Wanaoendelea kujadili EPA wameishiwa hoja

Kitia

JF-Expert Member
Dec 2, 2006
418
74
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Bw. Yusuph Makamba, amesema wapinzani na watu wanaoendelea kujadili suala la ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje, EPA na Richmond kila kukicha ni dalili kuwa watu hao wamenyang`anywa hoja za kuzungumza.

Bw. Makamba alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na viongozi wa CCM Mkoa wa Tanga mara baada ya kuwasili mjini hapa kwa ziara ya siku mbili kuhamasisha uhai wa chama hicho.

``Kama mnavyosikia kwenye vyombo vya habari kila siku mara ufisadi, Richmond na EPA hizo ni kelele mnazozisikia, ni kelele zinazotolewa na watu walionyang`anywa hoja ni wimbo unaoimbwa na wapinzani, hawana wimbo mwingine,`` alisema Bw. Makamba.

Alisema hakuna haja kwa wapinzani kuendelea kujadili masuala hayo wakati serikali imeanza kuchukua hatua na kwamba Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda ameahidi kutoa taarifa ya EPA mara baada ya tume iliyoundwa na Rais kukamilisha kazi yake.

Katibu Mkuu huyo alisema mara baada ya suala la ufisadi, EPA na Richmond kuibuka Bungeni, Rais Jakaya Kikwete aliamua kuunda tume inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambayo itakamilisha kazi ya uchungunzi Julai mwaka huu.

Akiongea na Nipashe kuhusu hoja hiyo ya Makamba kuwa wanaoendelea kuzungumzia EPA na Richmond wamefilisika hoja, Dk. Slaa alisema kwa sasa CCM iko kitanzini.

Alisema Bw. Makamba hana jipya la kuwaeleza Watanzania kwani kama ilivyo kawaida yake amekuwa akiendekeza porojo za siasa.

Alisema Watanzania wanapaswa kuiuliza CCM na serikali yake waeleze ukweli kuhusu fedha zilizoibwa Benki Kuu ya Tanzania.

``Tumetoa hoja na vielelezo vinavyojitosheleza sio porojo kama za Makamba. CCM waeleze fedha za wananchi zimekwenda wapi na tukiendekeza porojo za siasa kama CCM inavyofanya, nchi hii haitaendelea,`` alisema.

* SOURCE: Nipashe
 
HIvi huyu mzee ana akili timamu au?au anayaongea haya maneno kwa kuwa watoto wao wako kwenye nafasi nzuri za kazi au?niashindwa kumwelewa kabisa.yani kuongelea sualala epa ni kuishiwa hoja?kweli kadata na anahitaji kupumzishwa kisiasa
 
Sasa uyo mzee hamuoni kama ameshakufa ,unajua inawezekana ikawa unatembea na maiti lakini hujui ,makamba ni kibudu maana kuweko kwake hapo kwenye ngazi ya Ukatibu hakuna faida yeyote wala hana hadhi ya kuamua jambo kama katibu hana tofauti na wapiga debe wengine au mazungumzo yake yanachukuliwa kama mazungumzo ya gengeni.Makamba kama katibu wa Chama ni msimamo gani ametoa dhidi ya wabunge waliotuhumiwa na mambo ya ufisadi na kufika kujiuzulu mbona hajawachululia hatua za kinidhamu kwa kukiaibisha Chama Chao , hakuna lolote alilosema anasubiri wapinzane waseme ndio yeye apate kauli ,na kama kweli ukatibu wake una hadhi na kuthaminiwa basi awasulubishe na kuwawajibisha waliohusika na ufisadi ili kulinda heshima ya Chama ,sio kurukia vyama vyengine juwa havina sera au vimeishiwa na sera,watu hawajaishiwa na sera ila hii sera ya kuwakurupusha mafisadi katika hazina ya Taifa bado haijakamilishwa hivyo atulie asubiri kufa kihoro.
 
Huyu Makamba msameeni kwa bure bure kabisa, jamani si mnajua yeye ni mzee wa kusema chochote wakati wowote bila kufikilia lolote linaloweza tokana na kaulizake?

Afu anadhani bado watz tuko mwaka 47 wa ndiyo mkuu kasema. nooooo! not anymore.
 
haiwezekani kabisa...mii nadhani magazeti yanawaquote vibaya hawa watu...haiwezekani namna hii...anasimamaje na kusema watu wamekosa hoja??? kama sio hoja za kuzungumzwa mbona hawatoie maelezo makini wanajikanyaga kanyaga na kuropoka ovyo bila dire?
 
Watu wakinyamaza wataona wameshinda nawatazidi kufanya madudu yao. Hakuna kulala mpaka kieleweke. Na kama atafikiri huo uongo wa Pinda utanyamazisha watu he is very mistaken
 
Kumbe ndicho kinafanya CUF wamwite darasa la 4,Muafaka ulimshinda kwa kauli hizo hizo za kukurupuka,hii si kauli ya Katibu mkuu aliye mahiri na makini kutumikia Taifa.Akajiunge na Chitaliho ili waropokaji wawe wengi
 
Zamani Kusingaliko Elimu, Mvi Zilihesabika Kama Busara, Kwa Sasa Kungalipo Elimu, Kamwe Mvi Haiwezi Kuhesabu Busara Aliyo Nayo Mtu-nukuu Isiyo Rasmi Toka Kwa Shaban Robert
 
Huyu Mzee hastahili kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi kumi achilia mbali kuwa katibu mkuu wa CCM. CCM imefilisika inakosa hata viongozi wenye uwezo wa kuchanganua mambo na kujua umuhimu wake kuhusiana na Taifa letu.
 
Back
Top Bottom