Wanaohama kwenye vyama wapokelewe kwa tahadhari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaohama kwenye vyama wapokelewe kwa tahadhari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyange, Jul 23, 2010.

 1. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini, tumeshuhudia baadhi ya watu ambao walijiunga na vyama vya upinzani na kuviharibia mwelekeo. Tulimwona Augustine L. mrema, Dr. Masumbuko Lamwai, Mabere Marando, Makongoro Nyerere na wengine wengi. Lakini mambo yalikuwa tofauti na tulivyo tarajia, make kila waliko jiunga waliacha ugonvi na kutoelewana na pengine vyama hivyo kukumbwa na migogoro.

  Kwa maoni yangu, naomba Uongogozi wa Chadema kuwa makini na huyo Marando manake amechangia kwa kiasi kikubwa kudumaza upinzani. Wadau mnasemaje? Isije ikawa chanzo cha yeye kuvuruga Chadema.
   
 2. C

  Calipso JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa mtazamo wangu,

  Kutokana na dimbwi kubwa hivi sasa la wanaohama vyama vyao na kuhamia vyama vyengine,inanipa wasi wasi mkubwa sana.

  Inakuwaje mpaka huhama vyama tena inatokea kwa muonekano wa wazi kabisa, ama kupigwa na chini ktk nafasi wanazotaka kugombea, ama kwa kupunguzwa vyeo, ama kwa tofauti ambazo zipo ndani ya chama ambazo ni za lazima kwa kila chama,sasa najiuliza ni kwa utashi gani mtu mpaka anaamua kuhamia chama kingine?

  Ni kwa maslahi binafsi, au kwa msukumo wa maendeleo? Enzi za miaka ya nyuma, tukiona viongozi wakitoka CCM na kuunda vyama, lkn walionekana hasa ni wapigania ukombozi, je na hawa wa zama zetu hizi ni wapigania ukombozi?

  Kwanini tuendelee kuwapokea?
   
 3. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Toka lini ulianza kufanya utafiti kuhus viongozi wanaohama vyama baada ya kura za maoni. Kutokana na kuonewa baadhi yao hutokea kuwa watumishi wazuri kwenye vyama walivyohamia. Endelea kufanya utafiti uwagundue baadhi yao
   
 4. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Chadema kuweni na Tahazari Musigeuke Pakacha la Uchafu mukakumbatia kila mkimbizi wengine sio wana ageta za siri kukisambaraticha Chama.


  chadema jitahazarini sana na mamluki kutoka ccm, musisahaukuwa ccm ni Gangi la Mafia na wana kilambinu , hivi karibuni Cuf walitaka kulizwa na Hamad Rashid na Gangi lake kwanjama ya kutaka kuvivuruga cuf.


  Viongozi wa Ccm Bara/ na Visiwani Zanzibar hivi sasawametaharuki na kuona nguvu ya Chadema inavyo kuwa siku hadi siku na kipimokizuri ni Uchaguzi wa Arumeru na Uzi Zanzibar kujinyakulia nafasi ya pili Chadema kinapanda Chart na Nguvu kubwa kwa kukubalikanchi nzima.

  Imefika hadi hata Zanzibarkuna harufu ya kukubalika sera zao na hata Ccm/Smz wanahofu ya Sera za Chadema kuhamia Zanzibar na kuwapiku kwa vile Cuf hawana siasa tena nikugawana wizara tu Zanzibar.

  Kwa hio Smz wana hofu kuwa sera za Chadema zikivuka Bahari basi watakuwa na kibarua kigumu kwa vileviongozi wa Chadema wako ngangari na siwatu wa kuwatongoza kwa kuwahonga pesaau kuwa pa madaraka.

  Madaraka ya Chadema yanatokana na jitihada zao na nguvu mbele ya Wananchikwa hio hivi sasa hofu imetanda Zanzibarna viongozi wote tumbo joto.
   
 5. N

  NGAGHE Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana jf,sina imani na ujio wa James Ole Millya CDM. Anaweza kupandikizwa na magamba ndani ya CDM baadaye aje asaidie kuisambaratisha CDM kama walivyoifanya NCCR-MAGEUZI baada ya uchaguzi wa 1995 na kupelekea Mrema kukimbilia TLP baada ya kupandikiziwa mamluki.Wanajanvi mnasemeaje hili?
   
 6. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Usiwe na wasiwasi na hilo pale chadema kama ni pandikizi utajulikina mapema sana na hutashirikishwa chochote,kuna inteligensia ya kutosha,kama una wasiwasi muulize Shibuda mpango wake wa kuwa m/kiti cdm umeishia wapi?,atakwambia hata yeye alitumwa na akafanikiwa kuwa mbunge lakini hata ratiba ya vikao vya chama havijui wala hamna anayemsemesha, huyu dogo hata kama katumwa akijivalisha ngozi ya kondoo mpaka 2015 tutamsimamisha simanjiro tuchukue jimbo tukimstukia ni mamluki atajikuta yuko mwenyewe.
   
 7. n

  nmaduhu Member

  #7
  Apr 18, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF,

  Kila anayefuatilia siasa za hapa nyumbani anajua nchi yetu inapitia kwenye mageuzi makubwa ya kisiasa huku CCM ikiangamia, CHADEMA wao wanashamili kwa afya. Kwa sasa Chadema wamekuwa wakivuna wanachama toka CCM, binafsi jambo hili sio zuri kwa chama kinachotaka kuleta mageuzi ya kweli, hizi ndo sababu zangu kwa nini naanza kuona mwisho mbaya kwa CHADEMA:

  1. Itashindwa kudhibiti hawa watu wanaokimbilia maana ni watu ambao haijawalea, ni sawa na kuchukua mtoto aliyekulia malezi ya wazazi wengine ukataka kumlea wewe, atakusumbua sana sana. Chadema wameweza kuwazibiti kina Zito, Mnyika na wengine kwa sababu wamewalea tokea utoto wao wa kisiasa.

  2. Italeta chuki kwa wanachama ndani ya Chadema ambao wapo muda mrefu maana wengi wa wanaohamia wanataka nafasi za uongozi mfano kugombea ubunge, wale walikitumia chama kwa muda mrefu wanaachwa, hii ni hatari kubwa.

  3. Harufu ya U-CCM haijaondoka kwa hawa wanaohamia, mimi naamini mabadiliko ya kweli yatapatikana kwa kuanza upya na watu wapya wasiokuwa na harufu ya enzi tunazozichukia, hawa wahamiaji wana damu za CCM, wana mitandao yao bado inayowaunganisha. Huwezi kushona nguo mpya ukawa unaiwekea viraka vya nguo ya zamani iliyozeeka.

  4. Chadema kwa kupokea wakimbizi toka CCM itaonekana haina tofauti kabisa na CCM maana watu ni wale wale ila wamekuja upande wa pili na kubadili mavazi yao tu.

  Mwisho nawashauri CHADEMA wawapokee hawa wakimbizi toka CCM ila isiwapatie uongozi bali wawe wanachama wa kawaida na waanzie ngazi za chini kama ilivyo kwa watu wengine wa chini ndani ya chama na si leo tu kahamia kesho anagombea ubunge, kama Chadema wataendelea na tabia hii, basi mie nasema wajiandae kwa kifo cha kisiasa, wao eti wanasema wanapokea watu safi tu kutoka CCM, wanajidanganya sana, haitachukua muda kabla hatujaanza kuona mwisho wa CHADEMA.

  Nawasilisha.
   
 8. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,804
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Hivi Chadema ndio kitu gani hasa.
  .
  "WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
   
 9. buhange

  buhange JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 494
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  CHADEMA ni Alfa na Omega ktk mapinduzi ya siasa ya kweli ktk kupigania haki za walipa kodi, Na bado, 2015 ndo hasa gharika kuu la CCM, Yanayotokea Arusha na maeneo mengine ni mvua za rasharasha. Its total M4C
   
 10. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama umakini wa CDM umepotea katika kupokea wanaoikimbia CCM. Ili CDM ipate ridhaa ya kuongoza nchi inahitaji kukubaliwa kikatiba na wananchi wengi wakiwamo wana-CCM pia. Vilevile CDM bado inahitaji rasilimali watu wenye UZALENDO na wanaoitikia SERA za chama ili kulitumikia taifa kwa uadilifu na tija. Ninaamini kuna wana CCM wazalendo na waliotayari kutumikia Taifa badala ya picha tuliyonayo sote. Umakini katika kupeana majukumu uimarishwe kwa kufuata katiba ya chama pamoja na itelijensia. Ila angalizo lako ni zuri pia.
   
 11. M

  Marytina JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  uongozi wa juu wa chama ndio unaotoa picha halisi ya chama
   
 12. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  chadema sio wajinga,wanafanya vitu kwa makini hata wakiwapokea hao wajinga wa ccm wanajua jinsi ya kudeal nao sio kwamba wataingia kicwakichwa,usiitabirie mabaya
   
 13. s

  schwester Member

  #13
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hilo wazo. Pia lengo si cheo ni kutaka kuangusha chama kwa kupenyeza mambo yao hivvyo wawe makini sana hata kuwapokea. Wanataka kuonyesha na kuwathibitishia wananchi kuwa ni cha kaskazini na udini wakati si kweli tuwe makini hasa kwa wapambanaji wetu wa kweli!
   
 14. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hizi ni nadharia tu ambazo hujazifanyia utafiti yakinifu. Naomba nikuhakikishie tu kuwa Chadema wako makini ktk kila hatua.
   
 15. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kadri kundi la EL linavyozidi kutimkia CDM napata picha moja tu kwamba hata Rostam na kundi lake wanawaza hivyohivyo. Kuna kila dalili ya RA na EL kujiunga CDM.

  My Take
  Kama hayo yakitokea na kwa kwa kweli yanaonekana yakitimia kwa kasi kubwa, tuhuma za ufisadi zilizokuwa zikiielemea CCM sasa zitahamia CDM na CCM kubaki na ushindi wa Mkakati wa kujivua gamba hivyo kuwa chama chenye watu safi.

  Tusubiri tuone.
   
 16. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Kutokana na wimbi la uhamiaji wa makada wa zamani wa CCM ndani ya CHADEMA,chama hicho kikuu cha upinzani nchini hakiko salama.Kuna kila uwezekano kuwa wahamiaji hao,akiwemo Millya wa Arusha,wako kwa maslahi ya CCM.Nimedokezwa na wachambuzi wa mambo kuwa uhamiaji huo una lengo la kukidhoofisha chama cha CHADEMA. 'Wametumwa kupeleleza siri ya nguvu ya CHADEMA,wakimaliza kazi yao watarudi CCM' 'Nani hajui kuwa Millya ni mfuasi nambari moja wa Lowassa? kimeeleza na kuuliza chanzo kimoja toka chama tawala.

  Uongozi wa CHADEMA na uwe macho na makini na wahamiaji hawa.Kamanda Mbowe na timu yako na mnisikie...
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ulaaniwe!
   
 18. Sorrow to Joy

  Sorrow to Joy JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 293
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  katika hali ya kushangaza cdm na wafuasi wake wamekuwa wakiishangilia hatua ya wafuasi wa ccm kukihama ccm na kujiunga na cdm. Kuweni makini, mkuu huyu mtarajiwa wao ameshaona kuwa nguvu yake ndani ya ccm ni kubwa na ana uhakika wa kupitishwa na chama chake kugombea urais 2015. Hofu kuu aliyonayo ni nguvu ya cdm. Mkakati mkuu naouona hapa ni kuwatanguliza hawa mnaowapokea kwa mikono miwili waanze kukidhoofisha cdm taratibu na ikifika 2015 anakuwa na nguvu zaidi ya mnayoiona sasa. Cdm kuweni makini. Msiwaamini hawa watu kamwer. Ni hatari.
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hivi changudoa haolewi? je akiolewa huendela na kazi ya kujiuza?
   
 20. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Abunuasi at work
   
Loading...