Wanaogopa kujitokeza hadharani kuunga mkono mapambano, ila wanajiandaa kushangilia matokeo hadharani!

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
9,757
2,000

Na: Emmaus Bandekile Mwamakula


Hawa wako wengi sana! Wengine niliwahudumia wakiwa mashuleni kwa zaidi ya miaka 18 nilipokuwa nahudumia wanafunzi nchini; wengine niliwafundisha Chuo Kikuu, St. John's University of Tanzania kwa zaidi ya miaka 9; wengine tulisoma nao Itunge, Kipawa, Azania na IFM; wengine tulifundisha nao Chuo, wengine ni ndugu, jamaa na marafiki; wengine ni majirani katika maeneo yote niliyowahi kuishi katika Wilaya za Kyela, Ubungo, Temeke, Ilala na Kinondoni! Wengine ni Wachungaji na Maaskofu, na wengine ni ma-ulamaa, mashehe na hata maimamu! Wapo watumishi wa Serikali na wamo wafanyabiashara na wajasiliamali! Nasikia kuwa waalimu ndio wengi zaidi! Wengine wengi ni Watanzania wasionijua ila wamesikia mapambano na harakati zangu za kupigania Haki!

Wengine ni Usalama wa Taifa na wengine ni wafuasi wa CCM wakiwemo wastaafu waliotumikia CCM na serikali zake zote! Wengine ni ndugu wa waathirika wa vyeti feki na wengine ni wahanga wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Nimeambiwa pia wengine ni Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Tanzania. Nimeambiwa pia kuwa Wanajeshi ndio wengi zaidi kuliko hata Polisi.

Wote hao wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na Askofu Mwamakula na watu wengine katika kutetea Haki, Tume Huru, na Katiba Mpya. Ila hawawezi kusema hadharani kwa kuhofia nafasi zao, mahusiano na hata maisha yao. Wanabaki kunong'ona katika familia zao au katika makundi ya watu wawili wawili. Wapo wanaoogopa hata kumtembelea Askofu ila hutuma ujumbe kupitia watu wanaowaamini wakisema Askofu asirudi nyuma na kwamba 'akamatie hapohapo'!

Siku moja nilikutana na Mwandamizi mmoja wa TISS alipokuwa akitokea Dodoma! Alishuka kutoka katika "chuma" lake jeusi, akanisalimia na kusema ananisoma kila siku na kwamba nisikate tamaa! Alisema kuwa wapo wengi wa aina yake hata ndani ya TISS.
Makundi yote haya wanajiandaa kusherekea ushindi kuliko hata walio mstari wa mbele katika mapambano.

Wapo ambao baada ya ushindi watajitokeza kuonyesha kuwa wanatujua zaidi na kutusifia hadharani. Watafufua hata picha tukizowahi kupiga nao au matukio ya nyuma ya kuonyesha jinsi wanavyotufahamu! Lakini kwa sasa hawawezi! Wamejawa na hofu ya kuogopa kupoteza hayo wanayoyadhani kuwa ni ya muhimu kwao kwa sasa! Kuongozana na kujitambulisha na sisi ni hatari kubwa! Majina yetu yanawakilisha hatari kwa watawala! Majina yetu yamepakwa kinyeshi na wapambe wa watawala! Lakini siku moja majina yetu yatakuja kuwa manukato nzuri na ghali kuliko vito vya thamani!

Jeuri yetu haipo katika makundi yanayotuunga mkono! Jeuri yetu ipo katika YEYE aliye HAKI (Zaburi 121). Huyo ndiye msaada, ulinzi na kimbilio. YEYE ni zaidi ya TISS, KGB, Scotland Yard, CIA, Mossad, nk.

Ninaendelelea kukualika katika Matembezi ya Hiyari na ya Amani nitakayoyaongoza nchi nzima kuanzia Januari 2021 kwa lengo la kuhamasisha Kuundwa kwa Tume Huru na Kuandikwa kwa Katiba Mpya!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.

Image may contain: one or more people, people dancing, people standing and people on stage
 

Mndali ndanyelakakomu

JF-Expert Member
Dec 14, 2016
13,061
2,000
Ibada ya wanafiki huisha kwa unafiki

Ibada ya wenye haki huisha kwa kubarikiwa

Ni vibaya kutumia madaraka yako kama ngao ya fikira zako

Ni vizuri kusimama upande uliopo kuliko kusimamia kivuli chako

Siasa ni ajira

Ukristo ni upendo

Uislamu ni upendo

Tuzidi kupendana maana ibada ya haki huabudiwa na wenye haki
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,021
2,000
Pambana baba askofu. Huyu mkandamiza haki na mtoa roho za wakosoaji kiukweli amefanikiwa kuwajengea hofu watanzania. Ndiyo maaana watu wananong'ona. Wanaogopa!
 

Kitwa-Mulomoni

JF-Expert Member
Oct 25, 2016
1,631
2,000
Askofu, uliyoandika na watu ulio wataja, ndiyo hesabu ya kura mlizo pata! 84% ya kura za Magufuli ni za wale ambao hukuwataja! Mnaungwa mkono na wananchi wachache, na hao utakuta ni wale disgruntled! Kwa mfano uliowataja wa vyeti hewa. Je hao ni wangapi? Na number za walimu, TISS, askari etc. wanaokusuport ni ndogo na jumla ni hiyo mliyopata! Mbona mwenzio (Lissu) amekubali kwamba watanzania hawakuwapa kura wapinzani! Eti haja amuka!

Halafu askofu unajuwa wewe unatumia rushwa kutaka ukubaliwe hizo fikra zako potofu - mfano siku moja ulikutana na mwandamizi mmoja wa TISS- hapo unaitumia hiyo TISS kuvunga watu waone na vyombo vya usalama vinakusupport. Rushwa nyingine ni pale ulipo tumia YEYE aliye HAKI (Zaburi 121)! Hivi mungu ni wenu wapinzani siyo wa CCM pia? Mbona hatujaona mungu anapowapendelea nyie kwenye siasa hizi? Kwa rushwa hii ni wachache watakusupport, hivyo % ge ya kukubalika itabaki ndogo.

Badilika unachotea maji kwenye tenga! Watanzania wanamjua atakaye wavusha, ni Pombe Joseph Magufuli.
 

Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
1,627
2,000
Askofu, jitahidi uombe au uhakikishe unapigania Katiba Mpya ambayo itaangalia haki na tume bora ya uchaguzi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom