au jamaa yako mpenzi .kodi hiyo inawafanya waishi maisha bora hata kuliko wewe ulioko uraiyani wanacho kosa ni kuwa miongoni mwa jamii tu lakini isitoshe wengi wao hufanya familia wakiwa humo jela kwa hiyo hawakosi sana uraiani.
   
 4. m

  mperwa Member

  #4
  Sep 23, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  lakini inakuwaje kuhusu haki za hao watu? ina maana ukishafungwa ndio huna haki tena au unakuwa unaweza kutumiwa kwa namna yoyote ile?, kumbuka kuna baadhi huwa wanaachiwa kwa msamaha, inakuwaje kama akiachiwa huru na alifanyiwa hayo na labda kuna madhara aliyapata?
  Kwa mfano wewe ndio ungekuwa mfungwa unachukuliwa kwa ajili ya majaribio ya kinga ya dawa fulani. utajisikiaje hapo? maana hilo ni jaribio tu lolote laweza tokea hapo(Mfano mtu aweza hata poteza maisha)
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Temea mate chini na uombe msamaha kwa mwenyezi mungu, kwani kila mmoja wetu ni potential criminal, leo uko free kesho hujui utakuwa keko au segerea.

  Kumbuka waliopo pale hawakupanga hata siku moja kuwa kufikia tarehe fulani watakuwa wafungwa. Wale ni binadamu kama wewe ni system tuliyonayo ndio imewafanya wawe wafungwa.

  Kamakeki ya nchi ingekuwa angalau ingawanywa vizuri hili wazo hata akilini mwako lisingekuja naona limekuja kwa sababu tayari umewaona wale sio binadamu tena na kama ni binadamu basi hawana kazi hapa duniani.

  Badilika kidogo.
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Sep 23, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Jamaa labda kasoma Urusi au China, tena enzi zile za Mwenyekiti Mao Zedong (Mao Tse-tung) na Nikolai Podgorny.
   
 7. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Utetezi wenu bado haujatowa hoja ya kuwatetea watu wabaya ndani ya jamii, leteni hoja zitakazo ingia akilini na mtu akaweza kuzitafakari.
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Sio wote waliohukumiwa gerezani ni wahalifu na si wote tulio huru nje ya magereza ni wasafi kiasi hicho. Tuanze kuwashughulikia wahalifu ambao wako huru baada ya hapo ndo tuendelee na wale waliopo magerezani.

  Pili waliopo magerezani wanatumikia adhabu utawapaje adhabu nyingine kwa kuwafanya labaratory fodder, mtu anahukumiwa mara moja kwa kosa alilofanya na sio mara mbili, ukiiangalia dhana yako inaleta kanuni ya kuadhibu mtu mmoja mara mbili kwa kosa moja.
   
 9. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  NN,

  Hapo kny bold...i like that.......look at fisadis...wanakula kuku mtaani tu, ukiangalia matatizo walioisababishia TZ ni zaidi ya mauji ya Albino.....so hao nao basi wakipatikana na hatia....tuwapeleke maabara kama ni hivyo!

  Kama ulivyomjibu mtoa maada hapo juu, watu hao kuhukumiwa kifo on one hand na kuamuliwa kutumika kwa manufaa ya taifa on another hand ni vitu viwili tofauti, hukumu ya kwanza (kifo) ni kwa mujibu wa sheria zetu, lakini hilo la pili halipo klwenye sheria kabisa, so kama tunataka hilo litendeke lazima tulitungie (au tubadilishe) sheria tena, sio kujiamulia tu from no where kuwatumia watu wale kwa namna nyingine as if wao sio binadamu kama sisi!
   
Loading...