Wanaofikiria kuhusu uwepo wa Level Seat katika daladala sio watumiaji wa usafiri huu

Chomo

JF-Expert Member
Mar 29, 2017
236
616
Wakuu,

Kumekuwa na tetesi na minong'ono miingi siku za karibuni kuhusu utumiaji wa usafiri wa umma (daladala), abiria wapande level seat lakini nimesikia huko Dodoma agizo limeshatoka tayari.

Turudi nyuma kidogo,ambapo mwaka jana tukiwa katika hali kama hiyo, ikumbukwe shule zilikua zimefunga pamoja na huduma za kijamii nyingi hazikufanya kazi katikamuingiliano wa kawaida.

Inakuaje sasa tuwaze hayo ilhali tupo katika maisha ya kawaida ya ufanyaji kazi,ka uwingi huu wa watu ni kusababisha taharuki isiyokuwa na tija.

Hiyo mwaka jana kwanza soko la mafuta lilishuka mpk kuuzwa lita 1400, na ilikua ni kawaida sababu hakukua na watumiaji wengi wakia self isolated.

Leo hii dunia inarudi normal na kuanza kulegeza baadhi ya masharti ya covid 19 eti sie ndo tunakumbuka kurudisha,ikiwa bei ya mafuta imepanda mpk 2400 kwa lita.

Ni boss gani atakubali ashushe posho ya siku mpk elfu 50 kama ilivo mwaka jana na ikiwa mafuta ni bei juu?

Kumekuwa na baadhi ya waandishi wa habari wanachochea hili,nadhan sio watumiaji na hawajui adha ya usafir huu..

Nawakumbusha tu wajue shule zinapokua katika matumizi,hata uhitaji wa huduma ya usafiri huu huwa ni mkubwa zaidi,ivo waangalie upya wanalotaka kufanya
 
Kama wewe unavyoita level seat au watumiaji kuvaa barakoa kuhami maisha ya watu kwanini isiwezekane?
 
Hili jambo linawezekena. Dunia ya sasa imestaarabika. Wala siyo corona tu lakini kuna magonjwa mengi sana yanayoweza kuambukiza kwa sababu ya kujaza kupita kiasi.
 
Kama wewe unavyoita level seat au watumiaji kuvaa barakoa kuhami maisha ya watu kwanini isiwezekane?
mpk sasa bado uhitaji wa huduma ni mkubwa sana,gari inapanfisha abiria kwa kujaza na bado haitoshi,hyo level seat inawezekana vip?
 
mpk sasa bado uhitaji wa huduma ni mkubwa sana,gari inapanfisha abiria kwa kujaza na bado haitoshi,hyo level seat inawezekana vip?
"... au watumiaji kuvaa barakoa .." Maisha ni lazima kuyalinda.
 
Hili jambo linawezekena. Dunia ya sasa imestaarabika. Wala siyo corona tu lakini kuna magonjwa mengi sana yanayoweza kuambukiza kwa sababu ya kujaza kupita kiasi.
hyo dunia ya wenzetu wametuacha mbali,na mfumo haukuja ghafla tu kuna maeneo mengi yameangali ikiwa ni suala la shule,ni wanafunzi wangapi wanaruhusiwa kupanda daladala? konda anaweza kuruhusu wapande watano wakalie siti walipe 200..? na mafuta bei ya 2400?
 
Mkuu kwanza nakudiss kwa kuandika hovyo.

Pili natala kukukumbusha kuwa haya magari ya abiria yalitengenezwa maalum kabisa kiwandani kwaajili ya kubeba watu kulingana na idadi ya seats zilizopo.

Maana yake ni kuwa kisheria hairuhusiwi kusimamisha abiria (labda kwa muundo wa magari ya mwendokasi tu) katika hizi daladala. Iwe ni kipindi hiki cha covid au kipindi kingine chochote.

Tatizo ni mifumo yetu ya uongozi iliyojaa rushwa ndio inapelekea mpaka makosa ya kuvunja sheria na kuhatarisha usalama wa raia na mali zao yanazoeleka katika jamii kana kwamba ni mambo ya kawaida.

Yani mtu unaandika uzi kabisa kudai/kutetea jambo ambalo kimsingi ni uvunjifu wa sheria za usalama barabarani.
 
kuandika sio kipaji changu..ungeangaliwa mfumo kwanza unataka nn ndio hilo lifikiliwe,kama ni mtumiaji wa daladala utajua adha tutakayokutana nayo..kkoo buza nauli ilikua 800 mwaka jana..alaf isitoshe watumiaji walikua ni wachache tofaut na ilivo sasa
 
Back
Top Bottom