Wanaofanyakazi ya kupamba kumbi za starehe, kusherehesha (Ma-MC), wapishi wa sherehe na wapiga picha, watatakiwa kulipa ada na ushuru

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
WATU wanaofanyakazi ya kupamba kumbi za starehe, kusherehesha (Ma-MC), wapishi wa sherehe na wapiga picha, watatakiwa kulipa ada na ushuru.

Ni baada ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema jijini Mwanza, kupitisha sheria ndogo za ada na ushuri ambazo tayari zimepata baraka za Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Barua iliyosainiwa na Emmanuel Kaponoke, Afisa Utamaduni wa halmashauri hiyo ya tarehe 15 Januari 2021 kwenda kwa walengwa, inabainisha ada hizo.

Washereheshaji (MC) watapaswa kulipa Sh.50,000 kwa sherehe moja huku wapambaji kumbi za burudani/sherehe watalipa Sh.30,000.

Wamiliki wa kumbi, unaochukua watu kati ya 100-200 ni Sh.50,000 kwa siku, ukumbi unaochukua watu kati ya 201-500 atalipa Sh.100,000.

Wapishi wa vyakula kwa siku moja ya tukio atapaswa kulipa Sh.30,000 na wapiga picha za video na mnato watapaswa kulipa Sh.30,000 huku muziki ikiwa ni Sh.30,000

“Kamwe, mmiliki wa ukumbi asiruhusu sherehe kufanyika ndani ya ukumbi wake bila kibali cha halmashauri,” inaeleza sehemu ya barua hiyo

“Ikumbukwe, ada hii ni kwa ajili ya kubali cha halmashauri tu na si gharama ya kukodi ukumbi.”

EsMpMZdW4AIPxcT.jpeg
 
Hii serikali sasa haitaki mtanzania abaki na chochote mfukoni, wanajiita serikali ya wanyonge kumbe ndio wanatufanya tuwe wanyonge kwa lazima?

Nikadhani wakijiita serikali ya wanyonge maana yake wanatusikiliza wanyonge kero zetu na kuzifanyia kazi, kumbe I was wrong in interpretation of that word "wanyonge"

Hakika wanatunyonga.
 
Waongeze na tozo ya parking 100,000/= kwa kila tukio

Tozo ya mazingira (uchafu/pollution) 100,000/=

Tozo ya kuacha kufanya kazi na kwenda kwenye sherehe 200,000/= kwa kila tukio.

Nasema uongo ndugu zangu ?
Jamaa wanazingua kwakweli
 
Bado kuna tozo ya kulipia makazi ndani ya hifadhi tengefu zilizo chini ya Buhindi tunalipia kwa kila hatua shilingi elfu moja kwa mwaka. MITANO TENA!
 
Tukikusanya kias kisitosheleze basi.

Vi carry (kirikuu) vya kubeba vyombo vya muziki wajiandae 30000

Wabeba mapambo pikipiki ya miguu mitatu 20000

Wabeba camera za picha za mnato na jongefu (bodaboda)5000.

Mpk makasi tawatoke miaka hii.
 
Tatizo watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia
Tii sheria bila shuruti
Lipa kodi
Utafaidi matunda ya awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake
Vinginevyo utaumia sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
Sasa huyo mc analipwa 50k tozo yake sasa atoe 50k abaki na nini?

Wapishi wanalipwa mpaka 70k sasa tozo 30k mnataka nn nyie maCCM?

Hapo mwenye ukumbi ashalipa kodi na tozo nyingine
 
Hawa watu hawana akili kabisa sengerema ni wilaya ndogo sana kuna ukumbi gani pale mwenye ukumbi atoe 220,000 au 270,000 kwa ajili ya halmashauri?

Sengerema asili yake ni wasukuma na wasukuma wengi wanapenda kufanyia sherehe zao manyumbani au kwenye jamii yake.Anyway sasa hivi sherehe tutakuwa tunafanyia makanisani na penyewe waje wadai kodi.

Mfumo mbovu kabisa wa kutafuta mapato..sasa hivi kijana kuoa inakuwa adhabu.
 
Sasa huyo mc analipwa 50k tozo yake sasa atoe 50k abaki na nini?
Wapishi wanalipwa mpaka 70k sasa tozo 30k mnataka nn nyie maCCM??
Hapo kanla mwenye ukumbi ashalipa kodi na tozo nyingine
Mkuu Yaani wewe Tii sheria za nchi bila masharti
Lipa kodi
Utafaidi sana
Vinginevyo utaumia maana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
 
Hawa watu hawana akili kabisa sengerema ni wilaya ndogo sana kuna ukumbi gani pale mwenye ukumbi atoe 220,000 au 270,000 kwa ajili ya halmashauri?
Sengerema asili yake ni wasukuma na wasukuma wengi wanapenda kufanyia sherehe zao manyumbani au kwenye jamii yake.Anyway sasa hivi sherehe tutakuwa tunafanyia makanisani na penyewe waje wadai kodi..
Mfumo mbovu kabisa wa kutafuta mapato..sasa hivi kijana kuoa inakuwa adhabu..
Ni wakati wa kujifunga mkanda
 
Back
Top Bottom