Kitia
JF-Expert Member
- Dec 2, 2006
- 418
- 73
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Bw. Yusuph Makamba, amesema wapinzani na watu wanaoendelea kujadili suala la ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje, EPA na Richmond kila kukicha ni dalili kuwa watu hao wamenyang`anywa hoja za kuzungumza.
Bw. Makamba alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na viongozi wa CCM Mkoa wa Tanga mara baada ya kuwasili mjini hapa kwa ziara ya siku mbili kuhamasisha uhai wa chama hicho.
``Kama mnavyosikia kwenye vyombo vya habari kila siku mara ufisadi, Richmond na EPA hizo ni kelele mnazozisikia, ni kelele zinazotolewa na watu walionyang`anywa hoja ni wimbo unaoimbwa na wapinzani, hawana wimbo mwingine,`` alisema Bw. Makamba.
Alisema hakuna haja kwa wapinzani kuendelea kujadili masuala hayo wakati serikali imeanza kuchukua hatua na kwamba Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda ameahidi kutoa taarifa ya EPA mara baada ya tume iliyoundwa na Rais kukamilisha kazi yake.
Katibu Mkuu huyo alisema mara baada ya suala la ufisadi, EPA na Richmond kuibuka Bungeni, Rais Jakaya Kikwete aliamua kuunda tume inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambayo itakamilisha kazi ya uchungunzi Julai mwaka huu.
Akiongea na Nipashe kuhusu hoja hiyo ya Makamba kuwa wanaoendelea kuzungumzia EPA na Richmond wamefilisika hoja, Dk. Slaa alisema kwa sasa CCM iko kitanzini.
Alisema Bw. Makamba hana jipya la kuwaeleza Watanzania kwani kama ilivyo kawaida yake amekuwa akiendekeza porojo za siasa.
Alisema Watanzania wanapaswa kuiuliza CCM na serikali yake waeleze ukweli kuhusu fedha zilizoibwa Benki Kuu ya Tanzania.
``Tumetoa hoja na vielelezo vinavyojitosheleza sio porojo kama za Makamba. CCM waeleze fedha za wananchi zimekwenda wapi na tukiendekeza porojo za siasa kama CCM inavyofanya, nchi hii haitaendelea,`` alisema.
* SOURCE: Nipashe