Wanaohama CCM ni 'Oil Chafu' - Nape | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaohama CCM ni 'Oil Chafu' - Nape

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DOMA, May 31, 2012.

 1. D

  DOMA JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nape leo ktk East Africa Radio amekaririwa akiwaita watu wanaohama CCM ni sawa na 'Oil chafu' kwani unapoendesha taasisi kubwa kama CCM ni sawa na Gari ambapo hufika mahali huitaji kusafishwa kwa kumwaga oil chafu na kuweka nyingine mpya.

  My take:
  Kama ni hivyo mbona CCM haitafuti wanachama wapya (oil mpya) badala yake hata oil chafu inaisha (wanachawa wa zamani). Je, gari litatembea kweli au ndio kufa tu?
   
 2. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ukizolewa na mto ukiona unyasi karibu yako lazima ukamate ukiamini huo unaweza kukoa.Ndo hivyo lazma watafte kila namna ya kujiokoa lakn mara hii wamekamatwa masaburini kila wakijaribu kujinasua hawawezí
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Oil chafu ni hao waliobakia
   
 4. G

  GALIMA JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  i hate this GAMBA
   
 5. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 930
  Likes Received: 696
  Trophy Points: 180
  Poor Nape! Kila mfano anaoutumia una kasoro kubwa.
  Oil chafu: Maanake ni kuwa hata yeye soon atakuwa oil chafu maana hakuna oil ya kudumu ndanio ya injini. Kinachotokea ni kuwa, oil ya kwanza kuingia kwneye injini inachafuka kwanza na kuondoka na iliyoingia baadaye itafuata ( first in, first out). Kwa hiyo, soon, Nape ataisha kama oil na kuondoka ili oil mpya iweze kuwekwa. Very poor illustration!

  -Au wanachama wanaohama kutoka vyama vingine kwenda CCM, kama ni oil chafu, basi CCM inapokea oil chafu pia. Orodha yao ni ndefu ikiongozwa na Steven Wassira. Ohh kumbe Wassira ni Oil chafu ndani ya CCM! Huyu kijana, reasoning yake ni ndogo sana. Ningeshauri acheze mbali na keyboard ya JF au aache kuongea na wana habari. Kuna siku atamtukana Kikwete.
   
 6. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Alisema "hata wakihama wote atabaki mwenyewe na chama hakitakufa". Huu ni uchizi, sina iman na uwezo wa Nape wa kufikiri hata kidogo!!! Mbona hazungumzi juu ya wanachama wanaohamia(oil mpya)?? Maige kamwambia kuwa yeye ni gamba namba moja. Gamba halijtambua kuwa lenyewe ni gamba!! Kauli kuwa atabaki mwenyewe na ccm haitakufa ni sawa na kusema yeye ni kila kitu pale ccm...!
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Watu hawajifunzi, speech za mbayuwayu nilidhani zimetoa somo lakini naona bado.
   
 8. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Huyu ni kilaza zaidi ya Yusuf Makamba.
   
 9. R

  Roben Member

  #9
  May 31, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yes kasema hivyo.ilikuwa ni capital radio kwenye morning jam.then kasema hawajaanza kuihama ccm leo,kwani hata waanzilishi wote wa vyama vya upinzani walitoka ccm hivyo hashangai kuhama kwao leo!
   
 10. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,649
  Trophy Points: 280
  Nape ni bingwa wa kuokota okota maneno na kuropoka bila kufikiria,
  namshauri akae kimya kuliko anavyoropoka.
   
 11. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,239
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo yeye alivyokuwa na ccj alikuwa grease chafu?
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  huyu kijana hajitambui
   
 13. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Huyu Kijana anaweza kuwa mamluki kweli
   
 14. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nashangaa great thinkers hamjafahamu dhima ya Nape kuwepo kwenye wadhifa ule hadi leo.
  Mnakumbuka 2005 Askofu Kilaini alisema JK ni chaguo la Mungu.
  Mnadhani alikosea?
  La hasha!
  JK aliinuliwa na Mungu kuleta anguko la CCM(kwamba vitaumbwa vipya, na nchi itageuka).
  JK akamuinua mtumishi wa Mungu, kijana Nape Nnauye, aweze kuharakisha anguko hilo la CCM na hivyo nchi hii ya hadi, yenye maziwa ambayo hayajakamuliwa bado na asali ambayo haijarinwa, iweze kupata ukombozi wa pili na kuzaliwa upya bila CCM!
  Lolote ninalosikia Nape kafanya au kunena, namtukuza Mungu na kushangilia ukuu wake.
  Na pindi nchi ikiishakuwa imekombolewa, nashauri Nape na JK wawe miongoni mwa watu muhimu wa kupewa tuzo/nishani maalum kwa kuwezesha hilo kutokea.
   
 15. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wakati uliokamilika ukifika hakuna wa kuuzuia,nape halijui hili hata katibu mwenezi angekuwa Kikwete asingeweza kuuzuia wakati wa CDM,mwache awaite majina yote machafu wanaotoka ccm,wakati unaonesha kwamba waliobaki ccm ni wale walio gizani ndani ya Mwanga wa jua
   
 16. blea

  blea JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Vipi tena jamani tunaitana majina ya ajabu ajabu. Ni vyema bro utafute mtu atakaekua anaedit speech zako kwani naona sasa unakoelekea siko. Wewe ni kiongozi wa chama uliepewa dhamana na wanachama kuwa katibu wao sijui wa nini vile LEO HII WANAKERWA NA MAOVU YA VIONGOZI WA SERIKALI WANAONDOKA NA kujiunga na vyama vingine unawaita oil chafu. HIVYO unataka tuamini ndivyo ulivyo?
   
 17. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu Baija Bolobi,
  Kama ni nyoka basi umempiga kichwani. Heshima mbele!

  TUMBIRI (PhD, Hull University - UK),
  tumbiri@jamiiforums.com
   
 18. U

  Uswe JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  utakua umesahau hii, hebu soma hii kuhusu nape kumshukia JK

  Nape amgeukia Kikwete | Gazeti la MwanaHalisi
   
 19. U

  UmtwaAlumbwagwe Member

  #19
  May 31, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Binafsi naona mdogo wangu Nape anachoongea kina hekima sana ila cc ndo tunakuwa wagumu kuelewa. Ukiona mtu anamwaga oil ya zamani bila kuongeza nyingine na anaendelea kulitembeza hilo gari, tambua ana nia mbaya ya kuliua na mwenye gari lake asipo tambua mapema atakuta gari limekufa. MWENYE GARI ni KIKWETE na NAPE ni DEREVA asiyelitakia mema gari alilokabidhiwa. Nape mimi nimekuelewa vizuri. Nakutakia ukamilishe salama huo mpango wako.
   
 20. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #20
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nape amgeukia Kikwete

  [HR][/HR]
  [​IMG]
  Na Jabir Idrissa - Imechapwa 13 July 2011

  [​IMG][​IMG][​IMG]  NAPE Nnauye, katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amemjia juu Rais Jakaya Jakaya Kikwete na kusema, “ni sehemu ya chimbuko la migawanyiko inayokikumba chama chake,” imeelezwa.

  Amesema, “Pamoja na kwamba hatuwezi kumwajibisha mwenyekiti kwa sababu ni wajibu wetu kulinda hadhi yake, lakini naye hawezi kujinasua katika tuhuma za kuvurugika kwa chama chetu hadi kufanya vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita.”
  “Ni kweli ndani ya CCM hakuna umoja kwa sasa. Sehemu kubwa ya migawinyiko hii imesababishwa na Rais Jakaya Kikwete mwenyewe. Mtandao wake uliomuingiza madarakani ndio umekivuruga chama hiki. Sasa ili tukinusuru, sharti wote waliohusika na kukivuruga chama chetu waondoke.”

  Nape alitoa matamshi hayo ya kwanza kusikika kwa kiongozi aliyepo ndani ya usukani wa uongozi wa chama, Jumatano iliyopita alipotembelea chumba cha habari cha kampuni ya New Habari Corporation inayochapisha magazeti ya Rai, Mtanzania, Bingwa, Dimba na The African. Kampuni ya New Habari Corporation Limited, inamilikiwa na Rostam Aziz, mmoja wa watuhumiwa watatu wa ufisadi wanaotakiwa na CCM kuachia uongozi. Wengine ni Edward Lowassa na Andrew Chenge.

  Katika ziara hiyo, Nape alikutana na mtendaji mkuu wa New Habari, Hussein Bashe na baadhi ya wahariri wa magazeti ya kampuni hiyo.
  Mjadala wa mtandao kuvuruga chama, taarifa zinasema, uliibuliwa ndani ya mkutano na waandishi ambapo Nape alijitosa kuushambulia mtandao wa Kikwete akisema, “ndiyo chanzo cha CCM kufika hapa kilipo.”

  Akimgeukia mwenyeji wake alisema, “Wewe Hessein (Hussein Bashe) unafahamu jinsi mtandao wenu ulivyokivuruga chama hiki. Ulikuwa mwanachama wa kundi hilo, unafahamu mlichokitenda. Kama kweli tunataka kukinusuru chama hiki, ni sharti wote waliohusika na mtandao, waachie ngazi.”

  Hata hivyo, MwanaHALISI lilipowasiliana na Nape kufahamu undani wa alichokisema aling’aka, “Najua kuna watu wanataka kupika maneno ili kutekeleza mkakati wao wa kunichafua kutumia baadhi ya waandishi wa habari na vyombo vyao vya habari.” Nape hakutaja anaosema wana mkakati wa kumchafua.

  Lakini amekiri suala hilo lilizungumzwa katika mkutano huo, bali alisema, “Suala hilo lilitokana na maoni ya mmoja wa waandishi wa magazeti hayo.” Alisema, “Sitaona tabu kuchukua hatua nikihisi nimelishwa maneno, maana tumerekodi kila kitu,” alieleza.
  Hata hivyo, MwanaHALISI lina uhakika kwamba suala la mtandao lilijadiliwa kwa kina kati ya wahariri wa New Habari Corporation, Nape na Bashe.

  Alisema, “Mimi nafahamu kila nilichozungumza. Siamini kama rais anahusika au ana mchango wowote katika hili…Kama ingekuwa hivyo basi tusingemsikia akikemea migawanyiko ndani ya chama.”Alisema, “Ndiyo maana kwa kuhofia mkakati wa kunichafua, kila ninapopita narekodi mazungumzo yetu na wahusika. Nilipokuwa New Habari, tulizungumza kwa uwazi, lakini Bashe alipokuwa anazumgumza ya kwake, ndiyo akawaambia waandishi wake watoke, lakini mimi maofisa wangu walikuwapo”.

  Mhariri mmoja mwandamizi wa magazeti hayo ameliambia gazeti hili, “Bashe na Nape wamezungumza mambo makubwa sana, ambayo kawaida yasingejadiliwa katika mkutano wa aina ile. Ni vema wangekutana faragha kuliko kueleza yale kwa kisingizio cha off record.”
  Naye Bashe alipoulizwa juu ya suala hilo, haraka alihoji, “Hizo habari mmezipata wapi?” Alipoelezwa zimetoka ndani ya chumba chake cha habari, kwanza Bashe alishusha pumzi na kisha akasema, “Tuacheni jamani. CCM ina matatizo mengi na tunakoelekea ni kugumu.”
  Akiongea kwa njia ya kusisitiza, Bashe alisema, “Kaka, kaka, kaka, nakuomba niko chini ya miguu yako, tuna matatizo mengi yanatutosha. Tunapitia katika wakati mgumu. Mkiandika haya mtatuweka pabaya…”

  Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, Nape alisema ni mtandao wa Rais Kikwete uliofanikisha mkakati wake wa kuingia ikulu mwaka 2005 ambao umesababisha matatizo na kudhoofisha umoja ndani ya CCM. Nape amenukuliwa akisema, “Chama hakina umoja. Kimeuawa na mtandao; bali pamoja na hayo, hatuwezi kumbebesha mzigo huu mwenyekiti peke yake; lakini naye ni sehemu ya tatizo lililopo ndani ya chama. Ili tuweze kuondoka hapa tulipo sharti yeye na wenzake, Lowassa, Rostam na wengine waachie ngazi.”Hata hivyo, Nape alisema kwa kuwa Kikwete ndiye mwenyekiti wa chama na rais wa nchi, haiwezekani kumbebesha mzigo huo. Akatoa mfano wa John Malecela alipojiuzulu kwa kubariki kuwapo kwa serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano, akisema “Huwezi kusema yale yalifanyika bila baraka za Mzee Mwinyi (rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi).”

  Mtoa taarifa anasema wakati Nape alikuwa akimtaja Rais Kikwete kama sehemu ya mgawanyiko ndani ya chama, Bashe yeye alikuwa akituhumu viongozi wapya wa sekretarieti ya CCM walioteuliwa katika mabadiliko ya Aprili mwaka huu, kwa kusema wanakipeleka chama hicho mahali siko kutokana na kusimamia kaulimbiu ya “kujivua gamba.”Imeelezwa kuwa Bashe alithibitisha katika mjadala huo kuwa ni kada aliyepo kundi la kina Lowassa, Chenge na Rostam.

  Awali Nape alimtuhumu Bashe kwamba amekuwa akitetea watuhumiwa hao watatu ambao chama kilishaelekeza wajivue uongozi wa chama ili kukirejesha katika umoja wake. Lakini Bashe akijibu hoja ya Nape, pamoja na kukiri kutetea wanaoitwa na CCM kuwa “mafisadi,” alipinga wazo la kuwafukuza watuhumiwa hao kwa madai kwamba matatizo ya CCM hayawezi kumalizwa kwa njia hiyo.
  Alisema, “Nape, mnachokifanya ni unafiki na hakiwezi kumaliza matatizo yetu. Tutaendelea kutafunwa na makundi hadi tumalizike.”
  Kufika hapo, ndipo Nape akasema, “…Wote wana makosa na kama tunataka kuokoa hiki chama, hatuwezi kurudi nyuma. Ni lazima waondoke.”

  Kuhusu hilo, Bashe ameripotiwa kusema, anachokifanya Nape ni kutaka kuingiza mgombea wake ikulu mwaka 2015. Naye alijibu kuwa ana msimamo, hayumbi kwa analolisimamia. Mwaka 2005 Nape anatajwa kuunga mkono Profesa Mark Mwandosya katika uteuzi wa ndani ya chama. Nape hakuishia hapo. Aligusia hata mwenendo wa uchaguzi ndani ya Umoja wa Vijana (UV-CCM), kwamba alimuunga mkono Bashe ambaye aliamini kuwa ni mtu huru, lakini alipobadilika alimpinga katika harakati zake za kuwania ubunge jimbo la Nzega.
  Alisema “Mimi sifichi ninachokisimamia. Inawezekana maamuzi tulikosea, lakini sharti twende mbele. Katika uteuzi wa ubunge jimboni Nzega, nilikupinga. Nilimuunga mkono Lucas Selelii.

  Akiongea kwa sauti ya upole, Bashe alisema, “Tunakuwa wanafiki. Kila mtu amebeba briefcase (mkoba) yake yenye wagombea.”
  Bashe aliendelea kusema kuwa kuwatuhumu Lowassa, Rostam na Chenge ni kuwaonea kwa kuwa karibu viongozi wote wa CCM ni wachafu. Vyanzo vya taarifa vinasema Bashe alimwambia Nape, hoja ya ufisadi si agenda ya CCM. Ni agenda ya upinzani, hususani Chadema. “Siku zote tumekuwa tukitetea kwamba ndani ya chama chetu hakuna ufisadi. Sasa tumetangaza tunao mafisadi. Tukimaliza hili, wananchi watatuuliza, je, ‘mafisadi’ ni hawa watatu tu?,” aliuliza. Akitetea watuhumiwa hao watatu, Bashe alisema, “Hatujadili mambo ya msingi, kwanini? (Hii) ni hoja ya Chadema.”Bashe alinukuliwa akizidi kujenga hoja yake kwa kumuuliza Nape kama katika tuhuma za rushwa ya rada, mtuhumiwa ni Chenge peke yake. Bashe alikaririwa akilaumu namna serikali inavyoshindwa kutazama hali za wananchi masikini kufuatia kitendo chake cha kuachia ushuru wa kiwango cha juu wa petroli uwiane na ule wa mafuta ya taa, nishati inayotegemewa na sehemu kubwa ya wananchi masikini.

  Akionyesha athari za matatizo ya msingi yanayokabili uongozi wa juu wa CCM na kuathiri utendaji wa serikali, Bashe alisema, “Tumepandisha bei ya mafuta ya taa kwa sababu ya kudhibiti petroli. Mnakiri udhaifu wa serikali kuumiza wananchi?” “Turudi chini. Kutoka asilimia 80 tumepata asilimia 61 kwa sababu ya makosa, vidonda vya kura za maoni na wagombea wasiofaa. Haya ndiyo matokeo ya makosa yetu katika chama,” alinukuliwa Bashe akilalamika kama kuonea huruma chama.
   
Loading...